KAULI MBIU YA"HAPA KAZI TU"SASA NI KEJELI MTAANI KWA WANA CCM NA WALE BENDERA FATA UPEPO

Afixa0

JF-Expert Member
Jun 16, 2015
464
485
Kipindi cha uchaguzi hii kauli mbiu haikupewa nafasi sana kwa Watanzania wengi maana neno " MABADILIKO" iliteka nchi kila kona.
=Baada ya uchaguzi, Kauli mbiu ya hapa kazi tu ikaanza kutumika kwa kasi kubwa sana kwenye taasisi za serikali na binafsi. Ikawa ni msemo wa watu wengi sana hadi wanamichezo, bodaboda, wakulima nk. walipokuwa wanafanya shughuli zao walikuwa wakiitumia hiyo kauli kama kibwagizo cha kuonesha Ujembe flani hivi au kujituma kwa umahiri.
=Kwenye vyombo vya habari ikawa ni kauli ambayo kila baada ya dakika kadhaa hasa radioni na Tv lazima uisikie ikitamkwa na viongozi wa kiserikali, watangazaji au wale wanaojiita washikadau pamoja na wananchi. Tena baadhi ya vyombo vya habari ilifikia hatua wakawa na vipindi mahususi vilivyotengwa kwa ajili ya kusifia hapa kazi tu. Magazeti ya Tanzania nayo kwa kuongoza duniani kwa kuandika uwongo, walikuwa wanaandika maneno mengiiii watakayojisikia lakini lazima yawe na maana ya kusifia hapa kazi tu.
=Huku mtaani watu wa vyama vingine wakaonekana ni wanyongeee hawana la kusema la kusema kabisa maana HAPA KAZI TU ndio iliyokuwa wimbo wa taifa. Wanachama wa CCM na wale bendera fata upepo flani flani wakaanza kusema kwamba "mwaka huu sijui upinzani watakuwa na ajenda gani" maana walikuwa wanadai kila kitu kiko sawa, nchi inarekebishwa vizuri, maisha yatakuwa nafuu nk. Hayo yote yalitokana na kauli za viongozi mfano; kuna waziri fulani hadi leo bado analazimisha kwamba "oooooh wananchi wametuelewa, wanatukubali na wanatuunga mkono". Hapa kazi tu ikanogeshwa kwa koras iliyotiwa kila aina ya nakshi maarufu kama: Tumbua tumbua,ziara za kushtukiza, usafi nk.
=Yaani kwa muda mfupi Watanzania wengi walichezeshewa movi hadi wakasahaulishwa kwamba nchi hii ina matatizo tena makubwa kiasi kwamba kuna wengine walisahau hata mlo mmoja ni shida kwao. Watu wengi wakabaki wakiimba hapa kazi tuuuu hapa kazi tuuu wakiwa na matumaini ya kupata walau maisha bora waliyo ahidiwa kipindi kileeee,,,Ikifika saa mbili watu wanawahi kwenye Tv wakaangalie leo nani katumbuliwa, leo nani kafanya hivi na vile maana matukio ya kuchekesha na ya kusisimua yalikuwa mengi kwenye hiyo filamu ya hapa kazi tu. Watu waliopewa jina la "Wanyonge" wakawa wanaimba na kurudia ubeti wa hapa kazi tu kwa lengo tu la kutaka matajiri wafirisiwe ili walingane nao. Wimbo ukaimbwaaaa weee hadi sauti zikakauka, wimbo ukaisha utamu na kuanza kuwa chungu. Wimbo ulianza kuwa mchungu kwa waleee mabwana wakubwa wa idara mbali mbali, wimbo ukawa mchungu zaidi ya shubiri kwa wanyonge.
=Kilichofata ni wimbo kubadilika kuwa kejeli kwa wale waimbaji, wanaovaa sare za ccm, wenye hali ngumu kimaisha, omba omba, wakulima, wafanya biashara, wagonjwa mahosptalini, mama ntilie, waalimu, watoto wa mtaani nk. Wale wote waliojitenga na kujivisha taji la wanyonge wakabaki bila hata mate ya kumeza.
=Kilichosababisha huu wimbo wa hapa kazi tu uwe mchungu ni kwa sababu; Tunayoyaona yakifanywa na viongozi, tunayoyasikia yakisemwa nk yanaishia huko huko bila utekelezaji. Ikafikia hatua myonge aliyekosa walau chakula cha nusu siku, aliyesubiria atatetewa akawa ananyongwa nyongwa na kunyonywa kila kona.
=TRA nao wakanogesha wimbo wa hapa kazi tu kwa kutoa takwimu nzuri za ukusanyaji wa kodi lakini hali ikazidi kuwa mbaya zaidi.Maafidhina wa CCM wakawaaminisha Bendera fata upepo kwamba" tusubirini bajeni ya trioni 29" nayo ikawa ni chungu hadi inakata koromeo.
Kilichopoteza wimbo wa hapa kazi tu kwa kasi kubwa ni suala la BUNGE LIVE, SUKARI, LUGUMI,BAJETI, chumvi nyingi kuhusu khali ya uchumi nk. Hadi sasa huku mtaani ukienda dukani kununua bidhaa ukaambiwa bei imepanda ukiuliza sababu ni nini au tatizo ni nini, jibu ni " Hapa kazi tuu" au "serikali yenu",,,,,,hosptalini ukienda ukauliza huduma au dawa kama hamna watakujibu hapa kazi tuu,,,, watoto wa mtaani na ombaomba wanapoomba pesa mtaani wanajibiwa "hapa kazi tu" tena kwa hawa Wananchi wameenda zaidi wanawajibu kamwombeni...... maana inaonekana kipindi cha kampeni huwa wanasombwa kwenda kujaza uwanja huku wamevaa T-sheti za ccm na uchaguzi ukiisha hamna kitu, wanatupwa kama pampas jalalani.,,,,,,,, Umeme/ maji yakikatika majibu mtaani ni hapa kazi tuu,,, Wanafunzi wakikosa Bum huko vyuoni jibu ni Hp kz tu. Kwahiyo hapa kazi tuu sasa hivi inaendana na vitu vibaya tu,ukosefu wa kitu flani, maumivu nk
=Kwa ujumla kwa sasa neno hili limekuwa chungu kwenye midomo ya wana CCM na wale Bendera fata upepo. Hii ndio maana baada ya kuona hapa kazi tuu haina umuhimu tena viongozi wakawa wajanja mapemaaa wakabaki na misemo ifuatayo: Hii ni serikali ya viwanda, mara serikali ya mwendo kasi, wengine wana nogesha kwa kusema hii ni serikali ya madawati,tumbua majipu nk.
=Tunajua maisha yatarahisihwa 2018-19 ili kuwasahaulisha Bendera fata upepo

