Kauli mbiu ya CHADEMA nguvu ya Umma na wabunge 23

weka kwanza hapa jamvini mgogoro kati ya Nape na Millya umefikia wapi.

Mimi sio CCM mimi ni Independent Thinker, sio mtumwa wa chama cha siasa..

Kama unataka habari za Nape muanzishie thread..hapa tunajadili nguvu ya umma ya CDM
 
Naomba mwana CDM yoteyote mwenye data za ushindi wa urais wa CDM tuwekeeni tujadili..

Tujue Dr. Slaa alipata kura ngapi za urais

Mimi nilidhani una details za kutosha lakini kumbe hata hesabu rahisi hujui.

Tusichanganye hesabu za urais na idadi ya wabunge, kama zina uzito mbona Jk alipata 61% lakini bungeni wako zaidi ya 61%?

With our election systems, Mathematically it is possible for someone to get roughly 50.1 % of all the presidential votes and yet secure all the seats in the parliament. WINNER TAKES ALL.

Unapongelea swala la wabunge usichanganye na urais. Imagine uchaguzi wa Igunga kama ingekuwa urais, Kafumu angekuwa ameshinda. Lakini nyuma ya Kashindye kuna zaidi ya 40% ya wananchi. You can not just disregard that number. Asalam Aleikum.
 
Wana JF.
Mpaka sasa hivi sijajua itikadi na falsafa ya CDM. ni chama cha siasa kisicho na nadharia inayoelezeka wazi..

Ni sawa kabisa ni shirika lisilo la kiserikali NGO ninachoweza kusema viongozi wa CDM waache kupotosha wanachi kuwa CDM ni nguvu ya Umma.

CDM ina wabunge wa kuchaguliwa 23 tu kati ya wabunge 239. Bara 189 na Visiwani 50 Pemba 18 Unguja 32..

Sasa hii kauli mbiu ya CDM kuwa ni chama cha nguvu ya Umma inatoka wapi?

Tumeona maandamano ya CDM yasiokuwa na tija kwa taifa zaidi ya kugawana posho za maandamano kimsingi ni ufujaji pesa zetu wananchi ruzuku..

Viongozi wa CDM msiwapotoshe wananchi huwezi kuchukuwa nchi na wabunge 23 ukiwa na uwezo mkubwa wa kufikiri utaona huu ni umbumbu wa fikra..

Cha kushangaza zaidi CDM wanaenda mbali zaidi na kusema walishinda kiti cha urais, utashinda vipi urais na wabunge 23
Unajifanya kipofu hujui maandamano yamezaa nini hukuona maandamano yalivyoanza tu tukaona wakuu wa nchi wanaingilia bei za vyakula ikiwa ni pamoja na kushusha bei ya sukari kuzuia nafaka zisiuzwe nje kama mahindi kwa Dar mkuu wa mkoa aliamuru wafanyabiashara wa unga wa sembe wapunguze bei baada ya kuuziwa mahindi kuoka katika magala ya serikali ukiangalia trend hiyo yote hayo yametokea baada ya CDM kutangaza maandamano nchi nzima kupinga ughari wa maisha sasa ni kwa kiwango hilo ni suala jingine ile kushituka tu kwa viongozi imetokana mojakwa moja na maandamano ya CDM sasa unajifanya huoni kwakuwa umenunuliwa iliulisaliti taifa lako kuna umuhimu kujua uraia wako.
 
Naomba mwana CDM yoteyote mwenye data za ushindi wa urais wa CDM tuwekeeni tujadili..

Tujue Dr. Slaa alipata kura ngapi za urais

Kama ungekuwa umejipanga hizo data ungetakiwa kuwa nazo kabla ya kupost thread yako.

Lakini kwakuwa umekurupuka hata mambo ya msingi kabisa kwa ajili ya ku support hoja yako umeshindwa kuwa nayo. Umekuwa na haraka ya kuongeza idadi ya post tu!
 
Mimi sio CCM mimi ni Independent Thinker, sio mtumwa wa chama cha siasa..

Kama unataka habari za Nape muanzishie thread..hapa tunajadili nguvu ya umma ya CDM

nenda makao makuu ya chadema ujadiliane nao hoja zako.
 
Umesahau kuwa mlikuwa mnawaita chama cha msimu? Mbona leo mnapagawishwa?
 
WanaJF tupuuze post hii, haina mashiko. Siyo GT otherwise angekuwa ameng'amua maana ya nguvu ya umma, uwakilishi wa wabunge wa CDM na nguvu ya wabunge hao ukilinganisha na wale mia 2 wa CCM.
 
Mnapoteza muda na hawa wapumbavu ? Nilijua wanasoma mada za moto hawagusi ila wanategea kuja na pumba kama hizi .Can learn how to ignore these loosers jamani tujenge heshima ya mijadala ya maana ? Maana wao na Chadema tu ndiyo walivyo ambiwa wakiwa ukutani .
 
