Kauli ya Dr. Slaa kuhusu hoja za ccm Jangwani - CCM mna majibu ya tuhuma hizi?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli ya Dr. Slaa kuhusu hoja za ccm Jangwani - CCM mna majibu ya tuhuma hizi??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Honolulu, Jun 10, 2012.

 1. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  WAKATI CCM, ikihaha kujaza watu kwenye mkutano wake, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa, amekidhihaki chama hicho kuwa hakiwezi kuendelea kutawala nchi kwa kuwalipia nauli, kuwabeba na kuwapa posho watu wanaokwenda kwenye mikutano.
  Slaa, alisema ilani ya chama chochote makini inapaswa kuonekana machoni mwa wananchi na siyo kusemwa kama ambavyo Rais Jakaya Kikwete na timu yake ndani ya CCM wanavyofanya.

  Kauli hiyo aliitoa jana katika Uwanja wa Likangala wilayani Ruangwa mkoani Lindi wakati akihutubia mkutano wa hadhara, huku akitanabaisha kuwa wafuasi wanaokipenda chama chao hawawezi kubebwa na magari kwenda kwenye mikutano kwa kulipiwa nauli.
  Dk. Slaa alikuwa akijibu matamshi mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na viongozi wa CCM katika mkutano wao wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam na kurushwa moja kwa moja na vituo vya redio na runinga.

  Alisema mawaziri wa CCM wamekuwa makasuku kwa kushindwa kutathmini kauli zao za awali, ambazo hazijatekelezwa na kwamba sasa wanakuja na hoja nyingine zisizotekelezeka.

  Akiwachambua baadhi ya mawaziri na kuanza na Jumanne Maghembe, alisema kuwa anapaswa akumbuke miaka zaidi ya kumi iliyopita serikali ilikuja na mkakati wa kilimo cha umwagiliaji na kusema imeshapata kiasi cha dola milioni 12 za Marekani kwa ajili ya shughuli hiyo.
  "Tunataka watuambie hizi fedha zimeenda wapi mpaka sasa wanakuja na kauli nyingine, hivi hakumbuki tulikaa katika ukumbi wa mikutano wa Pius Msekwa wakatuambia hizi fedha zipo, sasa zimeenda wapi?" alihoji Dk. Slaa.
  Kuhusu ujenzi wa barabara kilomita 11,000 zilizoelezwa na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, Slaa alisema huo ni upuuzi kwa kufananisha hali hiyo na mahitaji mazima ya nchi.


  Alisema fedha zilizoibwa na watumishi wa serikali ya CCM ni nyingi kuliko hivyo wanavyojinadi kuwa wamefanya, na kuitaka serikali ieleze dola milioni 1.5 zilizokutwa katika akaunti ya mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM) zimefanyiwa nini.

  Alibainisha kuwa, Serikali ya CCM inapaswa kutolea maelezo fedha za chenji ya rada zimefanya nini wakati katika mahesabu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) hazionekani kutumika.


  Kuhusu kauli ya Steven Wassira kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe atalaaniwa kwa kuwa baba yake aligombea uhuru na Mwalimu Nyerere, Dk. Slaa alisema viongozi hao walisimama kwa ajili ya kuwatetea Watanzania na kama watasimama leo kuna hatari ya kuwachapa viboko viongozi wa CCM kwa kushindwa kuendeleza malengo waliyofikia.

  Naye Mbowe alisema anamsikitikia Wassira kwa kile alichoeleza kuwa, anashindwa kusimamia hata utendaji wa nafasi yake na badala yake anahangaika kuropoka kila wakati mambo yasiyo na tija kwa taifa.
  Alibainisha kuwa, Wassira si saizi yake kwenye majukwaa ya kisiasa kwa sababu hana hadhi ya kupigania ukombozi wa kweli, hivyo akamtaka awatafute watu wenye hadhi yake.

  Alisema katika hali ya sasa, CCM haioni mahaba ya wananchi, hivyo wanajitahidi kukusanya watu katika maeneo mbali mbali ya nchi ikiwa ni pamoja na kununua kadi za CHADEMA kwa ajili ya kujiaminisha mbele ya wananchi.

  "Hawa watu vipi, wana nini sijui kwa kuwa wanatunga uongo wanauaminisha umma na mwisho wa siku wanauamini huo uongo walioutunga kama ambavyo wamefanya leo kule Jangwani," alisema Mbowe.

  Source: Tanzania Daima
   
 2. S

  STIDE JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Yap!! Dr wa ukweli amenena!! Yaani over compyuta!! Big up Dr!! Ccm na wakuda wake wooote njooni na majibu yenye ujazo!!

  I'll be back.
   
 3. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #3
  Jun 10, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,206
  Likes Received: 3,769
  Trophy Points: 280
  Hawana majibu kabisa, kwanza hata sasa hivi uwafuate na kuwauliza waliyozungumza jana jangwani nakuhakikishia hakuna atakae kumbuka,

  Hawatakumbuka kwakuwa mioyo yao ilipingana na uongo wao!
   
 4. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #4
  Jun 10, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  CCM ikifikia mnaanza kujibishana badala ya kufanya kazi basi siku zenu za kuishi uongozini zinahesabika. Kwahiyo badala ya kufanya kazi nyie mtazunguka kila mkoa Chadema ilikopita?
   
