Kauli tata za viongozi wetu tukio la NMB - TMK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli tata za viongozi wetu tukio la NMB - TMK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fidel80, Aug 1, 2009.

 1. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #1
  Aug 1, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Jana wakati nafuatilia tukio zima la ujambazi katika Bank ya NMB tawi la Temeke {katika Luninga ITV nikiwa Bar} Kuna kauli za baadhi ya viongozi na watendaji wetu ziliamsha manung'uniko kwa baadhi ya member sehemu niliyo kuwepo pale. Nitanukuu
  Waziri Masha alitamka ".....ninafrahi kuona askari wangu wamefika eneo la tukio...."
  Kwa hiyo amefrahi lakini hao askari wake wamefanya nini?
  Je toka eneo la tukio na eneo la kipolisi mkoa wa Chang'ombe kuna umbali gani mpaka hao askari wake wakatumia dk 15 kufika katika eneo la tukio?
  Alafu akaja Kamanda Kova nae sijui alikurupuka au ulimi uliteleza au vp sikuelewa kwakweli namnukuu ".......tunao askari wa miguu ya magari...tumejidhatiti tutawakamata....."
  Hawa askari wa miguu ya magari ni akina nani? Au ndo yale yale ya kukariri?
   
 2. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #2
  Aug 1, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Hah hah hah....Alimaanisha Askari waliovalia Boot..kwa kikwao...!! Anadhani Askari akivaa Boot anakuwa na Speed ka Gari...!! Ooohlalal...Mbavu sina...!!
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Aug 1, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Hahahaha au wale askari kanzu wanao vizia magari yaliobeba mizigo wapate angalau posho wanakera wale.
   
 4. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #4
  Aug 1, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kumbe Askari polisi ni wa Masha siyo wetu sote?, Ndiyo maana wameshindwa kulinda wananchi na mali zao wanalinda viongozi na mali zao za kifisadi.

  Ukweli ni kwamba askari polisi nao ni binadamu, wanahitaji kuishi vile vile, huwezi kukurupa kichwa kichwa kama alivyokuwa akisema afande Tibaigana kuelekea eneo la kivita bila kuwa na uhakika ni nini kinaendelea.

  Halafu bongo kinachofanya kazi ya polisi kuwa ngumu ni vitendea kazi, hivi kama jamaa wanapatiwa magari ya delaya hawataogopa kufika eneo kwa kuogopa kumiminiwa risasi na mabomu, ila unapowapa defender lenye turubai unatarajia nini?,

  Kingine wananchi nao wanachangia ugumu, maana wakisikia risasi wanakimbilia kuangalia kuna nini?, hapo sasa ndipo inawafanya majambazi kutumia wananchi kama shield na kutokomea, maana askari wakirusha risasi ovyo watau innocents wanaoshangalia tukio. Cha muhimu ni Masha na wizara yake kutoa elimu kwa wananchi siyo kufika maeneo ya tukio na kutoa kauli za 2010 election.
   
 5. M

  Mvutakamba Member

  #5
  Aug 1, 2009
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna usanii , na pili kuna kula hadi ukalewa madaraka .Neno wizara yangu, askari wangu nk mh .
  Mabomu haya ni yale ya Mbagala jamaa waliokota kiasi ?
   
 6. B

  Bobby JF-Expert Member

  #6
  Aug 1, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,683
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Heri umeliona hilo H. Hii tabia ya tuliyowapa dhamana kutuongoza kujimilikisha vile tulivyowapa kuvisimamia huwa inaniboa sana. Kuna zile kodi zetu zilizomwagwa mikoani kiholela kwa jina la mabilioni ya nani sijuwi. I thought ni vyombo vya habari ndio vinavyomislead mpaka nilipomsikia mwenyewe akisema "nirudishieni pesa zangu mimi ndio mwenye pesa" mweshimiwa ni kwa mshahara upi huo mpaka uwe na mabilioni yote hayo? Jamani hizo ni kodi zetu tumewapa dhamana muongoze nchi hatujawapa nchi.
   
 7. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #7
  Aug 1, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Kwa mujibu wa BBC wanasema tukio ni la kwanza na la aina yake kwani majambazi walitumia mabomu ya mkono wakati wanataka kuiba na hivyo kusababisha mshtuko na tafrani miongoni mwa wateja na wafanyakazi wa bank na kisha wao kuiba.

