Kauli ya Chagulani dhidi Manyerere (Council Mwanza) ni sahihi kwa afya ya CHADEMA?

vijana nao wawe na subira, haraka za nini? sidhani kama kuna haja ya kila kitu wakapewa vijana, lazima wajifunze kuwa wavumilivu.... nadhani wote tunakumbuka issue ya JK an Slaa, ni ukweli ulio wazi kuwa ukomavu wa Dr ulisaidia sana tusiingie kwenye machafuko baada ya uchaguzi wa 2010.... nadhani walichofanya CC ni sahihi juu yao....
 
Ukomavu gani wewe, alishaona kuwa ameshindwa. Ukomavu anao Zitto na Mbowe.
 
usikurupuke!Hivi huyo Meya ni Engineer?sasa standard za ujenzi wa barabara meya anahusikaje?Mhandisi wa ujenzi Mkoa,Mhandisi wa ujenzi Tanroad,na mhandisi wa ujenzi Wilaya ya Ilemela pamoja na Matechnician wao wanafanya kazi gani au ulikuwa unataka meya akasimamie hiyo kazi?yeye anachotakiwa kuangalia ni je project inaenda kwa muda kama ilivyokubaliwa.hayo mengine ni political tu unaongea.Pili nafikiri kama kuna matatizo ndani ya nyumba yako huwezi kwenda kuyaeleza kwa majirani kabla ya wewe na mkeo kuyatatua kwanza.
 
Kwa hili la mwanza CDM naomba muwe makini sana na madiwani wenu.

Ktk majimbo ambayo ccm wanajutia kuyapoteza ni ilemela na nyamagana.mkakati wa ccm kuwanunua madiwani wenu ulianza ktk uchaguzi wa meya.

Isingekua busara za viongozi wenu umeya mngeusikia tu.Wengi wa madiwani wenu hapa mza si watu makini waligombea kwa kubahatisha.mfano diwani wangu sikuwahi kuona akipiga kampeni ila siku 1 tu alipokuja wenje kuomba kura naye akatokezea hapo.

Wengi wa madiwani hawa elimu yao ni duni hawana kipato na wamepigika ki maisha, unategemea nini kwa madiwani km hawa kuhimili vishawishi kutoka upande wa pili. Ni rahisi kwa kijana mdogo kama chagulani kuasi kwa kuahidiwa hata ukuu wa wilaya.

Pia unategemea nini kwa diwani wa kitangiri ambaye alishindwa ccm na kuhamia cdm. Sisi wana Mwanza tunaamini kuwa 2015 cdm watajitokeza watu makini kugombea nafasi hizo.kama hawa waliotaka kujaribu, tuliwapa kura basi itakuwa rahisi zaidi kwa watu makini kwa uchaguzi ujao.

Mungu ibariki mwanza,Mungu ibariki Tanzania

Well stated mkuu, ama kweli wewe ni mtabiri na maono yako yametimia, Chagulani na meya wa Kitangiri wameadabishwa, so nafasi zpo wazi
 
“Mimi ninataka niseme ukweli kwa sababu siogopi mtu, mimi ni taasisi inayojitegemea, sina imani na wewe mwenyekiti (Meya wa Jiji la Mwanza), umekuwa hufuati kanuni, utaratibu wako wa kuendesha vikao kila mara unataka kusababisha vurugu, ninataka baada ya hapa nipewe karatasi mimi nitakuwa wa kwanza kuandika jina langu ili nipate idadi ya madiwani 10 wanaoweza kuleta hoja kuomba tukupigie kura ya kutokuwa na imani na wewe,” alisema diwani huyo kijana.

Habari zaidi soma hapa Raia Mwema - CHADEMA yatikisa mashabiki wake

Hii ni kauli ya Chagulani kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani wa Jiji la Mwanza alipowataka Madiwani wapige kura ya kutokuwa na imani na Meya wa Jiji hilo Bw. Josephat Manyerere (CDM). Kwenye orodha ya waliosaini kumpiga chini meya Manyerere jina la Chagulani ni la kwanza, kisha linafuatiwa na mwenzake Matata halafu wanafuata madiwani wa CCM na CUF. Hakuna jina la diwani mwingine wa CDM aliyesaini.