#CCM INAWANYONGA WANYONGE.
Na hii ndio hashtag ninayowaomba Watanzania waitumie kwa sasa dhidi ya CCM kwa wanayozidi kuyafanya dhidi ya wanyonge
 
MBONA UNAMUONDOA MWENZAKO KITANZI JICHONI WAKATI UNA BORITI JICHONI?ONDOA KWANZA BORIT JICHONI KWAKO NDO UONDOE KITANZI CHA MWENZAKO.MBONA KAULI MBIU YA PEOPLEZ POWER YA WATU FLANI NA BENDERA MFUATA UPEPO HAUJAISEMA AMBAYO IMEKUFA KIFO CHA MENDE UJAISEMA?HAPA KAZI NDO HABARI ZA MJINI NA VIJIJIJN ACHA KUROPOKAROPOKA
 
Mada za ajabu ajabu kila kukicha. Kwani unaishi wapi wewe? Tuelekeze mtaani kwako tuje tuone.
 
MBONA UNAMUONDOA MWENZAKO KITANZI JICHONI WAKATI UNA BORITI JICHONI?ONDOA KWANZA BORIT JICHONI KWAKO NDO UONDOE KITANZI CHA MWENZAKO.MBONA KAULI MBIU YA PEOPLEZ POWER YA WATU FLANI NA BENDERA MFUATA UPEPO HAUJAISEMA AMBAYO IMEKUFA KIFO CHA MENDE UJAISEMA?HAPA KAZI NDO HABARI ZA MJINI NA VIJIJIJN ACHA KUROPOKAROPOKA
Jibu hoja zake acha kupaniki,kwani kasema uongo?
 
