Kauli ya Dr. Lwaitama kuhusu Mhariri wa Tanzania Daima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli ya Dr. Lwaitama kuhusu Mhariri wa Tanzania Daima

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by thatha, Aug 12, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  JUU YA MUUNGANO: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Nimesikitishwa na aina ya uandishi wa habari uliojiweka wazi katika taarifa iliyonukuliwa kuandikwa na mwandishi wa gazeti moja la kila siku (Tanzania Daima la tarehe7 Agosti 2012), Datus Boniface.

  Huyu mwandishi, pamoja na wahariri wake walioruhusu habari hiyo kuchapwa walithubutu kusema uongo kuwa eti "Dk Lwaitama, Prof. Sheriff na Prof Shivji waliushambulia Muungano.." Tena, mwandishi huyu na wahariri walioruhusu habari hiyo ichapishwe wakaenda mbali zaidi na kutumia kichwa cha habari kilichosema eti ‘Shivji, Lwaitama wataka Muungano uvunjwe'.
  Nafahamu Prof Shivji tayari ameisha toa tamko juu ya upotoshwaji wa hali ya juu uliobebwa na kichwa cha habri hiki na makala nzima ya mwandishi huyu mwenye aina yake ya ujuzi wa kuandika habari, Datus Boniface. Mimi katika tamko langu sitojisemea mimi tu kama alivyosema Prof. Shivji katika tamko lake. Nitajaribu kueleza kile ambacho nilidhani kilizungumzwa na kila aliyechangia katika Mazungunzo ya yale ya Kifungua Kinywa ( Breakfast Talk), Jumatatu tarehe 6 Agosti 2012, yaliyofadhiliwa na Baraza la Habari Tanzania( MCT).

  Wakwanza kuzungumza alikuwa Prof Abdul Sheriff na aliainisha kile alichotaka kibainike kama historia a sababu za kuwepo Muungano katika ya Tanganyika na Zanzibar. Alieleza kile alichotaka kieleweke kama mapungufu ya kisheria katika mchakacho wa kuwepo Muungano. Pia alieleza kile alichotaka kieleweke kama Muungano kukosa kuwa na uhalali wa kisiasa ( political legitimacy) kutokana na ushirikishwaji hafifu wa viongozi wa Serikari ya mapinduzi wa wakati huo na wananchi kwa ujumla. Akahitisha maelezo yake kwa kusema Wazanzibari walio wengi sasa hivi wamefikishwa mahali ambapo wanatamani kutumia mchakato wa kuandika katiba mpya uliozinduliwa hivi karibuni unaoongozwa na Jaji SJoseph Sinde Warioba kujadili Muungano kwa kina na kuingia kwenye maridhiano mapya juu ya kama Muungano uendeleee kuwepo na kama ndiyo kwa mfumo wa serikali ngapi. Ilikuwa wazi kuwa Prof Sheriff alikuwa haamini kuwa walikuwepo Wazanzibari wengi waliokuwa tayari kuendelea na Muungano wa serikali mbili kama wa sasa. Sikuwahi kusikia mahali popote ambapo Prof Sheriff alitamka kuwa eti "anataka" Muungano uvunjwe, yeye kama yeye. Sasa huyu mwandishi Datus Boniface halipata wapi ujasiri wakumlisha mwanataaluma ya historia huyu wa Kitanzania, hata kama ni Mzanzibari pia? Uandishi wa habari wa aina hii ya Datus Boniface ni wa kusikitisha sana.

