Kauli ya katibu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni kuhusu vitendo vya polisi kwa raia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli ya katibu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni kuhusu vitendo vya polisi kwa raia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Zak Malang, May 24, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  KAULI YA KATIBU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSU

  VITENDO VYA JESHI LA POLISI KWA RAIA

  NA

  KUKAMATWA KWA WABUNGE WA CHADEMA


  Katibu wa Wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani inayoongozwa na CHADEMA nalaani vitendo vinavyofanywa na Jeshi la Polisi kwa kusababisha mauji ya raia na kukwepa kufanya uchunguzi kamili na huru kuhusu wahusika wa vifo hivyo na kuingilia haki za msingi za jamaa za marehemu na wananchi wa eneo husika kushiriki katika maziko ya wakazi wenzao na hatimaye kupatiwa haki nyingine zinazostahili kutokana na madhila yaliyotokea.

  Aidha nakemea hatua ya jeshi la polisi ya kuwakamata wabunge wa CHADEMA, Tundu Lissu na Esther Matiko wakiwa katika kazi ya kuwatumikia wananchi na natoa mwito waachiwe mara moja; wao pamoja na wote waliokamatwa nao.

  Tundu Lissu (Mb) ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Sheria na Katiba aliitwa na wahanga wa tukio husika pamoja na chama kwenda kusimamia haki za msingi za familia za marehemu baada ya polisi kukataa kufanya uchunguzi na pia kuminya mazingira ya haki kupatikana.

  Akiwa katika kutekeleza wajibu huo, jana (23 Mei 2011) alitaarifiwa na familia za marehemu na wananchi wengine kwamba polisi ina mpango wa kuchukua miili ya marehemu usiku na kuipeleka kusikojulikana na kuombwa kuungana nao katika kuwapa huduma za kisheria katika hatua zote. Aliambatana na familia za marehemu, wananchi na viongozi wa chama kufuatilia suala hilo ndipo alipokamatwa yeye na wengine na kuwekwa rumande kuanzia jana mpaka hivi sasa.

  Esther Matiku ambaye ni mbunge wa viti maalum kupitia mkoa wa Mara anayetokea Tarime akiwa katika eneo lake la kazi leo (24/05/2011) alijulishwa na wananchi wa Nyamongo kwamba maiti ambazo walizichukua polisi kwa nguvu zingine wamezitelekeza njiani na kuitwa kwa ajili ya kushuhudia na kuchukua hatua zinazostahili kwa niaba ya wananchi. Akiwa katika kushughulikia suala hilo naye alikamatwa na jeshi la polisi na kuwekwa rumande mpaka hivi sasa.


  Ifahamike kwamba matukio ya Nyamongo na Tarime kwa ujumla ni matokeo ya uongozi wa serikali kushindwa kusimamia vizuri sekta ya madini ikiwemo kuacha kuchukua hatua zinazostahili kwa wakati wa miaka kadhaa sasa kutokana na vitendo vya ukiukwaji wa sheria na mikataba vinavyofanywa na kampuni Barick Africa Gold na vile vinavyofanywa na polisi na vya kifisadi vinavyofanywa na viongozi wengine wa kiserikali wanaonufaika na hali hiyo yenye athari kwa wananchi katika maisha yao kutokana na mauji, uchafuzi wa mazingira, upotevu wa mapato ya umma na watanzania wa eneo husika kutokunufaika kwa rasilimali.

  Naungana mkono na wananchi na wadau wote waliotoa mwito kufanyika kwa uchunguzi huru wa vifo (inquest) ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa na kwa nafasi yangu nyingine kama Waziri Kivuli wa Nishati na Madini nitatoa tamko karibuni lenye kueleza kwa kina udhaifu wa serikali ulivyosababisha mauji hayo na kutaka wahusika akiwemo waziri kuwajibika.

  Aidha, kwa mara nyingine narudia tena kutoa pole kwa familia za marehemu ambao wanapitia kipindi kigumu wakati huu kutokana na matukio yanayoendelea; Mwenyezi Mungu awape uvumilivu wa kusimamia haki na ukweli kwa mustakabali wa taifa.

  Imetolewa tarehe 24 Mei 2011 na:

  John Mnyika (Mb)
  Katibu wa Kambi Rasmi ya Upinzani
  Na Wabunge wa CHADEMA
   
 2. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Na ww mnyika kumbe bure kabisa ! watu walio vunja sheria hata kama ni mbunge hawawezi kuachiliwa mpaka sheria ichukue mkondo wake. Ww huna hadhi ya kimamlaka ya kuwaamrisha polisi wawaachie wahalifu .
   
 3. kyangara

  kyangara Member

  #3
  May 25, 2011
  Joined: Nov 10, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ni sheria zp za nchi wamevunja hawa wabunge we kilaza?
   
 4. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Think Twice unasema kwa kutumia njia ya haja kubwa na unafikiria kwa kutumia makalio.
  Ebu tueleze Tindu Lisu na wengine wamekosea wapi au hayo makosa waliyosomewa Mahakamani unaona yanalingana na yanahadhi sahihi kabisa na kazi yake kama Waziri Kivuli wa katiba na Sheria? Mashitaka yote ni mambo anayopaswa kuyatekeleza katika shughuli zake za kila siku ......

  Please, acha ujinga maana tuko kwenye msiba na maombolezo.
   
 5. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #5
  May 25, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  we ndugu kila mara unaleta upumbavu ktk jamii. Ipo siku taifa litakuwa huru!
   
 6. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #6
  May 25, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  magafu, mbona inatukana zaidi kuliko kuchangia na kujadiri hoja?, nawewe usitumie downstairs kutoa maoni yako, niambie polisi waliowaua hao vibaka wamekosa nini? Au ulitaka polisi hao wauawe na hawa vibaka ndo ungeamini kuwa wananchi wamenufaika na sekta ya madini?. Wewe uko mjini unastarehe harafu unawachochea wananchi waji-expose kwenye risk. Acha ufara.
   
 7. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #7
  May 25, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Taifa letu lilikwisha poteza nafasi ya kuwa huru, watu badala ya kuhamasishana kufanyakazi na kujiletea mandeleo mnakalia kuhamasisha watu wavunje sheria: SUY. Subiri tuendelee kushuhudia vijana wetu wakifa vifo vya aibu.
   
 8. Fungo N.

  Fungo N. JF-Expert Member

  #8
  May 25, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kila laheri Mungu akubarikieni nyote hao ndo polis wetu tutafanyaje lakini one day yes
   
 9. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #9
  May 25, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kweli safari ya kuwakomboa watanzania (Kama wewe) ni ndefu sana. Kwa mawazo yako hao wabunge wamejunja SHERIA GANI maelezo yote yako wazi hujiulizi kwanini walioua watanzania hao watano wako wapi ?
   
 10. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #10
  May 25, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,234
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Kama ni ukombozi wa taifa lolote lile dunia basi mstari wa mbele siku zote ni vijana!! Unayewapinga bila shaka upo upande wa ukoloni na hufai ktk kisima cha fikra mchipuko!!!!!!!!!! F$$$ uuuu memkwa weee!!
   
Loading...