Kauli ya Chagulani dhidi Manyerere (Council Mwanza) ni sahihi kwa afya ya CHADEMA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli ya Chagulani dhidi Manyerere (Council Mwanza) ni sahihi kwa afya ya CHADEMA?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GHOST RYDER, May 18, 2012.

 1. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  JF UP-CLOSE: KAULI YA CHAGULANI DHIDI MANYERERE COUNCIL MWANZA NI SAHIHI KWA AFYA YA CDM?

  Katika kikao cha Bajeti cha Halmashauri ya Jiji la Mwanza Mei 15, Diwani wa Kata ya Igoma CDM Mh. Adam Chagulani ametamka kutokuwa na imani na Meya wa Jiji hilo Mh.Jackson Manyerere kwa madai ya kuwayumbisha katika vikao hivyo.

  Akionyesha kutomuunga mkono Meya huyo, Chagulani aliiitisha kufanyika kwa zoezi la kukusanya saini za madiwani kutosheleza idadi inayokubalika kisheria kupitisha mswaada wa kupiga kura ya kutokuwa na imani na Manyerere ambaye ni kada mwenzie wa CHADEMA.

  Chagulani ambaye katika kinyang'anyiro cha kusaka Meya wa Jiji hilo alikuwa akipewa nafasi kubwa kutoka kambi ya CDM kabla ya maamuzi ya hekima yaliyotumika baada ya kuzuka kambi mbili ambazo bila shaka zingeishia kuuweka rehani umeya kwa mgombea wa CCM Stanslaus Mabula ambaye alikuwa na kiu kubwa ya dhamana hiyo, anaonekana dhahiri bado anateswa na jinamizi hilo kwa kauli ambazo sijui tafsiri yake ni nini kwa afya ya chama.

  Akizungumza kwa hisia na kuungwa mkono na madiwani wa CCM na CUF chagulani alimhoji Manyerere, '' Mweyeketi kwa nini tusisign petition ya kutokuwa na imani na wewe kwa kuwa umekuwa ukituyumbisha kila mara'' alimaliza chagulani na kushangiliwa kwa nguvu na kambi ya CCM na CUF katika baraza hilo.

  Kama haitoshi Stanslaus Mabula nae hakuwa nyuma kwa kumrushia tuhuma Meya huyo kuwa amekuwa akikiuka mara kwa mara taratibu za chama kwa kutoa nje ya vikao mijadala inayohusu halmashauri hiyo na kujadiliwa katika vikao visivyokubalika kisheria.

  UP-CLOSE DEBATE:

  1. Uko wapi umakini katika hatua hii ya Adam Chagulani Diwani wa Igoma CDM?

  2. Hakulijua hili mapema Mh. Wenje ambaye alikuwepo katika kikao na alisimama kidete kuonyesha mapungufu ya Bajeti iliyopita ya 2011/12 na kuelezea hakuna sababu ya kujadili Bajeti ya 2012/ 13 wakati iliyopita imejaa madudu?

  3. Saini 16 zimepatikana kutimiza Column ya kupiga kura ya kutokuwa na Imani na Meya Mh. Josephat Manyerere, Nini hatima ya zoezi hili na nani hasa anayeandaliwa kushika wadhifa huu?

  4. Ni kweli sasa dalili za kambi mbili ndani ya CDM zinataka kushika hatamu au ni uchu tu wa madaraka wa baadhi ya makada wa CDM?

  5. Mkakati wa kitaifa wa chama unayatazamaje haya?Karibu katika mjadala huu Mh. Mnyika, Mrema kwa Misimamo ya Chama.

  VIDEO YA TUKIO HILI NIMEIDAKA KATIKA LINK INAYOONEKANA HAPA CHINI  ADIOS

  NEXT WEEKJF UP-CLOSE: UONGOZI UNAHITAJI VIPAJI AU TAALUMA?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mi nadhani hoja ya msingi hapo ni madhaifu ya huyo meya na jinsi anavyokigharimu chama katika siasa za kanda ya ziwa!!!

