Kauli ya Freeman Mbowe kufuatia kutoweka kwa Msaidizi wake, Ben Saanane

Binafsi naunga mkono matamshi ya mbowe juu ya kupotea kwa beni,japo kama chadema watu walizoea matamko ya kutosha japo hayajawahi kuwasaidia.
 
Ndio maana namkumbuka Dr Slaa Mbowe kawa mpole sana ccm wanachezea sharubu wanavyotaka........

Jambo serious kama hili ni la kulipua tu kama mbwai iwe mbwai..........

Angekuwa Dr Slaa sizani kama angekubari kuburuzwa namna hii.....

Shame on you Mbowe.......
Kwa hiyo ajilipue mwenyewe!!

Eti nilikuwa safari ulaya na bado nimerudi nikawa na majukumu ya kutembelea kanda..! Kwa sasa tunaenda likizo tukirudi tutapata muda WA kusema.

Mbowe mfanya biashara...angekuwa anajali hata kipind yupo ulaya angetweet tu kuonesha concern mtumishi wake haonekani. Mbowe hajali utu wa MTU. Tunapigwa siasa hapa.
 
Mimi nahisi kama vile Mbowe anajua kilichomtokea Ben...
Mkuu kwa hili hata mimi nahisi Aikaeli anaelewa kila kitu,na kwa habari za hapa na pale,huyu dogo wanamshikilia sehemu.
Kumshikilia kwake ni sbb ya "Lugha kali" dhidi ya "PhD" ya Sizonje.Lugha aliyotumia na namna alivyoishambulia "Taasisi" ya Urais na Rais kama mtu binafsi.

Ziara ya Kenya na namna Rais alivyohutubia na kusalimiana na Uhuru,tai ya Rais na sign and gestures zake wakati wa kusalimiana na Uhuru,ulikuwa ni mjadala mkubwa aliouanzisha bwana mdogo akiwashutumu watu wa usalama na wanadiplomasia wa Tz kwa "kutokumfunda" Rais vizuri juu ya namna ya kuji-behave mbele ya hadhira ya kimataifa.

Sasa utaona,huyu dogo si tu alijenga "bifu" ya ukosoaji wa elimu ya Rais tu,bali aliitawanya mpaka kwa wasaidizi wake,watu wa wizara ya mambo ya nje na hata idara ya usalama wa Taifa.

Kwa aina ya msg alizokuwa anaandika Fb,na kwa namna alivyokuwa na marafiki wengi fb,ujumbe aliokuwa anauweka ulisambaa kwa kasi na kutengeneza picha ya chuki kati yake na wale walio na madaraka
 
Mh. Mbowe kayasema haya leo mara baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu maalumu wa kanda ya Nyasa katika ukumbi wa Igimbi mkoani Mbeya.

Mwandishi: Nini kauli yako juu ya kupotea kwa msaidizi wako Ben Saanane?

Mh. Mbowe: Mambo mengine yanapokua katika masuala ya kiuchunguzi sio kila jambo litasemwa hadharani wakati wote, na tunatambua jambo hili lina hatari, linahusu maisha ya mtu, sasa sio kila wakati kusema kuyarahisha.

Unaweza ukasema kumbe kwa kusema sana unawaruhusu na watesi wake pengine waweze kumtoa roho. Kwa hiyo kuna mambo mengine ni sensitive, siyo mambo ya kuzungumza rahisi sana. Tunafanya kazi kwa njia mbalimbali kama chama cha siasa na tunakuwa waangalifu sana kuhusiana na tuseme nini kwa wakati gani na kwa taratibu gani lakini kwamba chama kinafuatilia suala hili,

Kinawasiliana na vyombo mbalimbali. Chama kina vyombo vyake vingine vya ndani ambavyo vinafanya jambo hili lichunguzwe kwa makini.

Tuko hivyo na tunawahakikishia Wote kwamba muda muafaka ukifika tutaweza kutoa taarifa za kina tumekwamia wapi na nini kifanyike cha ziada.