  Aliyezungumza wa pili alikuwa mimi, Dkt Azaveli Lwaitama. Mimi kazi yangu ilikuwa kujibu hoja (Discussant) za mzungumzaji mkuu ambaye kwa kweli alikuwa Prof. Abdul Sheriff peke yake. Kwanza nilimkosoa ndugu yangu, Mtanzania mwenzangu, Prof Abdul Sheriff, kwa kuomba wote tukubali kuwa viongozi wetu waliotuunganisha na kusimamia kuzaliwa taifa letu la Tanzania walikuwa watu walioongozwa na dhamira safi iliyochimbuka katika kuwa waumini thabiti wa itikadi ya Umajumui wa Kiafrika ( Pan Africanism) ya kutaka kuwaunganisha watu wa dola zetu hizi za watu waliokuwa wamekusanywa pamoja na wakoloni na kupachikwa majina kama Tanganyika na Zanzibar bila ridhaa ya wakazi walikuwa ndio wengi wa sehemu hii ya Bara la Afrika. Nikaeleze jinsi mbavyo mwelekeo wa viongozi hawa haukuwa wa kufungwa sana na matakwa ya kisheria bali na kile walichokiamini kingesadia kufanikisha lengo la kuwaunganisha Waafrika wote bila kujali kabila ( tribe) au uzawa ( race).

  Nikatolea mfano wa jinsi Mwalimu Nyerere alivyoshirki katika kuimiza kuungana kwa Shiraz Association na African Association kuzaa Afro Shiraz Party ( ASP) tarehe 5 Februari 1959, siku na mwezi ambavyo mwaka 1967 vilikuja kuwa siku na mwezi wa kuzaliwa Azimio la Arusha , na mwaka 1977 vilikuja kuwa ni siku na mwezi kilizaliwa Chama cha Mapinduzi kutokana na kuunganisha Tanganyika African National Union ( TANU) na Afro Shiraz Party ( ASP).


  Nilisisitiza kuwa leo tunaweza kuyaona wazi mapungufu makubwa katika taratibu za kisheria zilizogubika mchakato wa kuunda Muungano lakini si vizuri kusema eti tuukatae Muungano kutokana tu na mapungufu haya ya kisheria. Si vizuri na si busara kusahau kuwa Muungano uliundwa kwa sababu za dhamira ya kuunganisha Washiraz, Waafrika, Waarabu, Wahindi na Wazungu na kuwaweka pamoja kama Waafrika waumini wa Umajumui wa Kiafrika (Pan Africanism), wawe wa dola lilosimikwa na wakoloni la Zanzibar au dola lililo simikwa na wakoloni la Tanganyika.

  Mwalimu Nyerere na Mzee Abedi Karume walisukumwa na kutaka kuunda taifa ya Kiumajui wa Kiafrika jipya la TANZANIA, baada ya kuona Mzee Jomo Kenyata wa Kenya na Ndugu |Milton Obote wa Uganda hawakuwa tayari kwa wakati huo, mwaka 1964, kuunda dola jipya ambalo lingeongozwa na itikadi ya vuguvugu la utaifa wa Umajumui wa Kiafrika ( Pan Africanist nationalist movement) la Shirikisho la Afrika Mashariki.


  Kwa waasisi hawa wa Muungano taratibu za kisheria hazikupewa kipaumbele bali dhamira safi ya kutenda liloonekana kuwa la manufaa kwa wananchi walio wengi wa sehemu hii ya Afrika. Tukumbuke kuwa Mzee Karume na Mwalimu Nyerere walikuwa wanafanya kazi katika mazingira ya kivuli cha Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 1964 mwezi mmoja baada ya Uhuru wa Zanzibar tarehe 9 Desemaba 1963 uliopatikana kwa kufuata taratibu za kisheria lakini matokeo yake yakapinduliwa kijeshi tarehe 12 Januari 1964 kwa vile taratibu hizo za kisheria zilitumika kukwepa kupatikana kwa ridhaa ya kisiasa ya walio wengi katika kupatika Uhuru ule wa Zanzibar wa Desemba 1963!!