  Ni sahihi kumpigia kura ya kutokuwa na imani anatuchelewesha sana, pia alionyesha kutokuwa na uwezo toka mwanzo na akawapa waandishi wa habari ya kusema.

  Hilo la makundi sijui ila naona kuna hoja za msingi tu katika kuzingatia usimamizi na kuonyesha uongozi wa manispaa, huyo meya wa saiv kashindwa sana kwa kweli.
   
 3. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Well said Mkuu, Mjadala uko wazi sasa.
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Adam Chagulani,,,dah huyu jamaa kwa waliosoma UDSM wanamkumbuka sana hasa kuanzia 2008-2011,alikua ni katibu kama si mwenyekiti wa hall II,mkandala anamtambua huyu na aliyekua warden wa hall II anamtambua,Chagulan ana uwezo wa kuzungumza na kupanga hoja,,,,na kama atakua meya wa mwanza,,,,basi mkuu wa mkoa na mkurugenz wa jiji wajipange na changamoto za CHAGULANI,,,,chagulani ndio product moja na silinde,owawa
   
 5. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Huyu Mayor wa Mwanza ni dhaifu sana, very bad representation kwa siasa za upinzani. Wananchi hatuoni tofauti na wale viongozi walaji wa CCM. Angalia jinsi Nyanza road wanavyoboronga katika ile barabara ya Buzuruga to Pansiasi, haijulikani wanajengwa kwa kiwango gani lakini mayor ametulia kama mwana ccm. Heri meya wa Mwanza angekuwa wana ccm tungetupia lawama magamba lakini hapa CDM itapata wakati mgumu sana 2015 maana hadi sasa hakuna cha kujivunia rock city, same dirty stuffs kama wakati wa ccm
   
 6. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #6
  May 19, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Kukatikakatika kwa JF kwa sasa kunaathiri sana mijadala kama hii itabidi tuwapenyezee na watu wa Magazeti na TV kutanua wigo wa JF kupata audience kubwa
   
 7. Naibili

  Naibili JF-Expert Member

  #7
  May 19, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,681
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  hapa kuna mawili swala la makundi na hoja ya chagulani, binafsi naona hoja ya chagulani ina mashiko cha msingi Dr. slaa afanye jambo la mbolea kulishughulikia hili kwani matatizo ya chagulani anayafahamu vizuri, maana kuna taarifa pia kuwa diwani huyu haelewani na Wenje hii inapelekea kumuona kijana huyu kama bado ana makovu ya kwenye uchaguzi lakini ukweli ni kuwa meyor ana matatizo yake, kama ana matatizo aondolewe tu tusifuge matatizo kama wafanyavyo magamba
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #8
  May 19, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  wakati anachaguliwa Manyerere wakati marehemu NOVATH MANOKO yu hai ilikuwa shughuli nzito hasa kumpitisha hadi busara PhD kutumika kusawazisha mambo na kuondoa mpasuko uliokuwepo wakati huo, licha ya ufinyu wa madarasa lakini Marehemu Manoko alikuwa Makini sana kupewa nafasi hiyo wakati huo kwa sie tunayemfahamu toka miaka ya 90.

  Huyu jamaa alikuwa mpiganaji sana. R.I.P kamanda.

  Endapo Chagulani ambaye nasikia kanyang'anywa kadi ya chama tayari akifanikiwa azimio hili, majaaliwa ya chama yatarejea square zero kama kabla ya uchaguzi huo
   
 9. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #9
  May 19, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Kimsingi nakubaliana na wewe lakini madhaifu ya Meya yanashindikanaje kudhibitiwa katika mfumo imara wa CDM ambao unahitaji zaidi kufuata misingi ya chama kuliko utashi wa mtu binafsi?
   
 10. Naibili

  Naibili JF-Expert Member

  #10
  May 19, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,681
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  hapo kwenye red ndipo mkanganyiko unapoanzia kanyang'anywa kadi kwa kosa gani? maana tatizo la mwanza ni wanachama wengi hasa wanaohudhuria vikao vya chama kwenye matawi bado wana element za kimagamba!

  naamini kijana ni mwelewa wakae nae chini haya mambo wayamalize kwenye vikao vya chama.
   