Mwandishi: Mbona kama mwenyekiti umekua kimya sana kuhusu jambo hili kuliko kawaida yako, kulikoni?

Mh. Mbowe: Ah, sasa inategemea, hiyo ni tafsiri, kwa sababu chama ni taasisi sio mwenyekiti

Na mimi nilikua niko safari kwa muda mrefu. Nilikua ziara ya Ulaya wakati jambo hili likiendelea kwa muda wa wiki mbili na nusu. Nimerejea tu kama siku tano zilizopita na nikaja moja kwa moja kwenye ziara jana na juzi usiku. Lakini tunamaliza sasa jukumu hili la kwenda kwenye ziara tunaporejea majumbani kwa likizo hii ya krismasi tutapata mambo ya kujadiliana zaidi.

Lakini chama kama chama Kilikuwa kinawasiliana sana na familia wakati mimi niko safari.

Mbowe anajuaje habari za watesi kutaka kimtoa roho msaidizi wake kijana Ben?

What if kauli ya Mbowe juu ya kutoweka kwa Ben ikasaidia kurejea kwa msaidizi wake kijana Ben?
 
Mh. Mbowe kayasema haya leo mara baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu maalumu wa kanda ya Nyasa katika ukumbi wa Igimbi mkoani Mbeya.

Mwandishi: Nini kauli yako juu ya kupotea kwa msaidizi wako Ben Saanane?

Mh. Mbowe: Mambo mengine yanapokua katika masuala ya kiuchunguzi sio kila jambo litasemwa hadharani wakati wote, na tunatambua jambo hili lina hatari, linahusu maisha ya mtu, sasa sio kila wakati kusema kuyarahisha.

Unaweza ukasema kumbe kwa kusema sana unawaruhusu na watesi wake pengine waweze kumtoa roho. Kwa hiyo kuna mambo mengine ni sensitive, siyo mambo ya kuzungumza rahisi sana. Tunafanya kazi kwa njia mbalimbali kama chama cha siasa na tunakuwa waangalifu sana kuhusiana na tuseme nini kwa wakati gani na kwa taratibu gani lakini kwamba chama kinafuatilia suala hili,

Kinawasiliana na vyombo mbalimbali. Chama kina vyombo vyake vingine vya ndani ambavyo vinafanya jambo hili lichunguzwe kwa makini.

Tuko hivyo na tunawahakikishia Wote kwamba muda muafaka ukifika tutaweza kutoa taarifa za kina tumekwamia wapi na nini kifanyike cha ziada.

Mwandishi: Mbona kama mwenyekiti umekua kimya sana kuhusu jambo hili kuliko kawaida yako, kulikoni?

Mh. Mbowe: Ah, sasa inategemea, hiyo ni tafsiri, kwa sababu chama ni taasisi sio mwenyekiti

Na mimi nilikua niko safari kwa muda mrefu. Nilikua ziara ya Ulaya wakati jambo hili likiendelea kwa muda wa wiki mbili na nusu. Nimerejea tu kama siku tano zilizopita na nikaja moja kwa moja kwenye ziara jana na juzi usiku. Lakini tunamaliza sasa jukumu hili la kwenda kwenye ziara tunaporejea majumbani kwa likizo hii ya krismasi tutapata mambo ya kujadiliana zaidi.

Lakini chama kama chama Kilikuwa kinawasiliana sana na familia wakati mimi niko safari.
well said he is a diplomatic politician
 
Mimi naona serikali wanajuwa kinacho endelea na Chadema wanajua kinacho endelea. Pande zote mbili zina tuvisha kanzu na matobo.
 
Serekali ya awamu ya 5 haieleweki unapotaka kuongelea jambo kubwa kama hili umakini mkubwa unahitajika,vinginevyo viongozi wote wa CHADEMA wataishia mikononi mwa polisi kama Lissu,nao unaweza ukawa ni mtego maalumu uliowekwa na wazee wa kung'oa kucha,ili kuwanasa viongozi wa CHADEMA.
 