  Poleni sana ndugu zetu.
   
 8. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #8
  Aug 1, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Kwa vile tukio ni la kwanza na la aina yake Je polisi ndo wasifike muda muafaka kwenye la tukio?
   
 9. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #9
  Aug 1, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  .

  Walifikiri ni matukio ya MBAGALA hivyo walikuwa wanasubiri MP waje kwanza.....joke
   
 10. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #10
  Aug 1, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hivi hawa majambazi wameyapata wapi magom,u yale, isije ikawa yalipatikana Mbagala
   
 11. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #11
  Aug 2, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mwenyezi Mungu anawalani na zaidi anawaonyesha ni wapi panahitajika kuwepo kwa askari kuliko Pemba ,halafu mi nawashangaa sana hawa walinzi wanaowekwa kwenye mabenki utamkuta mlinzi analinda na gobore ,ei jamani ndio nilimuona pale TRA Temeke Benki ipo kando ya ofisi hiyo ya TRA ,kule tra kama hela ni nyingi wanakwambia ukalipe hapo benki na urudi na risiti ,nilipoenda benki nikaona yule mlinzi kachoka ile mbaya ,nilivyohisi hata ile bunduki aliyoishika anaiona nzito ,yaani kidogo tu ningemvaa na kuchukua changu hapo benki ila ile bunduki aliyokamata sikuiamini kwani nayo ilikuwa ni zile zilizotumika vita kuu ya kwanza.

  Jambo jingine pale Temeke kwenye hii benki iliyoibiwa nilishawahi kwenda kama mala tatu kufanya utafiti wangu na pia kutoa hela ,kile kibanda cha ulinzi utafikiria ni sehemu ya kulindia mpunga tena imetengwa kabisa na benki eti walinzi ndio humo wanakaa ,nafikiri wamekijenga kwa maboxi tu hakina kinga yeyote ya kuweza kupambana kama kutatokea uvamizi ,tena kwa nionavyo hao jamaa kumi na tano ni wengi sana kuvamia pale ,yaani makomandoo watatu tu walioshiba maziwa ya mama yao wanaweza kabisa kuiteka benki na kuchukua wanachokitaka tena bila ya kuua mtu hata mmoja.

  Ikiwa kuna majambazi ambao wamo humu JF nawaomba wazidishe ustadi wa ujambazi kwa kuweka rekodi za kuiba bila ya kuua au kujeruhu mtu ,na huu ndio wizi stadi unaofanyika siku hizi huko nchi za nje ,hivyo wangejaribu kusoma kwa wenzao ambao wanaiba kwa style ya cinema ,hauliwi mtu ,hakwaruzi mtu ,watu wanavamia sehemu kubwa tu tena zenye ulinzi wa aina yake zikiwep[o kamera na sensor ,hivyo mambo ya kuiba mamilioni na kuuwa huwa hayazawadiwi zaidi ya kusema nchi imevamiwa maana kwa wizi uliotokea hapo Temeke inakuwa kama ulinzi wa nchi umekuwa under estimated na hivyo ukipima hali hiyo ya watu kumi na tano na njia zilizopo kama kweli akina Manumbu wamejipanga kuilinda nchi hii au mkoa huu na hujuma za aina hii basi majambazi hao hawawahi kutoka nje ya Temeke.

  Polisi hawa akina Manumbu na Kovu wote ni wateja wa ujambazi maana kwa upande wangu kule kwa wao kujigamba na kutoa makelele kuwa siku za majambazi zinaisabika hakunifanyi nione kuwa maneno yao ni kweli na hayana uzezeta ndani yake.

  Polisi wa kweli huwa wanafanya mipango yao kiaina na wanajua ni namna gani wanaweza kuufunga mji within a minute ,so baada ya kusikika milio ya risasi wangeweza kuwasiliana mara moja na kujua wapi pa kufunga njia za kuingilia na kutoka Temeke badala ya wao wote na vingunge wao kujikusanya lilipotokea tukio ,huo ni woga na kujificha ,hivi jamani mnaenda kwenye tukio wakati watu wanaondoka ? SI mtapishana nao njiani huku wanawacheka ?