  Nilitumia muda kuelezea jinsi ambavyo tabaka la mabepari uchwara Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar lilivyokuwa na ushawishi mkubwa juu ya uongozi wa serikali ya Muungano na serikali ya Zanzibar. Nilianisha kuwa hii ndiyo ilikuwa sababu kubwa ya kukosekana kwa wanasiasa madhubutu wenye ushwaishi ndani ya CCM ya miaka kuanzia 2006 wenye utashi wa kutetea dhamira ya waasisi wa Muungano waliokuwa waumini wa itikadi ya Ujamaa na Umajumui wa Kiafrika. Nikabainisha kuwa utetezi wa mfumo wa serikali unatolewa kikasuku na viongozi wa juu wa CCM ya wanamtandao ya kuanzia mwaka 2006 ni utetezi wa kinafiki kwani juhudi za makusudi za kuutetea Muungano kwa vitendo hazikuwa dhairi. Niliorodhesha nyanja kama uteuzi wa wakuu wa vyombo vya dola kama polisi na jeshi la wananchi au Benki Kuu ambao ungekuwa umefanywa kwa lengo la kulinda Muungano hata kero za Muungano zinazotajwa na wanasiasa wa Zanzibar zingekuwa pungufu.

  Nilisahau hata kutaja jinsi wana-CCM wa kundi la Mtandao walivyozima kwa njia za hila na hiyana kupatikana kwa Rais wa awamu ya Nne Mzanzibari, yaani Dk. Salim Ahamed Salim mwaka 2005. Nilibainisha kuwa hii ndiyo ilikuwa sababu kubwa ya watetezi wa dhati wa Muungano wa Serikali Mbili wenye kufuata nyayo za Mwalimu Nyerere kama mimi, wanaosukumwa na kuwa waumini wa itikadi ya Umajumui wa Kiafrika, kukikri kuwa kwa sasa ukitaka kulinda Muungano katika mazingira ya sera za uchumi na siasa za uliberali mambo leo lazima kukuballi kuwepo kwa Muungano wa serikali Tatu.

  Nilitumia muda mrefu zaidi nikieleza kufurahishwa kwangu na msimamo wa mwanasiasa kijana wa chama cha Chadema, Mheshimiwa Zito Kabwe, kuelezea, katika gazeti la kila wiki la Fahamu hivi karibuni, kuwa mwalimu wake wa nje ya darasa Dk Lwaitama sasa alikuwa anaunga mkono dhana ya kutafuta kuulinda Muungano kwa kuridhia kuwepo kwa Muungano wa serikali Tatu. Nilielezea jinsi Mheshimiwa Zitto alivyofafanua kuwa dhana hii ya kuulinda Muungano kwa kukubali sera ya serikali Tatu amekuwa nayo kwa muda sasa na ingelenga kuwepo kwa Serikali na Bunge la Muungano. Serikali hii ya Muungano ingekuwa ndogo, yenye kushughulikia mambo ya Muungano machache. Mimi mwenye nilielezea kuwa niliishapendekeza mahali pengine kuwa labda Serikali ya Muungano ingekuwa na wizara kuu zisizozidi nne au tano zenye uteuzi wa mawaziri wa sawa kwa sawa, Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, huku Urais wake ukiwa kwa zamu.

  Wizara kuu zingelihusu mambo ya ndani ( yaani uhamiaji, uraia, polisi), mambo ya nje ( yaani ulinzi wa nje na mahusiano ya kimataifa), uratibu wa mambo ya fedha na mipango ya uchumi ( yaani sarafu, sera ya uwekezaji, mambo wa ushuru, na kodi), na miundo mbinu inayoitaji uwekezji mkubwa( teknohama, uzalishaji na usambazaji umeme, usafiri wa bahari na maziwa, reli, na anga). Hata haya mambo ya muungano mengi yake baadaye yangelishugulikiwa na Jumuya ya Afrika Mashariki kadili itakavyo kuwa inaimarika kuelekea kuwepo kwa Shirikisho la Afrika Mashariki.