 5. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #5
  Jun 10, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Dr Slaa ana akili mile 1000,000,000,000 zaidi ya magamba yote!
   
 6. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #6
  Jun 10, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Inasikitisha sana chama kikongwe kila wakati kukaa na ku copy ya chadema. Hivi ccm, hamuwezi nadi sera zenu bila maji taka?
  Kujibu hoja za chadema iwe ni kutekeleza ahadi, na yale yote mnayosema mmeyafanya yaendane na hali halisi ya mapato yetu.
   
 7. kaburungu

  kaburungu JF-Expert Member

  #7
  Jun 10, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,600
  Likes Received: 2,455
  Trophy Points: 280
  Moja ya mbinu inayotumia serikali ya CCM ni kuhadaa wananchi kwa kuibua ahadi. nzuri zinazosikika vizuri masikioni mwa watanzania.

  Wanasahau kile walichohaidi jana au juzi kimetekelezwa au la bahati mbaya sana kwa CCM na serikali yake ni kwamba, watanzania wa leo ufahamu wao uko juu na hii ni kutokana na kazi nzuri inayoendelea kufanywa na CDM.

  Watanzania wa leo wanaujasiri wa kuhoji,kudadisi utekelezaji wa yale walohaidiwa mwanzo na kizuri zaidi washaelewa nani mchawi wao.

  Nawasilisha.
   
 8. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #8
  Jun 10, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Mama naona siku hizi umebadilika !!!!
   
 9. S

  STIDE JF-Expert Member

  #9
  Jun 10, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mkuu, hivi ndie huyu au ID zinaelekeana!? Maana nahisi kama yule kimeo alikuwa anaitwa R. Sweke au!?
   
 10. D

  DOWN SYNDROME Member

  #10
  Jun 10, 2012
  Joined: Jun 8, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CMD ni chama makini sana!
   
 11. h

  hans79 JF-Expert Member

  #11
  Jun 10, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Ukweli utajulikana tu waache waendelee na mipasho yao hawa nyinyiemu, unafanya mkutano huku unatangaza ya kuwa wasanii hawa watakuwepo. Je hao kuwepo kwao kunasaidia nini?
   
 12. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #12
  Jun 10, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  viva dokta,viva mbowe,viva cdm
   
 13. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #13
  Jun 10, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,253
  Likes Received: 1,194
  Trophy Points: 280
  yaan nyinyiem + plus Nape ni janga la kitaifa
   
 14. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #14
  Jun 10, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  ulitegemea mtoto mzuri kama radhia angeendelea kuwa ccm mpka lini kaiona nuru...kuishabikia au kuiunga mkono ccm lazima uwe na akili ya maiti..huoni hata akina faizafox,mwita25
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Jun 10, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kilomita zaidi ya 11,000 kwa kipindi cha Kikwete tu ni upuuzi? huyu mzee kweli hamnazo.

  Amesha jiuliza, Mkoloni, Nyerere, Mwinyi na Kikwete na yeye akiwemo hukohuko kabla ya ujio wa Kikwete walitengeneza kilo mita ngapi? jumlisha zote pamoja na za Slaa, uone kama zinafika hata nuzu za hii miaka 7 tu ya Kikwete.

  Kumbuka, ukitoa mkoloni, Nyerere miaka 24 KM ngapi? Mwinyi (na Slaa akiwepo)? Mkapa ngapi? Kiwete zaidi ya KM 11,000.

  Amma kweli akutukanae hakuchagulii tusi.
   
 16. S

  STIDE JF-Expert Member

  #16
  Jun 10, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mmh!! Crashwise inamaana FF alishaiona nuru!!? Mwita25 huyo nakumbuka alishaanza kuujua ukweli japo unafiki ulimtatiza, lakini huyu mwingine siwezi amini, na KAMA ni kweli basi CHADEMA LEVEL NYINGINE zaidi ya ninavoijua!!
   
 17. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #17
  Jun 10, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Mimi najiuliza iweje Serikali ijieleze mbele ya wanachama wake na si wananchi wake? Huu ni utumiaji mbaya wa madaraka kwa chama kuyahodhi kiasi hicho. Na nadhani hii move ni kama vile wanajifunga wenyewe goli katika harakati za kuokoa mpira.
   
 18. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #18
  Jun 10, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Dr. ulichonena hakina upinzani kinahitaji majibu yakina na si longolongo za kuongea maneno matupi majukwaani ccm ni serikali inatakiwa kutenda na wala sio kuongea sana bila vitendo. hawa wa meishiwa kabisa na ndio mwisho wa kutawala wajiandae kwenda kukaa uhamishoni maana nawatamani sana nje yahapo wote wataishia gerezani na maisha yaliyobaki watayamalizia gerezani.
   
 19. sexologist

  sexologist JF-Expert Member

  #19
  Jun 10, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 2,296
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 135
  Mkuu CMD bado kuanzishwa Tanzania, kwa sasa tuna CDM.

  Asante!
   
 20. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #20
  Jun 10, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Watanzania wanataka hoja zijibiwe na ugumu wa maisha udhibitiwe hasa mazao ya chakula ya ndani!!!sio kutupa vijembe kama taarabu,watu wameshaamka wanapoteza pesa zao bure maana watanzania wa leo sio wa jana kamwe,watashangaa sana naona kuna nusu ya wabunge watakosa ubunge mwaka 2015 sababu ya kutojali matatizo ya wananchi!!!
   
Loading...