Kauli ya katibu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni kuhusu kukamatwa kwa wabunge wa chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli ya katibu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni kuhusu kukamatwa kwa wabunge wa chadema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Vumbi, May 24, 2011.

 1. V

  Vumbi Senior Member

  #1
  May 24, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 191
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  KAULI YA KATIBU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSU

  VITENDO VYA JESHI LA POLISI KWA RAIA

  NA

  KUKAMATWA KWA WABUNGE WA CHADEMA


  Katibu wa Wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani inayoongozwa na CHADEMA nalaani vitendo vinavyofanywa na Jeshi la Polisi kwa kusababisha mauji ya raia na kukwepa kufanya uchunguzi kamili na huru kuhusu wahusika wa vifo hivyo na kuingilia haki za msingi za jamaa za marehemu na wananchi wa eneo husika kushiriki katika maziko ya wakazi wenzao na hatimaye kupatiwa haki nyingine zinazostahili kutokana na madhila yaliyotokea.

  Aidha nakemea hatua ya jeshi la polisi ya kuwakamata wabunge wa CHADEMA, Tundu Lissu na Esther Matiko wakiwa katika kazi ya kuwatumikia wananchi na natoa mwito waachiwe mara moja; wao pamoja na wote waliokamatwa nao.

  Tundu Lissu (Mb) ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Sheria na Katiba aliitwa na wahanga wa tukio husika pamoja na chama kwenda kusimamia haki za msingi za familia za marehemu baada ya polisi kukataa kufanya uchunguzi na pia kuminya mazingira ya haki kupatikana.

  Akiwa katika kutekeleza wajibu huo, jana (23 Mei 2011) alitaarifiwa na familia za marehemu na wananchi wengine kwamba polisi ina mpango wa kuchukua miili ya marehemu usiku na kuipeleka kusikojulikana na kuombwa kuungana nao katika kuwapa huduma za kisheria katika hatua zote. Aliambatana na familia za marehemu, wananchi na viongozi wa chama kufuatilia suala hilo ndipo alipokamatwa yeye na wengine na kuwekwa rumande kuanzia jana mpaka hivi sasa.

  Esther Matiku ambaye ni mbunge wa viti maalum kupitia mkoa wa Mara anayetokea Tarime akiwa katika eneo lake la kazi leo (24/05/2011) alijulishwa na wananchi wa Nyamongo kwamba maiti ambazo walizichukua polisi kwa nguvu zingine wamezitelekeza njiani na kuitwa kwa ajili ya kushuhudia na kuchukua hatua zinazostahili kwa niaba ya wananchi. Akiwa katika kushughulikia suala hilo naye alikamatwa na jeshi la polisi na kuwekwa rumande mpaka hivi sasa.


  Ifahamike kwamba matukio ya Nyamongo na Tarime kwa ujumla ni matokeo ya uongozi wa serikali kushindwa kusimamia vizuri sekta ya madini ikiwemo kuacha kuchukua hatua zinazostahili kwa wakati wa miaka kadhaa sasa kutokana na vitendo vya ukiukwaji wa sheria na mikataba vinavyofanywa na kampuni Barick Africa Gold na vile vinavyofanywa na polisi na vya kifisadi vinavyofanywa na viongozi wengine wa kiserikali wanaonufaika na hali hiyo yenye athari kwa wananchi katika maisha yao kutokana na mauji, uchafuzi wa mazingira, upotevu wa mapato ya umma na watanzania wa eneo husika kutokunufaika kwa rasilimali.

  Naungana mkono na wananchi na wadau wote waliotoa mwito kufanyika kwa uchunguzi huru wa vifo (inquest) ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa na kwa nafasi yangu nyingine kama Waziri Kivuli wa Nishati na Madini nitatoa tamko karibuni lenye kueleza kwa kina udhaifu wa serikali ulivyosababisha mauji hayo na kutaka wahusika akiwemo waziri kuwajibika.