  Nilielezea pia jinsi Mheshimiwa Zito alivyokuwa amependekeza kuwa kungelikuwepo serikali mbili za Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar zilizo sawa kila moja ikiongozwa na Waziri Mkuu na kila moja ikisimamiwa na Baraza la Wawakilishi. Nikaeleza jinsi Mheshimiwa Zito alivyopendekeza katika uchanguzi mkuu kungewepo uchanguzi wa Rais na Makamu wa Rais Mwenza wa Serikali ya Muungano na Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano pamoja na Uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Serikali ya Tanzania Bara na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Serikali ya Tanzania Zanzibar . Muda mwingi niliutumia katika kuunga mkono mawazo haya ya awali ya mwanasiasa huyu kijana na mzalendo , Zito Kabwe nikionesha furaha yangu kuwa mwanasiasa kijana wa chama cha upinzani cha Chadema kama huyu ameweza kuona mbali kiasi hiki kuliko viongozi wa sasa wenye ushawishi ndani ya chama kilichouasisi Muungano cha CCM.

  Nakumbuka katika mjadala uliofuata mchango wangu mwanahabari mwanandamizi amabaye ni Mhariri Kiongozi wa gazeti la Jamhuri, Deodatus Balile, alionyeshwa kuvutiwa mapendekezo haya ya jinsi ya kunusuru Muungano nay eye kupendekeza kuwa ingekuwa vizuri ikiwa Tanzania Zanzibar itaitwa Tanzania Visiwani!. Lengo la wachangiaji wote siku hiyo lilionekana kutafuta njia za kuzidi kuimiza kuukubali utambulisho wa kujiita Watanzania, iwe mtu ni anatokea kuwa mkazi wa Tanzania Bara au mkazi wa Tanzania Zanzibar na polpole kufifisha mawazo ya kubanguana kwa misingi ya Utanganyika na Uazanzibari. Mimi nilisisitiza kuwa utambulisho wa kwa misingi ya Utanganyika na Uazanzibari, majina tuliyopachikwa na wakoloni, ulikuwa ni utambulisho uliokinzana na kuwa waumini wa itikadi ya Umajumui wa Kiafrika, ambayo ndiyo ilituunganisha katika kupigania uhuru wa bendera miaka ya 1940 na 1950.

  Kwa lengo hili hili la kuufanya utambulisho wa Utanzania ushamili zaidi na zaidi, na kufifisha mwelekeo wa kubanguana kwa misingi ya Utanganyika na Uazanzibari, pendekezo langu liloonekana kuridhiwa katika andiko la Mheshimiwa Zito lilikuwa kuwa Mawaziri Wakuu wa Seriakali za Tanzania Bara an Tanzania Zanzibar wangeteuliwa na vyama vya siasa vilivyoandikishwa ki- Muungano kama sasa kutegemea ni chama kipi au muungano wa vyama vipi ungekuwa umepata viti vingi au kura nyingi katika changuzi za Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi husika.

  Pendekezo langu lilikuwa kuwa kutokuwepo kwa uchanguzi wa wakuu wa serikali ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar kungesaidia katika kupunguza, polepole, ushabiki na hamasa za kisiasa zinazojikita kwenye utanmbulisho wa Utanganyika au Uzanzibari. Haya yote lengo lake lingekuwa kutafuta njia za sasa za kuendelea kuwaenzi waasisi wa Muungano, Mwalimu Nyerere na Mzee Karume, ambao dhamira yao ilikuwa nzuri ya kuunganisha Waafrika wote bila kuwabagua kwa misingi ya kabila, rangi, dini, uzawa au upande wa bahari ya Hindi mtu alikokuwa anaishi kwa sasa au hapo nyuma.

  Nilisisitiza umuhimu wa itikadi ya Umajumui wa Kiafrika kwa kusema hata kama itatokea ushawishi wa tabaka lenye kutaka kuvunja Muungano wakawashauwishi Wazanzibari kwa sasa kuridhia kuuvunjika kwa Muungano basi Watanzania Bara waendelee kujiita Tanzania Bara na Wazinabari waendeleee kujiita Tanzania Zanzibar, kama Wasudani Kusini walivyoridhia kujiita Sudani Kusini licha yakupata uhuru. Mapendekezo yote haya yangesaidia kuimiza kuendeleza juhudi za kusimika utambulisho wa Kiumajumui wa Kiafrika wa U-Tanaznia ulioasisiwa na Mwalimu Nyerere na Mzee Karume. Hii nngekuwa kama ilivyo kwa kama kuendelea kuwepo utambulisho wa Sudani kwenye utambulisho wa Wasudani wote, Kusini na Kazikazini!!!! Sielewi uandishi wa Datus Bonaface ni wa aina gani uliomruhusu kusuka maneno kutoka kwenye mchango wangu hapo juu wakusema eti ‘Shivji, Lwaitama wataka Muungano uvunjwe' au eti " Dk Lwaitama, Prof. Sheriff na Prof Shivji waliushambulia Muungano.." Inasikitisha sana kuwepo waandishi wa aina hii na wahariri wanaoruhusu uchapishwaji wa uongo wa kiwango hiki!!!

