Kauli ya kejeli ya mtangazaji tbc1 noel mwakalindile juu ya mabomu ya gongo la mboto

magessa78

JF-Expert Member
Sep 28, 2009
270
31
Jana saa 2 usiku taarifa ya habari tb-ccm1 nimeshangazwa na kauli ya mtangazaji wa kituo hicho akitoa kejeli akifananisha mizinga 21 iliyokuwa inapigwa uwanja wa ndege ktk ziara ya rais wa somalia, na mabomu yaliyolindima gongo la mboto yaliyoua watu miezi mitatu ulopita. Awaombe radhi wana gongo la mboto kwa kejeli hii.
 
Hata mimi nilisikitishwa sana na kauli ile na bado kwa jinsi TBC isivyo makini bado waliirusha hewani. Uongozi wa TBC unapaswa kuwaomba radhi waliofikwa na dhahma ile Gongo la mboto.
 
Jana saa 2 usiku taarifa ya habari tb-ccm1 nimeshangazwa na kauli ya mtangazaji wa kituo hicho akitoa kejeli akifananisha mizinga 21 iliyokuwa inapigwa uwanja wa ndege ktk ziara ya rais wa somalia, na mabomu yaliyolindima gongo la mboto yaliyoua watu miezi mitatu ulopita. Awaombe radhi wana gongo la mboto kwa kejeli hii.

sioni kosa mkuu au una lako jingine kaka!
 
Jana saa 2 usiku taarifa ya habari tb-ccm1 nimeshangazwa na kauli ya mtangazaji wa kituo hicho akitoa kejeli akifananisha mizinga 21 iliyokuwa inapigwa uwanja wa ndege ktk ziara ya rais wa somalia, na mabomu yaliyolindima gongo la mboto yaliyoua watu miezi mitatu ulopita. Awaombe radhi wana gongo la mboto kwa kejeli hii.

Nafikiri tafsiri yako ndo mbaya kwani umepelekea kwenye kejeli. Yeye alikuwa analinganisha tu na pengine kama kujombeza katika kipindi. Sioni kosa hata mimi.
 
Kwa tafsiri yako unamaanisha mtangazaji alikuwa akiwajulisha wananchi wa gongo la mboto kuwa mabomu yalilipuliwa na siyo kulipuka kwa bahati mbaya?
Gongo la mboto walikuwa wakipewa heshima ipi? au maafa ni heshima?
Nawakilisha.
 
Back
Top Bottom