WanaJF tupuuze post hii, haina mashiko. Siyo GT otherwise angekuwa ameng'amua maana ya nguvu ya umma, uwakilishi wa wabunge wa CDM na nguvu ya wabunge hao ukilinganisha na wale mia 2 wa CCM.

ndio maana nimemshauri aende makao makuu ya chadema wakajadiliane.
 
Wana JF.
Mpaka sasa hivi sijajua itikadi na falsafa ya CDM. ni chama cha siasa kisicho na nadharia inayoelezeka wazi..

Ni sawa kabisa ni shirika lisilo la kiserikali NGO ninachoweza kusema viongozi wa CDM waache kupotosha wanachi kuwa CDM ni nguvu ya Umma.

CDM ina wabunge wa kuchaguliwa 23 tu kati ya wabunge 239. Bara 189 na Visiwani 50 Pemba 18 Unguja 32..

Sasa hii kauli mbiu ya CDM kuwa ni chama cha nguvu ya Umma inatoka wapi?

Tumeona maandamano ya CDM yasiokuwa na tija hao wabunge 23 wamepatikana kwa mbinde kama sio uchakakajuaji wangefika zaidi ya 100 mfano segerea, mbeya vijijini, njombe,shinyanga, kibaha mjini na kwingineko pia kumbuka uchaguzi wa 2005 cdm walikuwa na wabunge wasiozidi 10 2010 wabunge 23. 2015 wabunge zaidi ya 200
 
Mimi sio CCM mimi ni Independent Thinker, sio mtumwa wa chama cha siasa..

Kama unataka habari za Nape muanzishie thread..hapa tunajadili nguvu ya umma ya CDM
Kwa upupu huu unajiita hivyo?
 
Mkuu naomba unitajie majimbo ya uchaguzi walioshinda ubunge CDM
Hivi kwa akili yako nyembamba huwezi kujiuliza kwa nini Idadi ya Wabunge wa Viti Maalumu kwa Chadema ni kubwa kuliko wale wa kuchaguliwa??
..Jiulize tena ..ukishindwa Muulize Kiravu na yule mzee Makame aliyestaafu ..
 
Ndio maana sijataja wabunge wa kupewa wa viti maalum..hata Sabodo kakataa kuwajengea visima sababu hawana maana yoyote
 
Ndio maana sijataja wabunge wa kupewa wa viti maalum..hata Sabodo kakataa kuwajengea visima sababu hawana maana yoyote

acha uongo wewe kasema visima vijengwe kwenye majimbo 48 sawa na idadi ya wabunge wake.Alimaanisha majimbo yepi?
 
Magwanda wataanza kuporomosha matusi sasa hivi. Ukiwakamata pazuri tu, wanaanza.
 
Ritz, Mbona pumba hivyo? Hivi CCM kinakubalika zaidi ya CDM? Huhitaji ubongo mkubwa kuliko ubongo wa kuku kuona kuwa CDM imefanya makubwa ambayo sasa CCM inabidi iyakubali kwa NGUVU ya UMA. Je unafahamu kuwa mabadiliko ya katiba haikuwa sera ya CCM bali ya CDM? Sasa CCM wameivalia njuga. Mbona ni rahisi tu kuelewa mkuu? Hebu tumia ubongo wako ambao nina uhakika ni mkubwa kuliko wa kuku. Ooops mara nyingi ubongo mkubwa waweza kuwa tupu eh!

duu huyu jamaa haelewi nini nguvu ya uma,cdm ni nguvu ya uma,ccm ilikuwa nguvu ya uma,lkn wakakataa,nguvu ya uma ni uma kuwa na sauti ktk maamuzi yanayowahusu na kuhusu mustakabali wa nchi,
 
Ndio maana sijataja wabunge wa kupewa wa viti maalum..hata Sabodo kakataa kuwajengea visima sababu hawana maana yoyote

Hizo hela za Sabodo zinawauma sana,mngepewa nyie saa hizi mngeagiza magari ya kulia bata,mngekuwa mnalala bar mngechukuliana wake/waume zenu,Sabodo analitambua hilo ndio maana kawatosa saa hizi mnalialia tu kafieni mbali huko.
 
Tunapozungumzia nguvu ya umma inamaanisha umma, hatuzungumzii idadi ya kura au Wabunge.

WaTz waliopiga kura ni mil 8 tu, ambao hawakupiga kura ni mil 12 hapo umma uko kwa CCM au CDM? Kwa takwimu hizo nguvu ya umma haikuamua Rais ya Watz bali uchakachuaji na sheria mbovu na nguvu ya dola.

Kwa maana hiyo, Chama chochote cha siasa kinaweza kuitumia na kujivunia nguvu ya umma wa watu mil 12 ambao hawakupiga kura na ambao CDM wanaonekana kuuvutia na kuwatumia kutokana na kuporomoka kwa umaarufu wa CCM?
 
Back
Top Bottom