Kauli ya Chagulani dhidi Manyerere (Council Mwanza) ni sahihi kwa afya ya CHADEMA?

Haya tumekusikia, kingine...?
Unganisha mengine mengi, maana huku kutumikishwa mpaka utoe kitu kitakacholingana na malipo iko kazi.
Ukikwama omba tukusaidie kuunganisha mengine.
 
unajua hii migogoro inayojitokeza haina maslahi kwa taifa japo yanatuonesha taswira nzima ya chama hiki mapema, kiukweli hiyo migogoro yote ni maslahi binafsi ambayo wengi wao ni waroho na kujitafutia umaarufu.kuna mengi mno yataendelea kujitokeza, na wasira alisha yatabiri hayo.
 
Bila shaka wengi katika wachangiaji naona wamekubaliana na Mwenyekiti wa Chadema kuwa migogoro yao kwenye chama haijadiliki...!
 
CHADEMA is bigger than a single individual. Wapo madiwani waliopata vyeo kwa sababu tu walikuwa CHADEMA lakini wao binafsi hawauziki na kama sio CHADEMA wangekuwa mtaani. Sasa wameingia jikoni wanataka ku-rewind tabia zao. Bahati mbaya ni kwamba umma wa Tanzania ndio unatoa adhabu.

Huyo Diwani huko Mwanza anaweza kuandika essays anavyotaka lakini akumbuke bila 'Brand-CHADEMA' kwenye uso wake is nothing. Ukisoma waraka kuhusu Wenje hauna kitu hasa kikubwa cha kuleta mtafaraku mkubwa hivyo. Pengine amepewa kitu na Team Wassira na kwa muda alikuwa anatafuta mahali pa kuchomeka lakini azma yake ni kuvuruga chama. He will go with the wind.
 
The horse umefunga kazi. Hakuna hata gwanda mmoja anaeweza kusema kwi, au kujaribu kujibu hoja. Tazama watakavyoanza kukuvaa wewe badala ya hoja zako.

Na mashambilizi yote yataanzia kulekule kutoka kwa wanaodhani wao ni "UNTOUCHABLE DOMINANCE".
 
Nawashangaa watu wa aina ya 'the horse' wanaoamini kwamba CDM lazima isambaratike kama vile NCCR au CUF. Kwa taarifa ya watu hawa CDM ni kitu kingine kabisa, kina viongozi na Wabunge makini, wasomi nk.

Watu kama akina Shibuda hawatateresha chama ambacho Watanzania wamekikubali, kwani ukilinganisha CCM na CDM, CDM ndiyo mkombozi wao kwani magamba wameshindwa kuboresha maisha yao.

Hata kauli za kusema ati CDM nao wakishika nchi watashindwa tu kama CCM tu hazina ushahidi wowote, lakini ushahidi wa CCM kushindwa tunao.

Hebu nikumbushe uchaguzi wa Rais nani alishinda vile ? CDM kina wabunge wangapi vile ? Mkuu wa nchi ni nani na chama tawala ni kipi vile ? Ukiyajibu haya kwa usahihi utapata jibu la watanzania:bange::bange:

 
the horse

Hiyo ndio Demokrasia maana kila mtu anayo haki ya kusema atakacho na Chadema wanaonyesha njia kwa kuwaachia watu waseme wawezavyo ili sisi wananchi tuweze kupambanua kama huyo anayesema anafaa kuwa kiongozi au la.

Kama mtu akisema jambo ambalo ni upuuzi basi liende na upepo. Mfano mzuri ni Shibuda. Alisema upuuzi wake na umeona namna viongozi wa ukweli ndani ya CDM walivyokaa kimya,maana mazingira aliyotumia kusemea jambo lake yalimfanya na yanamfanya aonekane nunda tu
 
Last edited by a moderator:
Swala la mawasiliano kwa hawa vijana viongozi wa chadema nadhani ni changamoto kwa viongozi wao hata zile semina elekezi za madiwani na Katibu mkuu wa chama hazikuwasaidia,Chagulani mawasiliano ni muhimu katika safari ya kisiasa malingo ya kujiona wewe ndiye unayejua katika timu ni hatari sana nadhani msaaafu wako hauna jipya zaidi ya kujikosha uko kwenye timu chama chako kikiboronga kimeboronga kwa hiyo saidia kupunguza mapungufu kwa kumsema utakavyo huyo meya kwenye vikao vyenu lakini usitafute sympathy ya public mawili itakujenga au kukubomoa yote tisa
 
Nawashangaa watu wa aina ya 'the horse' wanaoamini kwamba CDM lazima isambaratike kama vile NCCR au CUF. Kwa taarifa ya watu hawa CDM ni kitu kingine kabisa, kina viongozi na Wabunge makini, wasomi nk.

Watu kama akina Shibuda hawatateresha chama ambacho Watanzania wamekikubali, kwani ukilinganisha CCM na CDM, CDM ndiyo mkombozi wao kwani magamba wameshindwa kuboresha maisha yao.

Hata kauli za kusema ati CDM nao wakishika nchi watashindwa tu kama CCM tu hazina ushahidi wowote, lakini ushahidi wa CCM kushindwa tunao.
The Horse wako wengi. Umemsikia Wassira naye akiota kuwa baada ya mwaka mmoja Chadema itasambaratika na kabla hata wiki kumalizika yeye akasambaratishwa kule kwao na maswali aliyoshindwa kujibu.
 
Hawa wapuuzi wanao quote thread nzima nitawatukana nyie mbona hamuelewi lakini K...........zenu.Mnashindwa kuchangia bila kufanya hivyo.Pambaf
 
umejitshidi sana kutafutiza migogoro yaelekea hata maana/tafasiri sahihi ya neno migogoro huijui
 
HATIMAYE yametimia STAR TV Mwanza sina shaka haya mtayafanyia kazi kesho katika Tuongee asubuhi tupate ukweli wa mambo kwa kina. Nilikuona Yahya Jumapili iliyopita ulikuwa na CHAGULANI Tafadhali mualike tena. Hatuhitaji uozo CDM atuambie lipi ni lipi nas tupate fursa kuchangia hapa.

ADIOS
 
Cha msingi hapo ni usafi na uadilifu wa mtu,haijalishi ana toka CDM au CCM.CDM wao wanapinga ufisadi hivyo basi ni bora kwanza kutoa boriti kwenye jicho lako ndipo utaweza kuona kibanzi kwenye jicho la mwenzako.Manyerere ana jaribu kuchafua na kuharibu M4C,lazima chama kimjadili ikibidi kimfungulie kesi na achunguzwe yawezekana ana elements za kifisadi
 
hofu yangu hapa ni unafiki wa CUF na MAGAMBA chagulani anaweza kuwa alikuwa na malengo yenye maslahi mazuri na manispaa ingawa anayo pia dhamira ya nafasi iliyojificha akajikuta hajawahi kumrekebisha hata mara 1 huyu meya na wala hajawahi hata mara0 kupendekeza chochote ndani ya chama chake ila akawa anasubiri ni lin na wapi meya atakosea ili acheze naye mashabiki atawapata sana ila sasa je ana uhakika wa nafasi hii kurudi CHADEMA UPO? 2 upeo wa wapiga kura na tfsiri zao pia ni kwamba oooh CDM HAWA BORA CCM HAWA WANA MALUMBANO WATCH OUT CHADEMA AND CHAGULANI
 
Back
Top Bottom