Kauli ya Jaji Tiganga kwamba huenda Shahidi Ling'wenya alikuwa anapewa majibu ya maswali aliyoulizwa yawaibua Wadau

Wadau wengi sana wamejitokeza kuhoji uadilifu wa Jaji anayeendesha kesi inayomkabili Mbowe na wenzake watatu , kauli aliyoitoa Mahakamani iliyojaa uongo ya Kwamba Shahidi aliyekuwa anahojiwa na Mawakili wa Utetezi Mbele yake na mbele ya umati wa watu , komando Ling'wenya huenda alipewa majibu ya maswali aliyokuwa anaulizwa , imeleta Taharuki kubwa na imethibitisha mashaka ya siku nyingi kwamba huenda Jaji Tiganga yuko upande wa Jamhuri .

View attachment 2023342
Anaonekana ana interest na KESI hiyo.
 
Huyu anatakiwa kupimwa akili, sidhni kama ana akili timamu. Hivi pale kizimbani shahidi anapelekewa hayo mijibu ya maswali na nani ambaye watu wasimwone. Au ni mizimu yake huyo jaji, ambayo yeye pekee yake ana uwezo wa kuiona imekaa na shahidi kizimbani?

Mawakili, washaurini washtakiwa wamkatae jaji kwa vile wana mashaka kama ana akili timamu.
mbona hili limesemwa sana. Lema aisisitiza kuwa Mbowe asijibu chochote, mpuuzi huyu aamue alivyotumwa
 
Teknolojia ni jambo la kuliogopa sana.....

Hii kesi inaripotiwa tofauti na zama za zamani.......

Tutambue kuwa dunia imebadilika sana.......

Ya kwamba Ling'wenya anataka ATHIBITISHIWE kama aliwahi kupelekwa mahabusu CENTRAL POLICE DSM......

Hapa ndipo yalipo mabishano makuu......


#SiempreJMT
#NchiKwanza
 
Bila kumung'unya maneno, aliyesababisha haya yote , Tena makusudi kabisa Ni Rais Samia,

Unatokaje kufanya mahojiano na vyombo vya habari kabla ya kesi kusikilizwa?? Na unatoa hukumu yako kabla ya mwenye mamlaka kutoa hukumu??

Sisi sote Ni Binadamu, na hapa Duniani tunapita TU, hata Kama unaweza kuwa juu ya sheria hapa ulimwengun lakin huwez kuwa juu ya Mungu! Na hii ndiyo tabia ya Shetani!!
 
Mimi sidhani kwamba haamini, ninadhani kuwa shahidi katoa maelezo mazuri na kwa ufasaha hadi jaji akahisi kuwa anafundishwa majibu, inshort jaji alitamani Ling'wenya avurunde, ndio maana baada ya kuona majibu ni mazuri akaweka pingamizi.
Nakubaliana na wewe mkuu, kilichomchanganya jaji ni umakini na ufasaha wa shahidi, akashangaa Jamaa anayaelewa ma PGO kuliko Kingai

Sent from my TECNO-L8 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu samahani.....

Mawakili siku zote huwa wanawafundisha wateja wao kujibu kabla ya kwenda mahakamani....

Hoja iliyopo ,je shahidi wa leo alionekana akifundishwa pale kizimbani kwa kusikika maneno ,kwa kuwa na simu anasoma ama kipande cha karatasi anadesa?!!!🤣
usijisumbue kumjibu hyu mdada, ni kichwani mtupu ingawa simjui, but one can tell from her posts on JF!
 
Nadhani ameshangazwa na umakini wa shahidi mshitakiwa. Kama shahidi mashitakiwa kaamua kusema ukweli anaoujua yeye, ni lazima wenye hila wajiulize kwanini yuko na mtiririko huo!!

Komandoo wa JWTZ wamefunzwa vyema mafunzoni jinsi ya kuongoza, kutoa amri, ukamataji, movement orders, chain of command na wanazizingatia sana wawapo kazini na kuziota usiku kiasi wanazifahamu kwa ufasaha hata wawapo katika misheni za ulinzi wa amani kimataifa askari na maofisa wa JWTZ / TPDF wanazifuata kwa umakini na ndiyo maana wanatambulika na Umoja wa Mataifa kwa kuzingatia kanuni, sheria vizuri .

Tofauti na polisi ambao hata PGO inayowaelekeza watende kazi vipi kipolisi tumeona hazifuatwi ndani ya jeshi hilo la Polisi. Hakuna movement orders, kuandika kumbukumbu vizuri ktk shajara za kipolisi n.k

Hivyo mtu yeyote pamoja na Jaji inatakiwa watambue nidhamu iliyopo ktk JWTZ / TPDF wa utendaji kazi ukiotukuka na wa kufuata kanuni na sheria .


Toka Maktaba :

07 October 2021
Wanajeshi wa Tanzania (TANZBATT 8) walivyopokea nishani za Umoja wa Mataifa


Ni "Habari za UN" kutoka makao makuu ya UN New York City. News.un.org/sw


Source : Mashariki TV
 
usijisumbue kumjibu hyu mdada, ni kichwani mtupu ingawa simjui, but one can tell from her posts on JF!
Mahakama si sehemu ya KISIASA/SIASA sasa hata tukiwa katika mrengo mmoja ni lazima tuambiane ukweli.....kwani YEYOTE anaweza kupelekwa pale....isipokuwa mh.Rais tu.....so kama mzalendo ni lazima TUILINDE MIHIMILI IUNDAYO Tanzania yetu pendwa.......


Siempre JMT
Nchi Kwanza
 
Back
Top Bottom