Kauli wanazopenda wanaume kuzisikia kwa wenza wao

Kanungila Karim

Verified Member
Apr 29, 2016
16,603
2,000


HAKUNA kitu kizuri kwenye uhusiano kama kujua mwenzako anapenda nini. Unapomjua mwenzako anachokipenda, itakusaidia katika suala zima la kudumisha uhusiano. Ukimfanyia yale anayoyapenda, sio kwamba atafurahi tu bali unamtengenezea kumbukumbu nzuri. Unatengeneza sifa njema kwa mwenzi wako. Anakuona umuhimu wako, anatambua utu wako na kukupa thamani ya kuwa mwenzi wake wa maisha.

Ule ubinadamu au mambo mazuri unayomfanyia mwenzi wako ndio silaha yako ya kumfanya azidi kukupenda. nakuweka kwenye nafasi nzuri ya mwenza wako kukupa thamani kama ambayo wewe unampa. Kukufanyia mema kama au zaidi ya yale ambayo wewe umekuwa ukimfanyia. Ndio maana leo nakuja na mada hii, mambo matano ambayo wanaume wanapenda kuyasikia kutoka kwa wanawake.

KUHITAJI MSAADA

Kwa uhalisia, mwanaume anapenda kuwa anahitajika hivyo mwanamke anapomuambia anahitaji msaada wake, anajisikia amani kabisa. Anajua ni wajibu wake kumsaidia mwanamke wake. Kumbe basi, unapokuwa na mwenzi wako onesha kwamba unamhitaji na unahitaji akusaidie mambo yako. Mathalan, unashindwa kuweka balbu. Unapomuambia; ‘baby naomba unisaidie kuweka hii balbu’ hakika hujisikia faraja sana. Mtaalamu wa saikolojia ya mapenzi, Tiya Cunningham- Sumter anasema; “Mwanaume anapenda kuona anahitajika kumsaidia mwenza wake.”

KUSIFIWA

Kwa kawaida, wanaume wengi wanapenda kusifiwa hususan na wenza wao. Wanaowapenda pale wanapokuwa wanafanya jambo fulani hususan lile la kumsaidia mpenzi wake basi atambue ile thamani kwa kusifiwa.

Mwanamke anapomsifia mwanaume wake huwa anajisikia faraja sana. Msifie mwanaume wako kwa kazi nzuri aliyofanya, inaongeza sana chachu ya kuzidi kukupenda. Mshauri wa mambo ya mapenzi, Carolyn Cole amewahi kusema; “Mwanaume anapenda kusifiwa kwa ujuzi hivyo mfanye ajue kwamba unatambua kwamba ni mzuri katika jambo fulani.”

MUELEZE ANAKUKOSHA

Hakuna kitu kizuri kama kumuambia mwanaume anakukosha kwa jambo fulani. Kama mwanaume wako anakufurahisha katika suala fulani, mueleze kwa kutumia lugha laini kwamba unajisikia furaha kuwa naye. Neno unajisikia furaha kuwa naye lina maana kubwa sana. Linaongeza morali ya mapenzi, linaongeza hamasa ya kuzidi kukufurahisha maana anatambua kuwa anapokufanyia jambo fulani unafurahia.

Wanaume wanapenda sana kujua kama wanachokufanyia kinakufurahisha hivyo anapofanya chochote kile ambacho unakipenda na kinakufurahisha, mueleze. Mwalimu wa masuala ya uhusiano Laura Bilotta amewahi kusema; “Kama mwanaume wako anakufanya uwe na furaha, muambie.”


AMEKAMILIKA

Mwanaume anapenda kuonekana amekamilika kwa kila kitu. Unapomueleza amekamilika, kwamba hakuna kitu ambacho atahitaji na ushindwe kukutimizia, inampa nguvu sana mwanaume. Pale unapoona amekamilika kama mwanaume katika kila idara, mfanye ajue. Mwambie kwa lugha ya kimahaba kwamba unamkubali na amekamilika kwa kila kitu. Hiyo itampa imani na kumfanya ajione ana thamani kubwa kwako. Atazidi kukupenda!

KUHESHIMIKA

Mwanaume anapenda sana kuona anaheshimika na mwanamke wake. Hivyo muoneshe kwamba unamheshimu, muoneshe kwamba unamthamini na unatambua mchango wake katika maisha yako. Unapomfanyia hivyo mwanaume lazima akupende. Lazima akuone mwenye thamani kubwa maishani mwake
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom