Kauli Potofu za viongozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli Potofu za viongozi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bowbow, Jan 11, 2008.

 1. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hongereni kwa jitihada waja JF

  Nimetaka kuleta hii mada ya kauli potofu za viongozi waandamizi na jinsi walivyoudanganya Umma na hatimaye kuumbuliwa na ukweli.

  Ningeomba tuweke kauli zote(nukuu halisi ya kiongozi) zenye Utaka kuanzia Sakata za Buzwagi, BoT, Balali,n.k

  Unamtaja kwa jina unaquote kauli yake(nukuu halisi)na jinsi alivyoumbuliwa. lengo ni kufikisha ujumbe kwa wananchi wengi zaidi kwa kuonesha jinsi viongozi wetu wanavyojitahidi kutudanganya. Naamini viombo vingi vya habari vinachukua habari hapaJF tutakuwa tumewarahisishia kazi.

  Karibuni
   
 2. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Naanza na Samweli Sitta

  "Kuanzia sasa, nitakuwa makini sana kwa siku za usoni kuhusu taarifa za intaneti maana zinatuvuruga"

  Aliyasema hayo bungeni tarehe 2007-06-30 muda mfupi baada ya Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA-Kigoma Kaskazini) kuzungumzia tuhuma za ubadhirifu wa fedha Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

  Sasa sio taarifa za internet tena Sitta aambiwe aombe radhi wabunge na Umaa kwa kutoa matamshi yenye utata
   
 3. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Asante Bow,
  Ila hapo nahisi umekosea kidogo nukuu, aliye ongea ni Dr.Slaa kama nakumbuka vyema.,
   
 4. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Akiongea D. Balali (aliyekuwa gavana wa BOT)na waandishi wa habari DSM
  ''Tuhuma zote ni za uzushi, hao wanaona wivu kwa vile sikuwapitishia mikopo yao''
   
 5. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2008
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Rwabugiri,

  Nimecheka kweli -haya ndo aliyosema Dr. Balali? ukirelate na aliyosema JK jana na report ya wakaguzi- inachekesha mno!
   
 6. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2008
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  JK akiongea na Waumini wa Kilutheri, wakati wa kusimikwa kwa askofu Alex Malasusa,
  "Hoja ya mahakama ya kadhi haikuanzishwa na sisiemu, ilianzishwa na Mrema akiwa mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi"
  Wahojaji wakamngæ'ang'ania Kikwete kwamba, "Mbona iko katika ilani ya sisiemu"? Kama sio yenu mliiweka ya nini?
   
 7. M

  Mr EWA JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2008
  Joined: Mar 15, 2007
  Messages: 332
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  1.Sam sitta
  Akiongoe ktk kipindi maalumu cha TV, alisema akionyesha makabrasha aliyosema ya Dr. Slaa kuwa nikiwa nasoma haya makabrasha ili nijiridhishe kabla ya kuruhusu hoja ya Slaa ijadiliwe bungeni nimegundua maelezo mengi ni yakubuni na hayana ukweli wowote na nimeviagiza vyombo vya sheria viyafanyie kazi kwani huu ni uongo na ni pollice case.

  2.Mhe Mzindakaya alisema ktk bunge kuwa watu wengine wanazusha tu mambo yao ya uwongo na pale BOT hakuna tatizo lolote na huu ni uzushi kutoka kwenye mitandao.

  .Hitimisho je viongozi hao bado wanaona habari za Bot zilikuwa ni uzushi? na hapa naomba vyombo vya habari vifanye kazi ya kuwahoji viongozi wote waliosema ni habari za kubuni ili watoe maoni yao tena na hili litakuwa fundisho kwa wabunge kutorukia hoja ambazo hawana uhakika nazo na pia yajengwe mazingira yakuwawezesha ama kuhojiwa hata na vyombo vya habari ni kwanini walilidanganya bunge huku wakijua kuwa kusema uwongo ni kosa na hili litakuwa somo zuri kwao na kuwakumbusha ni mambo gani yaliyowapeleka bungeni. na pia ombi kwa Dr Slaa,zitto,Hamad Rashidi na wengine wanaoweza kuhoji wamhoji Spika ktk mjadala wa Bot kuna idadi ya wabunge waliolidanganya bunge ni hatua gani wanastahili kuchukuliwa ili iwe mwisho na mwanzo mzuri wa kupunguza ama kumaliza itikadi za kisiasa pale Bungeni.
   
 8. Mtaalam

  Mtaalam JF-Expert Member

  #8
  Jan 11, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 1,278
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  ninachojiuliza mie kwanini huyo spika na hao waliokuwa wanatetea kwa nguvu zoote kuwa hamna tatizo lolote BOT kwanini wasijiuzulu??au waandishi wetu ndipo wangetafuta chance ya kuwahoji upya watu kama kina sitta tuone watavyojingata meno if not ndimi zao..mikubwa mizimaaaa haina hata aibu...!!
  mijitu mizima ovyooooo
   
 9. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #9
  Jan 23, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0


  Hayo ni baadhi ya maneno ya "mshi miwa" Balali
   
 10. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Balali alisema hii?
   
 11. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #11
  Jan 23, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Sikia hii na majibu yake

  Naye Mkapa akajibu,
  Mzee huyu alionekana Dodoma kwenye maswala ya chama sisiem Je amestaafu siasa gani?


  Ushupuvu wake ni upi? wa kujenga mafisadi?

  Umadhubuti upi na aliwatumikia wananchi wapi?
   
Loading...