Kauli ya Dk.Slaa kuhusu malalamiko ya Rais Kikwete ya kukithiri kwa rushwa ndani ya CCM

u have to face reality even though it pains
slaa n his chademonstration mobb are wasting their time..

HII MIJITU NDO MIROFA, JK JANA KAKIRI HALI YAO NI MBAYA HASA KTOKA CDM WEWE UNAKUJA NA KEBEI ZAKNW ZA KIROFA DHID YA DR. NANI KAFANYA II KAZ ATA JK ANAOGOPA, WEWE U R IDIOT MROPOKAJi
 
sasa mbona slaa anameza matapishi yake??
Lini yeye alishatoa tamko la kumkubali kikwete kama rais wa nchi hii??
Yeye si alishatamka waz waz kua rais wa nchi hii ni yeye na kwamba ushindi wa kikwete ni batili
hivi slaa bado tuh hajakata tamaa kua wananchi tushajua janja na siri iliyojificha ndani ya hiki chama cha kichaga na kidini??
Its bad that slaa n his mobb are wasting their time
and too bad indeed because this time will come to lost them too..

Kaka tulishakataza kuwagawa watanzania kidini na kikabila, dhambi ya dini matokeo yake umeyaona, sasa ya ukabila ndiyo itakuwa mbaya zaidi. Punguza Jazba.

ushauri wangu,nenda shule kajifunze vizuri kingereza, au ukiandika jaribu kutumia kiswahili. kiingereza kitakuumbua

"mobb are wasting their time
and too bad indeed because this time will come to lost them too"
 
Kaka tulishakataza kuwagawa watanzania kidini na kikabila, dhambi ya dini matokeo yake umeyaona, sasa ya ukabila ndiyo itakuwa mbaya zaidi. Punguza Jazba.

ushauri wangu,nenda shule kajifunze vizuri kingereza, au ukiandika jaribu kutumia kiswahili. kiingereza kitakuumbua

"mobb are wasting their time
and too bad indeed because this time will come to lost them too"
Mkuu achana naye, ni mmoja wa wanaotuibia kodi zetu bila aibu. He just can't see the workdone by CDM and appreciate for helping the majority. Watu kama hao si wakubishana nao, you just give them time.
 
ila ningekua mchaga ungenihitaji sio??
Ila me ni mkristo mwenzako,stil bado hunihitaji coz of umakonde wangu??
Do you see now where the problem rise?
I am telling you,this party is a natural calamity more than just tsunami,floods,global warming,earthquake and etc..
Lets us seek ingridients of acknowldgement..

Maneno haya hayana mvuto kabisa kwenye nchi tunayoitaka. Kwa nini kila kitu unakigeuzia kwenye udini, ukabila, kwa nini usiongelee hoja bila kutaja udini tena, ' mkristo mwenzako' hiyo kitu ni ya nini. tumetoka kwenye matatizo hayo, mbona bado unayapenda. Hebu siasa iseme siasa na dini itasemwa kwake.
 
Asingeingia Ikulu bila rushwa ya mabilioni iliyokusanywa na kundi chafu lililojiita "wana mtandao" kutoka kwa mafisadi mbali mbali wakiwemo Jeetu, Subhash Patel, Yusuf Manji na wengineo wengi. Na huyo mamvi naye ameanza kutoa rushwa miaka mitatu kabla ya uchaguzi!!!! Nchi yetu inahitaji kuombewa sana.

Raisi yeye mwenyewe mtuhumiwa wa rushwa, refer list of shame Mwembeyanga.
Alishawahi kupelekewa list ya majina ya wala rushwa lakini akashindwa kuchukua hatua. Taakuukuu i mean takukuru nao kupitia mkurugenzi mkuu waliwahi kuibuka na ngonjera za kuwapa muda wa kula krismasi kisha iwashughulikie, hadi leo kimyaaa.