  Wachangiaji kadhaa walifuata mchango wangu kabla ya Prof Shiji kutoa mchango wake ambao ameulezea vizuri sana katika tamko lake kuhusu upotoshwaji wa hali ya juu ulifanywa na mwandishi Datus Bonaface pamoja na wahariri walioruhusu habari hii ya uongo kuchapishwa. Laiti kama wahariri wale wangeomba ushaidi wa kanda ya kilichozungumza wangegundua mara moja kuwa mwandishi Datus Bonaface ni mwandishi wa ajabu kweli kweli. Naliambatisha Tamko la Prof. Shivji kama alivyolitoa, na nalo bila shaka yeyote ninaonesha wazi kuwa Prof. Shivji kamwe hakutamka mahali pale kitu chakumfanya mwandishi aseme eti ‘Shivji, Lwaitama wataka Muungano uvunjwe' au eti " Dk Lwaitama, Prof. Sheriff na Prof Shivji waliushambulia Muungano.." Inasikitisha sana kuwepo waandishi wa aina hii na wahariri wanaoruhusu uchapishwaji wa uongo wa kiwango hiki!!!

  Mwl. Azaveli Feza Lwaitama
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Jukwaa la Dira Afrika Mashariki
  &
  Mhadhiri Mwandamizi Mstaafu,
  Kitengo cha Falsafa,
  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
  +255784432696/+255782807728
  Agosti 11, 2012
   
 2. zubedayo_mchuzi

  zubedayo_mchuzi JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2012
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 4,922
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Dr Lwaitama Katika kipindi cha umbuzi kinacho rushwa Na TV SIBUKA,akichambua kuhusu kesi ya Mahalu..alisema kama waandishi wa habari wangekuwa makini katika kuchambua kesi hii,Lwaitama alisema kama uchambuzi wa kina wa kesi ungefanyika basi ingeshatupiliwa mbali,kwani imedumu kwa miaka 5 sasa,akaongeza kesi nyingine inayo mhusu ighondu ya utekaji wa Dr Ulimboka nayo kwa akili ndogo ni kupoteza muda.
  Akahoji kwanini waandishi wa habari hamfatilii kwa undani na mmekuwa mkitumika sana,Sasa ina mana WAHANDISHI WA HABARI mmekuwa ubao wa matangazo wa POLICE mnasikiliza then mnakuja kuandika..
  Waandishi mtajibu wenyewe.
  Source-Tv sibuka,uchambuzi
   
 3. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,706
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  huenda kuna ukweli fulani kesi hii ilipaswa iwe imeshatolewa hukumu siku nyingi
   
 4. zubedayo_mchuzi

  zubedayo_mchuzi JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2012
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 4,922
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Angalia kipindi cha hoja ya Mwlm.Lwaitama kupitia Tv sibuka.
  Anachambua hoja tofauti tofauti na sasa wameanza kwa kusoma meseji za watazamaji...

  Hoja ya leo:Mchakato wa Ukusanyaji wa maoni ya katiba.
   
 5. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #5
  Aug 13, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Gazeti la Tz Daima linaendelea kutawaliwa na makanjanja katika fani ya uandishi na ndio maana halina mvuto kwa habari makini.

  Niliwahi kumpigia simu mhariri fulani juu ya kukosa usahihi katika habari fulani, lo ilikuwa ajabu.
  Nikaisha kutukanwa kuwa mimi ni mtu wa system, na kwamba hatumbabaishi!!!