 11. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #11
  May 19, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Huu mjadala mzui sana!

  Huyo Mayor kwa jinsi ninavyomuona ni janga kabisa ila Chagulani naye haaminiki!
   
 12. k

  kitenuly JF-Expert Member

  #12
  May 19, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 336
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tufafanunulie hayo madhaifu ya mayor, hapo ndo tutaweza jenga hoja, fungua hiyo link Sakata la MEYA Mwanza.mpg - YouTube au Sakata la MEYA Mwanza.mpg - YouTube kuna taratibu zinazotakwa kukiukwa ili kufunika ubadhilifu. hivyo kama unajua madhaifu mengine ya mayor ebu fafanua zaidi.
   
 13. k

  kitenuly JF-Expert Member

  #13
  May 19, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 336
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna lolote si mwelewa lolote, angekuwa mwelewa angekijenga chama, kwa kujadili kabla ya kukkurupuka, huyu anaelement za ubunafsi sana
   
 14. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #14
  May 19, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Hi chelewa chelewa kuwachukuwa hatua juu ya mambo kwa wakati muafaka ndiyo ilioifikisha ccm hapo ilipo.
   
 15. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #15
  May 19, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,804
  Likes Received: 1,119
  Trophy Points: 280
  Siasa ni mambo ya kijinga sana.
   
 16. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #16
  May 20, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Moderators mmeunyima mjadala huu profile kwa kuuhamishia habari mchanganyiko wakati mie nilipost jukwaaa la siasa kwa wapiga siasa wenzangu tujadiliane sijui lengo ni lipi au hii kwenu si siasa. Mnatuvunja moyo kusaka details hot.
   
 17. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #17
  May 20, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Uchu wa madaraka unazidi kuitafuna Chadema Mwanza, mnazidi kuwachanganya wananchi wa Mwanza waliwapa madaraka ya kutawala jiji la Mwanza.
   
 18. U

  Ukana Shilungo JF-Expert Member

  #18
  May 20, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 911
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 60
  alili
  Aksante mdau kwa youtube na maelezo hayo,kama ni hivyo ni hatari,nina mashaka kuna dalili za usaliti na uroho wa madaraka,dawa pekee ni kushikisha adabu madiwani wa Chadema huenda ni mbinu za magamba kuleta mgogoro kwani uongozi wa cdm jiji la Mwanza unawanyima raha sana magamba.
   
 19. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #19
  May 20, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sijaacha kuamini bado kama hapa haupo mkono wa magamba
   
 20. n

  nyangasese Senior Member

  #20
  May 20, 2012
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa hili la mwanza CDM naomba muwe makini sana na madiwani wenu.

  Ktk majimbo ambayo ccm wanajutia kuyapoteza ni ilemela na nyamagana.mkakati wa ccm kuwanunua madiwani wenu ulianza ktk uchaguzi wa meya.

  Isingekua busara za viongozi wenu umeya mngeusikia tu.Wengi wa madiwani wenu hapa mza si watu makini waligombea kwa kubahatisha.mfano diwani wangu sikuwahi kuona akipiga kampeni ila siku 1 tu alipokuja wenje kuomba kura naye akatokezea hapo.

  Wengi wa madiwani hawa elimu yao ni duni hawana kipato na wamepigika ki maisha, unategemea nini kwa madiwani km hawa kuhimili vishawishi kutoka upande wa pili. Ni rahisi kwa kijana mdogo kama chagulani kuasi kwa kuahidiwa hata ukuu wa wilaya.

  Pia unategemea nini kwa diwani wa kitangiri ambaye alishindwa ccm na kuhamia cdm. Sisi wana Mwanza tunaamini kuwa 2015 cdm watajitokeza watu makini kugombea nafasi hizo.kama hawa waliotaka kujaribu, tuliwapa kura basi itakuwa rahisi zaidi kwa watu makini kwa uchaguzi ujao.

  Mungu ibariki mwanza,Mungu ibariki Tanzania
   
Loading...