Kipindi cha uchaguzi hii kauli mbiu haikupewa nafasi sana kwa Watanzania wengi maana neno " MABADILIKO" iliteka nchi kila kona.
=Baada ya uchaguzi, Kauli mbiu ya hapa kazi tu ikaanza kutumika kwa kasi kubwa sana kwenye taasisi za serikali na binafsi. Ikawa ni msemo wa watu wengi sana hadi wanamichezo, bodaboda, wakulima nk. walipokuwa wanafanya shughuli zao walikuwa wakiitumia hiyo kauli kama kibwagizo cha kuonesha Ujembe flani hivi au kujituma kwa umahiri.
=Kwenye vyombo vya habari ikawa ni kauli ambayo kila baada ya dakika kadhaa hasa radioni na Tv lazima uisikie ikitamkwa na viongozi wa kiserikali, watangazaji au wale wanaojiita washikadau pamoja na wananchi. Tena baadhi ya vyombo vya habari ilifikia hatua wakawa na vipindi mahususi vilivyotengwa kwa ajili ya kusifia hapa kazi tu. Magazeti ya Tanzania nayo kwa kuongoza duniani kwa kuandika uwongo, walikuwa wanaandika maneno mengiiii watakayojisikia lakini lazima yawe na maana ya kusifia hapa kazi tu.
=Huku mtaani watu wa vyama vingine wakaonekana ni wanyongeee hawana la kusema la kusema kabisa maana HAPA KAZI TU ndio iliyokuwa wimbo wa taifa. Wanachama wa CCM na wale bendera fata upepo flani flani wakaanza kusema kwamba "mwaka huu sijui upinzani watakuwa na ajenda gani" maana walikuwa wanadai kila kitu kiko sawa, nchi inarekebishwa vizuri, maisha yatakuwa nafuu nk. Hayo yote yalitokana na kauli za viongozi mfano; kuna waziri fulani hadi leo bado analazimisha kwamba "oooooh wananchi wametuelewa, wanatukubali na wanatuunga mkono". Hapa kazi tu ikanogeshwa kwa koras iliyotiwa kila aina ya nakshi maarufu kama: Tumbua tumbua,ziara za kushtukiza, usafi nk.
=Yaani kwa muda mfupi Watanzania wengi walichezeshewa movi hadi wakasahaulishwa kwamba nchi hii ina matatizo tena makubwa kiasi kwamba kuna wengine walisahau hata mlo mmoja ni shida kwao. Watu wengi wakabaki wakiimba hapa kazi tuuuu hapa kazi tuuu wakiwa na matumaini ya kupata walau maisha bora waliyo ahidiwa kipindi kileeee,,,Ikifika saa mbili watu wanawahi kwenye Tv wakaangalie leo nani katumbuliwa, leo nani kafanya hivi na vile maana matukio ya kuchekesha na ya kusisimua yalikuwa mengi kwenye hiyo filamu ya hapa kazi tu. Watu waliopewa jina la "Wanyonge" wakawa wanaimba na kurudia ubeti wa hapa kazi tu kwa lengo tu la kutaka matajiri wafirisiwe ili walingane nao. Wimbo ukaimbwaaaa weee hadi sauti zikakauka, wimbo ukaisha utamu na kuanza kuwa chungu. Wimbo ulianza kuwa mchungu kwa waleee mabwana wakubwa wa idara mbali mbali, wimbo ukawa mchungu zaidi ya shubiri kwa wanyonge.