  Mimi vile vile mwanahabari , nilitaka kuwatonya tu USAHIHI wa habari yao, hawKutaka kusahihishwa.

  Katika hili namwelewa Dr Lwaitama, mtu ambaye ni makini.
   
 6. T

  Tata JF-Expert Member

  #6
  Aug 13, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,737
  Likes Received: 657
  Trophy Points: 280
  Tumemwelewa Dr. Lwaitama mwanachama mfu wa CCM. Ila mimi nadhani njia sahihi ni kuwaacha wananchi wawe huru kuamua ni muungano gani wanautaka hata kama hilo lina maana ya kuuvunjilia mbali huu uliopo. Ni vyema kuendelea kuota huu unaoitwa umajumui wa Kiafrika anaozungumzia Daktari Lwaitama lakini ukweli ni kuwa utabaki kuwa ndoto tu na sioni ukufikia kiwango kile walichofikiria akina Nkurumah and Nyerere enzi hizo. Suala la nchi hizi zitaitwaje baada ya kuvunjika kwa muungano nalo ni la wananchi kuamua. Hatuwezi kulazimisha ziitwe Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara baada ya kuvunjika wakati sasa hivi tunaruhusu watu ndani ya muungano wajiite Wazanzibari.
   
 7. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Sikubaliani na Dr eti waandishi wangekuwa makini kesi ya Prof. Mahalu ingefutwa siku nyingi.. nasema tena sikubaliani naye hata kidogo, ni mtu anayeheshimiwa katika jamii lakini kuheshimiwa sio sababu ya kila ulisemalo nalo libaki lilivyo.

  Napenda kurejea habari ya gazeti la mwanahalisi iliyosababisha gazeti hilo kufungiwa, wote tunajua kilichojiri ndani ya gazeti lile, kama kweli polisi wetu, mahakama na vyombo vingine wanaheshimu taarifa za kiuchunguzi hakika yule mkenya ighondu ingeshafutwa na sasa tungekuwa kwenye level nyingine ya upelelezi na uchunguzi hatimae wahusika halisi wangefikishwa kunakohusika na sheria kuchukua mkondo wake, pia kama kweli vyombo vyetu vingekuwa na uwezo huo anaousema Dr Lwaitama leo kagoda ingekuwa imefikishwa mahakamani na wahusika wote kukamatwa na sheria kuchukua mkondo wake.

  Mifano ni mingi lakini hakuna haja ya kuchoshana, Dr Lwaitama anapaswa kuitendea haki nafsi yake kwa kusema kweli ni mamangapi yaliyochunguzwa na magazeti makini Tanzania na taarifa hizo za kiuchunguzi zikieleza kwa kina kiasi kwamba kufanya kazi za taasisi nyingine kama takukuru, uwt, polisi nk kuwa rahisi lakini matokeo yake ni kuvidharau vyombo vya habari na wakati mwingine kuvifungia?

  Ifike mahali sasa vyombo vya habari vitambulike rasmi kama mhimili wa nne wa dola ili viheshimike na adhabu itakapotolewa kwa chombo flani iwe kwa maslahi ya wenye nchi na sio watawala.
   
 8. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #8
  Aug 13, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  sikubaliani na wewe hapo kwenye blue,yaani hawa waandishi wetu mazuzu waje kuwa mhimili wa 4?????akina shigongo????hahahaha akina kibonde,we mdau wewe,
   
 9. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #9
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Nakubaliana na wewe mkuu, vyombo vya habari hapa kwetu havina ueledi wa kiuandishi wa habari wala fani nzima ya habari.
  Na hilo ndio lalamiko la Dr Lwaitama kwa Tanzaia Daima.
  Karibu vyombo vyote vinatekeleza yale ya waajiri wao na si kupresent news as it comes.
  Kwenye investigative reporting ndio wako hai bin taaban.