My Take:
1. Ni Kweli Chagulani hakutakiwa kuogopa wala kujali chochote na kwamba yeye ni taasisi inayojitegemea? Hana taasisi (Chama) kilichomu-endorse ambacho alipaswa kuongozwa na katiba, sheria na taratibu zake? Si kwamba, hii ni jeuri kuu ambayo haieleweki ni wapi inatoka?

2. Kwa nukuu hii si kwamba, Bw. Chagulani alikuwa anatekeleza mradi aliotumwa na CCM? Kitendo cha yeye kuanza kwa kujihami kuwa, haogopi mtu na kwamba yeye ni taasisi huru inayojitegemea kinatafsiriwa wazi, alikuwa na maelekezo kichwani kutoka kwa chama chake yaani CDM lakini alikaidi makusudi pengine ni kutokana na yeye kuwa na mradi aliokuwa anautekeleza (Bila shaka kuupata umeya/malipo kutoka CCM)

Tujadili.
 
Nafikiri mamluki wa CCM sasa ni muda wa kuumbuka. Chadema ni zaidi ya ujuavyo, wana mtandao mkali watakuumbua tuu, chezea Chadema wewe.
 
Mpaka sasa nimeona kwamba JKT lilikuwa la muhimu sana. Hili lilifundisha maadili na uvumilivu katika maisha na jinsi ya kukabiliana na jazba.
 
Kiukweli wakati mwingine CDM wanajitahidi kuwa wavumilivu sana, labda kwakuwa wengi wa viongozi wake ni vijana na wanamihemuko ya hali ya juu. Chagulani amekikuta chama kimesimama ambacho hajashiriki kukijenga hata kama kuna mambo hukubaliani ni vema kuwa na staha kidogo, lakini jeuri kama hiyo sidhani kama itamsadia hata huko atakokwenda
 
hajitambui huyu dogo,angejua asingejiamini kiasi hicho,let him dance to the tune he is listening to!
 
“Mimi ninataka niseme ukweli kwa sababu siogopi mtu, mimi ni taasisi inayojitegemea, sina imani na wewe mwenyekiti (Meya wa Jiji la Mwanza), umekuwa hufuati kanuni, utaratibu wako wa kuendesha vikao kila mara unataka kusababisha vurugu, ninataka baada ya hapa nipewe karatasi mimi nitakuwa wa kwanza kuandika jina langu ili nipate idadi ya madiwani 10 wanaoweza kuleta hoja kuomba tukupigie kura ya kutokuwa na imani na wewe,” alisema diwani huyo kijana.

Habari zaidi soma hapa Raia Mwema - CHADEMA yatikisa mashabiki wake

Hii ni kauli ya Chagulani kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani wa Jiji la Mwanza alipowataka Madiwani wapige kura ya kutokuwa na imani na Meya wa Jiji hilo Bw. Josephat Manyerere (CDM). Kwenye orodha ya waliosaini kumpiga chini meya Manyerere jina la Chagulani ni la kwanza, kisha linafuatiwa na mwenzake Matata halafu wanafuata madiwani wa CCM na CUF. Hakuna jina la diwani mwingine wa CDM aliyesaini.

My Take:
1. Ni Kweli Chagulani hakutakiwa kuogopa wala kujali chochote na kwamba yeye ni taasisi inayojitegemea? Hana taasisi (Chama) kilichomu-endorse ambacho alipaswa kuongozwa na katiba, sheria na taratibu zake? Si kwamba, hii ni jeuri kuu ambayo haieleweki ni wapi inatoka?

2. Kwa nukuu hii si kwamba, Bw. Chagulani alikuwa anatekeleza mradi aliotumwa na CCM? Kitendo cha yeye kuanza kwa kujihami kuwa, haogopi mtu na kwamba yeye ni taasisi huru inayojitegemea kinatafsiriwa wazi, alikuwa na maelekezo kichwani kutoka kwa chama chake yaani CDM lakini alikaidi makusudi pengine ni kutokana na yeye kuwa na mradi aliokuwa anautekeleza (Bila shaka kuupata umeya/malipo kutoka CCM)

Tujadili.

Dogo kalewa sifa kama anafikiri yeye ni taasisi angegombea udiwani bila chama.Nilimsikia juzi akijitea eti mbona zitto na makamba ni marafiki.poor chagulani umepoteza sifa za kuwa kiongozi
 
Ama! Yaani alisema yeye ni taasisi? Mimi sijawahi sikia hii maneno..........is he
a legion within?!
 
Back
Top Bottom