Chadema mnashindwa kusimamia Jiji la Mwanza kweli mtaweza kulisimamia taifa letu la Tanzania.
Meya wa Mwanza ni Chadema.
Mbunge wa Mwanza ni Chadema.
Madiwani wengi wa Mwanza ni Chadema.
Halmashauri ya Jiji la Mwanza ipo chini ya Chadema.
Miradi yote ya Jiji la Mwanza inapitishwa na madiwani wa Chadema.
Leo hii Chadema hawapatani wenyewe kwa wenyewe, cha kuchekesha wakiulizwa tatizo nini wanasema ni CCM.
Chadema bado sana kwenye masuala ya kiutawala.
Nikisimama kutoka kwenye maelezo yako, maoni yangu ni kwamba watanzania tuwe makini sana, hawa viongozi wa CHADEMA ni binaadamu na wanaweza kukosea kama wanavyofanya viongozi wa Magamba, tunachotakiwa kusimamia ni Mabadiriko na Uwajibikaji, kama kiongozi haridhishi katika utendaji wake sioni sababu ya kumtetea eti kwa vile ni CHADEMA, hizi ni tabia typical kabisa za CCM.Mi nadhani hoja ya msingi hapo ni madhaifu ya huyo meya na jinsi anavyokigharimu chama katika siasa za kanda ya ziwa!!!
Ni sahihi kumpigia kura ya kutokuwa na imani anatuchelewesha sana, pia alionyesha kutokuwa na uwezo toka mwanzo na akawapa waandishi wa habari ya kusema.
Hilo la makundi sijui ila naona kuna hoja za msingi tu katika kuzingatia usimamizi na kuonyesha uongozi wa manispaa, huyo meya wa saiv kashindwa sana kwa kweli.
Kimsingi Chagulani hajatumia busara hata kidogo na hakuma sababu ya msingi ya kumtetea Chagulani!