Kuna vitu haviingii akilini hapa kidogo. Hivi hadi umalize ziara ndiyo uanze kufatia kuhusu ben ? au hadi likizo ya Christmas ndiyo muanze kufatilia?
Hapo nimegunduwa kitu kumbe uhai wa mtu hauna thamani sana kama vitu vingine katika Siasa.
Hapo nwenyekiti umeniangusha kwa sababu beni ana mwezi sasa ivi hajaonekana na nyie katika chama hakuna report ambayo inaonyesha hata mmefikia wapi ila mpo kwenye mchakato•inamana ben alivyotoa taarifa anatumiwa msg za vitisho hauoni kwamba na kupotea kwake kuna leta taswira tofauti. Akiwa kama msaidizi wako ulipaswa kuonyesha ukaribu wenu wa kisaidizi kwenye kazi na kwenye taarifa ya vitisho na kwenye kupotea kwake akiwa ni moja ya msaidizi wako wa karibu•hapa naona kuna Giza.. loading...
 
Ndio maana namkumbuka Dr Slaa Mbowe kawa mpole sana ccm wanachezea sharubu wanavyotaka........

Jambo serious kama hili ni la kulipua tu kama mbwai iwe mbwai..........

Angekuwa Dr Slaa sizani kama angekubari kuburuzwa namna hii.....

Shame on you Mbowe.......
Uko sahihi ila Dr Mihogo alikuwa mtu wao ndiyo maana wamemfadhili akaishi ughaibuni. Mbowe hana kinasaba na serikali au chama tawala. Anatumia Buthelezi tactics
 
Anachosema mbowe ni kuwa inaweza kuwa huyo saanane yuko mikononi mwa watu fulani,na wakizidi kuchonga midomo ama kwa kueleza step wanazochukuwa,wamefikia wapi etc,
wale wanaomshikilia wanaweza kuamua kumpoteza mazima kuua soo.

Mwezi mzima kwa uhai wa mtu huoni kuwa tayari kapotea mkuu hujulikani ulipo wala nini, hawa wanasiasa wanajuana woote style zao za onyeshana mabavu
 
Msisitizo wa nini na hapo kawapiga porojo na hakutowa jibu lolote.

Mtangoja sana kwani kishasema anakwenda zake likizo ya Krismasi.

Bi FaizaFoxy,
Mhe Tundu Lissu kahojiwa na Polisi more than 3 hours baada ya Press conference yake kuzungumzia issue ya Ben!
Sasa mlitaka Mwenyekiti Mbowe aseme nini?
Hili jambo ni very sensitive linahusisha vigogo wa serikali kwenye mastermind ya kuplan, kuteka na kupoteza viongozi machachari wa Upinzani hasa CHADEMA! Kwenye PC Tundu Lissu aliomba Polisi wafuatilie mawasiliano ya simu ya mwisho ya Ben Saanane kuona aliwasiliana na nani,saa ngapi, lini na wapi, na nini kilizungumzwa! Hizi data zinaweza kuwa retrieved from Mobile operator database wa mtandao husika through TCRA, lakini mpaka sasa ni kimyaaa!!!!!!
Tuvute subira hizi mambo zitawekwa hadharani tu muda si mrefu!
 
Mpelekee taarifa
Hata kumtembelea mwenzao kisongo hakuna, Lowasa, Mbowe, Lissu, Mashinji, na Nasari yupo jirani tu hapo Arusha lakini wamemfungia vioo Christmas yote hii na mwaka mpya mh ananyea kwenye mtondoo, hii ndiyo chedema bhana.
 
Yaweza kuwa ni kweli ila ushahidi wa dhahiri haujapatikana kumfanya aseme hadharani.
Ninavyojua mimi hata kama Ben katendwa jambo na vyombo vya dola bado ndani yake wapo watoa taarifa kwa chama hivyo itajulikana tuu kwa uwazi
Huwa simuamini Mbowe kabisa....mabomu ya Arusha damu za watu zilimwagika na yeye amekaa na ushahidi mpaka leo bila kujali familia za wahanga.

Tuangalie pande zote za sumuni.
 
Back
Top Bottom