  Aidha, kwa mara nyingine narudia tena kutoa pole kwa familia za marehemu ambao wanapitia kipindi kigumu wakati huu kutokana na matukio yanayoendelea; Mwenyezi Mungu awape uvumilivu wa kusimamia haki na ukweli kwa mustakabali wa taifa.

  Imetolewa tarehe 24 Mei 2011 na:

  John Mnyika (Mb)
  Katibu wa Kambi Rasmi ya Upinzani
  Na Wabunge wa CHADEMA


  source: Kauli ya Katibu wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu yanayoendelea Tarime - Wavuti
   
 2. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Mwanzo mzuri tutafika mh.Mnyika hiyo ndiyo gharama ya demokrasia ya kweli lakini hiyo ni hatua tunasonga mbele na tuko karibu sana kuufikia mjio wa ahadi tulioandaliwa watanganyika
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Sambazeni habari kwa vyombo vyote vikubwa duniani, Reuters, CNN, BBC, Al-jazeera. Hawa watu lazima sasa waanikwe.
   
 4. L

  LAT JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  no sweet without sweat .....

  down fall will succeed .... tuvumilie na kupeana moyo ..... mungu awabariki wanyonge wote wanaonyanyaswa na watawala
   
 5. m

  mkulimamwema Senior Member

  #5
  May 24, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mwaka huu ni kupiga mawe viongozi wote wa ccm kuanzia mwenyekiti hadi mjumbe wa chini
   
 6. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tutawaomba mawaziri wa JK wanaotuletea matatizo kujiuzulu tmpaka lini? Muda umefika wa kuwashinikiza ili wajiuzulu na siyo kuwaomba jamani! Mfano Hussein Mwinyi (ulinzi), William Ngeleja (nishati na madini).
   
 7. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Kila upuuzi wanaoufanya hawa polisi kwa amri za CCM wataujutia siku inakuja upesi.
   
 8. kibakwe

  kibakwe Senior Member

  #8
  May 24, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sasa TANZANIA inakaribia kukombolewa mikononi mwa MAFISADI NA WAUAJI wa RAIA wa NCHI yao.Ipo siku tutafika
   
 9. O

  Omumura JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ole wao chama cha magamba kwa hiyo innocent damu ilomwagika Tarime, watailipa wao na vizazi vyao!
   
 10. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #10
  May 24, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Natoa pole kwa Mpiganaji wetu Mh. Lissu na Mh. Ester.
  Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu.
   
 11. Trustme

  Trustme JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,172
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ukiwa na serekali isiyothamini wananchi wake ndiyo jambo dhahiri kabisaa linaloonyesha ccm haipo kwa maslahi ya watz! U wajibikaji wa viongozi serikalini ndilo lingekua jambo la msingi, lakini mfumo huu wa kifisadi, kulindana, kujuana na kuteteana bila aibu ndiyo inawafanya watz wakose imani na serikali yoote ya JK! Kujivua gamba kumewashinda, basi kweli wangekua na dhamira ya kuleta mabadiliko serikalini tuone viongozi wanawajibika kwa mauaji haya ya watz wasio na hatia. Kama kuwang'oa kina EL an RA wameshindwa basi tumeeni mwanya huu kuwawajibisha Ngeleja na Nahodha kama kweli mlitaka kuwang'oa visiki (EL &RA). Na kina Ngeleja na Nahodha nao Visiki? Nape Jipu? Najua upo kwenye mtandao
   
 12. S

  Sobangeja Senior Member

  #12
  May 24, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 183
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Inasikitisha sana.Poleni sana wafiwa kwani kwa hivi sasa mmekuwa hamuelewi kinachoendelea.Makamanda mliokamatwa pigeni moyo konde kwani mwanzo wa mafanikio siku zote ni wa taabu na mateso.Tutafika tu! Tupo pamoja!
   
 13. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #13
  May 24, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,644
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  freedom is coming.. sooner than expected!
   