=Kilichofata ni wimbo kubadilika kuwa kejeli kwa wale waimbaji, wanaovaa sare za ccm, wenye hali ngumu kimaisha, omba omba, wakulima, wafanya biashara, wagonjwa mahosptalini, mama ntilie, waalimu, watoto wa mtaani nk. Wale wote waliojitenga na kujivisha taji la wanyonge wakabaki bila hata mate ya kumeza.
=Kilichosababisha huu wimbo wa hapa kazi tu uwe mchungu ni kwa sababu; Tunayoyaona yakifanywa na viongozi, tunayoyasikia yakisemwa nk yanaishia huko huko bila utekelezaji. Ikafikia hatua myonge aliyekosa walau chakula cha nusu siku, aliyesubiria atatetewa akawa ananyongwa nyongwa na kunyonywa kila kona.
=TRA nao wakanogesha wimbo wa hapa kazi tu kwa kutoa takwimu nzuri za ukusanyaji wa kodi lakini hali ikazidi kuwa mbaya zaidi.Maafidhina wa CCM wakawaaminisha Bendera fata upepo kwamba" tusubirini bajeni ya trioni 29" nayo ikawa ni chungu hadi inakata koromeo.
Kilichopoteza wimbo wa hapa kazi tu kwa kasi kubwa ni suala la BUNGE LIVE, SUKARI, LUGUMI,BAJETI, chumvi nyingi kuhusu khali ya uchumi nk. Hadi sasa huku mtaani ukienda dukani kununua bidhaa ukaambiwa bei imepanda ukiuliza sababu ni nini au tatizo ni nini, jibu ni " Hapa kazi tuu" au "serikali yenu",,,,,,hosptalini ukienda ukauliza huduma au dawa kama hamna watakujibu hapa kazi tuu,,,, watoto wa mtaani na ombaomba wanapoomba pesa mtaani wanajibiwa "hapa kazi tu" tena kwa hawa Wananchi wameenda zaidi wanawajibu kamwombeni...... maana inaonekana kipindi cha kampeni huwa wanasombwa kwenda kujaza uwanja huku wamevaa T-sheti za ccm na uchaguzi ukiisha hamna kitu, wanatupwa kama pampas jalalani.,,,,,,,, Umeme/ maji yakikatika majibu mtaani ni hapa kazi tuu,,, Wanafunzi wakikosa Bum huko vyuoni jibu ni Hp kz tu. Kwahiyo hapa kazi tuu sasa hivi inaendana na vitu vibaya tu,ukosefu wa kitu flani, maumivu nk
=Kwa ujumla kwa sasa neno hili limekuwa chungu kwenye midomo ya wana CCM na wale Bendera fata upepo. Hii ndio maana baada ya kuona hapa kazi tuu haina umuhimu tena viongozi wakawa wajanja mapemaaa wakabaki na misemo ifuatayo: Hii ni serikali ya viwanda, mara serikali ya mwendo kasi, wengine wana nogesha kwa kusema hii ni serikali ya madawati,tumbua majipu nk.
=Tunajua maisha yatarahisihwa 2018-19 ili kuwasahaulisha Bendera fata upepo

#CCM INAWANYONGA WANYONGE.
Na hii ndio hashtag ninayowaomba Watanzania waitumie kwa sasa dhidi ya CCM kwa wanayozidi kuyafanya dhidi ya wanyonge
Labda mnyonge ni wewe,ila sisi wanachama wa chama cha mapinduzi tunatekeleza kauli mbiu ya HAPA KAZI Tu kwa vitendo,kwa kujenga viwanda vyetu wenyewe na sio kubaki watumwa kama nyinyi# HAPA KAZI TU.
 
Back
Top Bottom