  Suala la Dr Lwaitama na Tanzania Daima is a case to investigate, kwa nini mwandishi au gazeti linaweka maneno asiyotamka mtu mdomoni mwake?
  Si kuwa huo si uandishi wa habari tu lakini ni uandishi ambao mwandishi/gazeti ndio lingependa kusema vile lilivyo andika.

  Huo ni ujinga wa hali ya juu.

  Kuna mtoa mada hapo juu Masopakyindi, ambaye alidiriki kuwaonyesha hata makosa ya kiuandishi lakini wenzetu ni wagumu kubadilika kwa vile wao wana the last say on what appears on their papers.

  News media kuwa mhili wa nne?
  HELL NO!!
   
 10. B

  Bigaraone JF-Expert Member

  #10
  Aug 13, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 722
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tuangalie na education basics ambazo Watanzania wa leo tunapata kama zinamuandaa mhitimu kuwa critical and critique in one's own nalysis. Mfumo wetu wa elimu tutake tusitake na tusifiche ukweli ulikuwa sabotaged tangu ilipoingia awamu ya pili ya ruksa. Mawaziri na watendaji wa elimu walianza kuteuliwa ili kulinda masilahi ya kundi fulani kwa kisingizio cha kuonewa na awamu ya kwanza. Bahati mbaya ukishaanza ubaguzi na kuacha maamuzi yawe nje ya quality na standards matokeo yake si mazuri sana na mwiso wake ni boomeranga maana ulichokitaka kukitetea unakuta nacho unakiharibu. Kwa hiyo kulianza kuwa na vitu vya ajabu na sekondari ambazo Mwalimu anasema "they secondary shools in name......."

  May be wahusika walikuwa na nia nzuri lakini walishindwa kupima matokeo katika upeo. Elimu ikadhalilishwa na shule hasa za serikali zikawa hovyo. Walimu wakuu waliokuwa makini wakapewa promotion au wakaingia kwenye siasa ili wapate maslahi bora. Ilipokuja awamu ya tatu ikaendeleza yaleyale ya awamu ya pili lakini walau heshima ya elimu ikarudi baada ya vijana wengi kuwa wamekimbilia umachinga.Lakini standards na quality havikuangaliwa ili zipewe heshima ya kale. Ndio maana hijabu ziliendelea kuvaliwa kwa woga wa kuwaudhi kundi lililolengwa kullindwa na kina Mungai wakachukua nafasi ya ubinafsi kubadili syllabus na kuharibu kabisa. Awamu ya nne ikaja na vihoja vilevile kuanzia sekondari za kata, kupandisha taasisi kuwa university statatus short of academic plans and preps. Walimu wamezidi kudharauliwa let alone wale wa so called voda faster walioandaliwa kwa miezi 3. All is pathetic in Tanzania as one cartonist has depicted "bla bla bla, bla....." Kama taifa mnapoanza kuchezea na kudharau sekta muhimu kama elimu na kutoa kipaumbele kwa siasa ujue taifa linaumwa. Dr. Lwaitama the Datus are so many in offices be it private or public, in informal sector, in the streets and everywhere because we have decided to starve the hen and we want it to bear golden eggs. Datus ni matokeo ya mfumo mbovu ambao hata hatupazi sauti kuutokomeza. Ingekuwa taifa lingine migomo miwili ya madaktari na walimu isingechukuliwa kama ya makundi lakini ingekuwa ni taifa zima. Lakini wapi wamedhalilshwa, wamekashifiwa, wamepigwa na wanaendelea uguza majeraha both physically and psychologically na Watanzania tupo to passive as ever. Where are the pressure groups- activists, intellectuals- where those intellectual of yester years from the Hill, where our learned brothers (lawyers) ambao mkuu alisema we suffering impact of corruption in contracts kwa sababu our lawyers are short of contract skills. Have you succumbed to that. The litany is so long but the bottomline we Tanzanias need to change the mindset if want to have a place under the Sun. Nawakilisha
   
 11. J

  Jumaane Member

  #11
  Aug 13, 2012
  Joined: Jul 7, 2012
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mambo hayo: ruhusa ipatikane, wazanzibari kuitwa wazanzibari.
   
Loading...