 14. D

  DENYO JF-Expert Member

  #14
  May 24, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  well done mnyika na chadema -taarifa hizi zipelekwe kwenye vyombo vya habari kitaifa na kimataifa. Huu ni unyanyasaji na ukandamizaji wa haki za binadamu ni ukatili usiovumilika wala hatuwezi kuendelea kuangalia haya yakitokea bila kuchukua hatua-redemption is closer
   
 15. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #15
  May 24, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Utawala wa ccm uko ukingoni. Mwema ajue kabisa kuwa siku yake yaja. Hawezi kuepuka kifungo.
   
 16. k

  kbhoke Member

  #16
  May 24, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Inasikitisha kusikia yanayoendea nchini mwetu.
   
 17. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #17
  May 24, 2011
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hawa POLISI (a.k.a vibaka in uniform) baada ya kugawiwa zile uniform wanazovaa na kufanana na PANZI kazi yao ni mauaji tu. Naona wanajifananisha na character wa Terminator series. Hata Polisi wa Makaburu enzi zile walikithiri kwa ukatili, uuaji na kila aina ya uvunjaji wa haki za binadamu. Walifika ukingoni and in the end Peoples Power swept through. Meanwhile,
   
 18. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #18
  May 24, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Waziri wa madini na Waziri wa Mambo ya ndani wawajibike kwa hili.... Hata makatibu wa wizara husika, pamoja na mkuu wa polisi wawajibike ipasavyo.....! Wasiachwe pia wahusika kama RC na RPC wa Mara, hadi wa wilaya kama DC, mkurugenzi na mkuu wa polisi huko Tarime....! na wengine wote watakaooneka kuwajibika kwa mujibu wa taratibu za utumishi na usalama wa raia.....!

  Wazo langu tu...!
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  May 24, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Duh, ama kweli nchi inakwenda pabaya! mimi sijawahi kusikia wakili akikamatwa kwa sababu ya kutetea wafiwa. Kisha inatisha zaidi kusikia Polisi wakivamia Hospital sehemu ya kuhifadhi maiti na kuchukua maiti ili hali hii ni kesi ambayo inahitaji ufafanuzi wa madaktari..Mbali na kuvunja sheria za wafiwa na haki ya wakili Lissu sidhani kama hao polisi wamefuata utaratibu wa kuchukua kibali cha mazishi au kuiondoa maiti ilipohifadhiwa..

  Hivi kwa nini JK anaachia watu kuchukua sheria mkononi wakati ilikuwa kazi rahisi sana kwa serikali kutufunga kamba?..Kama wangefungua mashtaka dhidi ya polisi waliofanya kitendo hicho na hata kama ilikuwa imepangwa, mahakama ingechakachua ushahidi na kuwaachia huru, kuwafunga miaka michache au hata kesi ingechukua miaka minne ijayo na kisha haya mambo yangesahaulika. Zipo njia nyingi tu ambazo serikali inaweza kutumia kulinda amani kama hofu yao kubwa ni malipizo ya wananchi kwa chombo hiki.

  Lakini kuchuua hatua waliyoifanya leo sii tu kwamba inazidisha chuki na uadui mkubwa baina ya vyama na kwa mwendo huu CCM inazidi kuchukiwa zaidi na zaidi kutokana na makosa madogo kabisa ambayo yangeweza kudhibitiwa. Lakini pamoja na hayo hii ndio tofauti kubwa kati yetu na nchi za Ulaya ktk tafsiri ya chombo hiki Polisi. Wenzetu Polisi ni chombo cha KULINDA na KUHUDUMIA wananchi wakati sisi Wadanganyika Polisi ni chombo cha KUKAMATA WAHALIFU...

  Tofauti hizi ndizo chanzo cha uvunjaji wa sheria na kinga kwa polisi wetu kwani Mhalifu ambaye wenzetu husema WANTED hukamatwa popote na wakati wowote ili afikishwe mbele ya sheria.
   
 20. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #20
  May 24, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Baada ya kushindwa kuongoza, sasa wanatumia nguvu na vitisho!
   
Loading...