Juzi katika uchguzi wa mkoa wa pwani vijana wa taakuukuu walishuhudia kwa macho yao wanaccm wakigawana rushwa lakini badala ya kuwakamata wao wakaamua kwenda kuripoti kwa mkuu wa mkoa. Hadi hapo tutakapoing'oa ccm ndipo tutpta raisi mwenye nia na uthubutu wa kupambana na rushwa.
 
sasa unaongelea hisia mimi sio mwanasiasa na sio mchumia tumbo
njoo ghorofa ya pili ministry of finance and economic affairs room no.302
office of commissioner of budget wagebill management and control nikuthibitishie haya nayokuambia..
Njaa kali itakuuua..

Kama kweli upo hapo unaishusha hadhi ofisi ya Serikali kwa uchangiaji unaoutoa - unategemewa kuwa mjumbe wa kuelimisha namna ya kujadili hoja sasa wewe ndio kwanza umeng'ang'ania udini. Unatakiwa kuelewa kuwa unachokisema ni hatari na kama hujui ni hatari sana.
 
maneno haya hayana mvuto kabisa kwenye nchi tunayoitaka. Kwa nini kila kitu unakigeuzia kwenye udini, ukabila, kwa nini usiongelee hoja bila kutaja udini tena, ' mkristo mwenzako' hiyo kitu ni ya nini. Tumetoka kwenye matatizo hayo, mbona bado unayapenda. Hebu siasa iseme siasa na dini itasemwa kwake.


tusipolikemea hili mapema baadae tutashindwa kabisa kulidhibiti
 

JK aingia woga
• Amtumia Mwandosya kujisafisha

na Happiness Mtweve
Tanzania Daima



HATUA ya Rais Jakaya Kikwete kueleza mshangao wake kuhusu vitendo vya rushwa kupenya katika chaguzi zinazohusisha wanawake ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imepokewa kwa hisia tofauti na makada wa chama hicho na wadadisi wa masuala ya siasa, Tanzania Daima Jumatano limebaini.

Kikubwa kinachoonekana kuwashtua wafuatiliaji wa siasa ndani ya CCM ni hatua ya Rais Kikwete kutoa kauli ya mshangao pasipo kuonekana akichukua hatua zozote za kukabiliana na vitendo vya rushwa ambavyo yeye mwenyewe anakiri kwamba vinahatarisha uhai wa chama hicho.

Mmoja wa makada wa muda mrefu serikalini na ofisa wa juu mstaafu wa moja ya taasisi nyeti za dola, amelieleza Tanzania Daima Jumatano kwamba, kauli ya Kikwete imeonyesha namna kiongozi huyo anavyojitanabahisha kwa namna tofauti na ilivyopata kufanywa na watangulizi wake watatu.
Ofisa huyo ambaye kama walivyo wengine wanne waliozungumza na waandishi wa gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa kwa majina yao, alisema Rais Kikwete ambaye ndiye mwenyekiti wa taifa wa CCM alipaswa kutoa kauli ya kukemea, karipio na yenye mamlaka dhidi ya wagombea wanaotoa rushwa katika chaguzi zinazoendelea ndani ya chama hicho.
Kwa mujibu wa ofisa mwingine mstaafu, kitendo cha rais kutoa kauli zinazobadilika badilika kuhusu rushwa huku akiwa na mamlaka ya kuwachukulia hatua watuhumiwa wa vitendo hivyo hususan ndani ya serikali na katika vikao vya chama anavyoviongoza, ni dalili za woga wa kuchukua maamuzi sahihi.

"Rais wangu ni mtu wa kushangaza na mwoga. Amepata kusema anawafahamu wala rushwa kwa majina. Ni huyu huyu aliyewahi kutamka kuwa siku za wala rushwa zinahesabiwa na leo anasema eti anashangaa kusikia hata wanawake wanajihusisha na rushwa katika uchaguzi," alisema kada mwingine mwandamizi ndani ya CCM.

Duru za siasa kutoka ndani na nje ya chama hicho tawala, zinasema kuwa kwa hali ilivyo sasa, CCM inaweza kufa kama isipofanya mabadiliko makubwa yatakayosaidia kudhibiti hali hiyo.

