demigod
JF-Expert Member
- Jan 2, 2015
- 8,223
- 15,075
Kwa utafiti wangu wa kina nilioufanya inaonekana mashabiki wengi hawakupenda kauli mbiu yao mpya kuelekea mechi yao dhidi ya Al Ahly.
Wengi wao wameonekana kuwa na hofu kubwa sana ya matokeo dhidi ya wageni hao kiasi kwamba kauli mbiu ikashindwa kuinua hamasa ya ushindi. Wapo wengi wanao amini kuwa kauli mbiu isiyo na uhalisia umepelekea upweke wa hamasa miongoni mwa mashabiki wa timu hiyo.
Pia, walio wengi wanaamini kauli mbiu hiyo huenda ikawasaidia kupata sare dhidi ya wababe hao wa bara la Afrika, lakini uhalisia ni kuwa ni vigumu mno kupata sare dhidi yao ukizingatia walipumzisha wachezaji wengi dhidi ya mechi yao na Al Mereikh.
Je, ni kwa kiasi gani unadhani hizi kauli mbiu za simba zina uhalisia na uwezo wao wa kuzalisha matokeo dhidi ya vigogo vilivyopo kwenye kundi lake?