  Walioouonyesha viongozi hawa wa ulinzi ni uzembe wa mwisho kabisa ,hili halina ubishi kwa maana walijua kuwa walihitajiwa kuziba njia kuu za kuingilia na kutokea Temeke ndio pale mlipowasikia kuwa asikari wetu wanajua kujipanga sijui helikopta inawafuata ,huo ndio ukweli ambao walitakiwa wakubwa na wadoge waizingire Temeke kila pembe mbali kabisa na tukio ili kuidhibiti mianya ya kutokea.

  Namaanisha pale baada ya kusikia milio na kuonyesha kuwa si ya kawaida wao badala ya kukimbilia kwenye tukio ilikuwa wajipange nje ya Temeke na aidha kuzuia magari yalioko kwenye mipaka ya kuingilia na kutokea Temeke ili kuwapa ugumu wa majambazi ambayo yapo mbioni kutoka nje ya Temeke ,hivyo kama kweli walikuwa wanawafuata kwa helikopta basi majambazi hao wasingetimiza hata kilomita mbili. na gari zilizotumika nazo zingeweza kubakia humo humo ndani ya Temeke labda iwe majambazi wamewekeza gari za kubadilisha na kwa kuwa njia zimefungwa in no time wangeonekana tu magari yalio kwenye harakati.

  Wamesoma lakini hawakufahamu ,zidini kupeleka majeshi na mapolisi Pemba na Mwenyezi Mungu atazidi kuwalaani na kuwafelisha katika kila harakati zenu na juhudi zenu ziwe hazizai matunda yeyote yale zaidi ya hasara ,mwenye kudhulumu hazidishi zaidi ya hasara ,askari hao wamevunjwa miguu ,kumbe nanyi mnaumia ?
   
 12. isambe

  isambe JF-Expert Member

  #12
  Aug 2, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 2,053
  Likes Received: 881
  Trophy Points: 280
  Utakuta Polisi kabeba SMG katega kwenye traffik lights,anakagua BIMA kwenye magari.Kazi ipo!!!!
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Aug 2, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,774
  Likes Received: 83,114
  Trophy Points: 280

  Ahsante sana, nilishangaa sana jamaa alipotoa kauli ya "Mnirudishie mabilioni yangu." Kikwete mabilioni haya ni ya kwako au ya walipa kodi wa Tanzania!!!!
   
 14. K

  Kachero JF-Expert Member

  #14
  Aug 3, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa mara nyingine tena jeshi la polisi limeonyesha kutokuwa makini na matukio ya ujambazi yanayotokea katika sehemu mbali mbali za Tanzania.Mimi baada ya kusikia tukio hilo na kuanza kulifuatilia ninatia mashaka uwezo wa Jeshi la Polisi kukabiliana na matukio ya ujambazi.

  Kwanza tukio lenyewe limefanyika kwa muda usiopungua dakika 10 ndipo baadae majambazi yakachukua hela na kutokomea.Polisi wamefika eneo la tukio nusu saa baada ya tukio kutokea.Kwa wale wenyeji wa maeneo tukio lilipotokea wanasema kituo cha polisi hakiko mbali na Benki hiyo ya NMB.Swali langu dakika 20 zote baada ya tukio kutokea polisi walikuwa wapi.

  Hii inatia wasiwasi kweli kweli isije ikawa kama kipindi cha Mahita mabenki yalikuwa yanaibiwa mchana kweupe na baada ya ujambazi kufanyika polisi wanajitokeza nusu saa baadaye wakiwa na magari lukuki na vifaa vya kufa mtu.Swali ni kwamba kama polisi wa doria wapo na wanavifaa vya kutosha, wakati matukio yanatokea wanakuwa wapi?au wanashirikiana na majambazi halafu wanazuga wananchi kuwa wanawalinda wao na mali zao.

  Waziri wa Mambo ya Ndani Masha amesema kweli polisi ni wake na wanawalinda wao sio wananchi walipa kodi,kazi tunayo Tanzania tutaendelea kudanganywa na kuibiwa mpaka tutakapo amka,na kuwawajibisha wote wanaohusika na hujuma hizi.
   
Loading...