Tangu kuanza kwa uchaguzi huo wa chama hicho ngazi ya shina hadi taifa, kumekuwa na malalamiko kila kona ya kukithiri kwa vitendo vya rushwa, huku watuhumiwa hao wakipitishwa na vikao vya juu na kuibuka na ushindi.
Tayari baadhi ya vigogo walioanguka katika uchaguzi wa ndani ya CCM katika ngazi tofauti, wamekuwa wakizungumza chini kwa chini kwamba kuongezeka kwa kasi ya vitendo vya rushwa ndani ya chama imetokana na udhaifu wa Rais Kikwete kushindwa kuchukua hatua kudhibiti hali hiyo.

Akihutubia Mkutano Mkuu wa Nane wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) wa CCM juzi, Rais Kikwete aliishia kuonya juu ya vitendo vya rushwa vinavyozidi kushamiri ndani ya chama hicho, akisema kuwa visipochukuliwa hatua mapema, kuna hatari ya kukifikisha chama katika hatua mbaya.

Hakuishia hapo, alikwenda mbele zaidi na kusema, imekuwa ni hulka sasa hasa baada ya kumalizika chaguzi kwa wanachama kuendeleza na kuwekeana uhasama kama uliokuwepo wakati wa kampeni na wengine kuwaadhibu ambao hawakuwachagua hali ambayo ni mbaya sana kwa mustakabali wa chama.

Rais Kikwete aliwaasa wagombea wa nafasi mbalimbali wa UWT walioshindwa kutoweka visasi na walioshinda kutowapiga vijembe walioshindwa kwani kazi iliyo mbele ni kubwa kutokana na CCM hivi sasa kukabiliwa na hali ngumu ya ushindani wa kisiasa.

"Kweli tusipokemea vitendo hivi na kuviacha vikiendelea, tutakipeleka chama mahali pabaya, ninasikitika sana kusikia hata wanawake sasa wanajihusisha na utoaji rushwa ili kununua nafasi za uongozi kitu ambacho ni hatari sana," alisema Kikwete.

Alifafanua kuwa chama kinapoelekea si kuzuri ni lazima zifanyike jitihada za mabadiliko.
Katika hatua nyingine, Rais Kikwete ameonyesha kutishwa na nguvu na kasi kubwa ya vyama vya upinzani.

Alisema wakati CCM ikichafuka kwa rushwa, vyama vya upinzani vimekuwa vikijiimarisha kisiasa hali ambayo inakifanya chama chao kiwe katika wakati mgumu.
Kutokana na hali hiyo, Rais Kikwete alizihimiza jumuiya za chama hicho kuongeza juhudi na kujipanga kupambana na hali hiyo kwa lengo la kuiwezesha CCM kushinda uchaguzi wa mwaka 2015.
 
yaani kikwete ni mtu msanii sana. yeye anawasema wengine wanatoa rushwa kwenye kupata cheo na je yeye kwenye chama chake kumchagua GAIDI LA UFISADI lowassa kwa uhalisia do you think he struggled with out using rushwa!!! TENA BORA KUTOA RUSHWA, KULIKO KUPOKEA RUSHWA!!! upo uwezekano kikwete akawa mpokeaji mzuri wa rushwa kutokana na viashiria fulani !!!
 
Inasikitisha kuona Rais na Mwenyekiti wa CCM eti anashangaa taasisi za CCM kuandamwa na rushwa. Rais analalamika na kuwaomba kuacha rushwa badala ya kuchukua hatua.

Kweli inatisha na kusikitisha
 
Katika hali inayoonyesha kushindwa kwa Mwenyekiti wa CCM Rais JK, ameamua kumuachia Mungu matatizo yanayoikabili CCM hasa swala la rushwa.

Akifungua mkutano mkuu wa UVCCM jana rais kikwete aliwaonya vijana kukataa kutumiwa na kuepuka kuchaguana kwa misingi ya rushwa. Alisema kama na nyinyi mtashindwa 'Mungu ibariki CCM'. Kwamba kama na vijana nao watashindwa kudhibiti rushwa, sasa aachiwe Mungu.

Maoni yangu:
Nadhani kwa CCM ilipofika JK hawezi kuirudisha kwenye mstari na ni kweli anatakiwa badala ya kufanya ziara nyingi za nje ashinde msikitini amwombe Mungu akinusuru chama hicho kinachokata roho. Pole JK.
 
Back
Top Bottom