Kauli mbiu na maneno yasiyo na tija kwa wananchi isiwe ndiyo njia ya kuombea misaada kwa wahisani

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Kaulimbiu za viongozi wetu na maneno ya ulaghai yamekuwa hayana tija kwa maisha ya Mtanzania wa kawaida.Tumekuwa mabingwa wa misemo na nahau katika kufanikisha staili zetu za uongozi bila kuyafanyia kazi yale yote tunayoyaundia kauli mbiu.Imekuja miradi mbalimbali kama vile MKURABITA na kupewa vipau mbele kiawamu lakini hakuna mafanikio yaliyomnufaisha mwananchi anaye ishi chini ya dola moja ya Kimarekani.

Leo hii kiongozi wetu mkubwa wa nchi alialikwa kwenye kikao cha G8 kuinadi sera yake na kauli mbiu ya kilimo kwanza.Alikwenda kuinadi kaul mbiu ambayo hatujaifanyia practice tangu serikali ya awamu ya nne ilipoiasisi.Ukisoma makabrasha juu ya mapinduzi haya ya kijani utaona kweli kilimo ndiyo mkombozi wetu na ndiyo sekta yenye kutoa ajira kwa asilimia zaidi ya 85% na mkombozi wa wananchi.

Kilmo hiki kimenadiwa huku jembe hili la mkono likizidi kumkandamiza na kumpindisha mgongo raia huyu aliyekata tamaa ya maisha huku hajui hatima ya soko la mazao yake.Na kama soko la mazao yake lipo basi itahakikishwa amekopwa mazao yake au kukandamizwa kwa kuuza mazao kwa bei ya kumkatisha tamaa.

Cha ajabu na kweli hata hawa wahisani wakija kufanya tafiti zao hawafiki maeneo kusudiwa ili kupata ukweli halisia na kupata changamoto zinazo mkabili mkulima huyu mdogo wa jembe la mkono.

Pia ukiangalia Mfumo wa kibenki katika nchi yetu utaona kwamba mfumo huu haumpi fursa mkulima huyu kuweza kukopa kwa kutumia ardhi yake ili aweze kujikomboa ilihali serikali ikitoa kila aina maneno na chepuo za kwamba ardhi ni dhamana inayoweza kumkomboa mkulima huyu,ilihali mkulima akinyimwa fursa hiyo kutokana na mfumo wa kibenki kutoitambua ardhi kama dhamana na rasilimali katika kufanikisha biashara katika ya benki na mteja.

Leo hii kutokana na matokeo ya mkutano wa G8 wahisani wakiongozwa na Mmarekani wamevutiwa na mpango huu wa kilimo kwanza wakiamini utaleta tija kwa wananchi ilihali kilimo kilichopewa kipau mbele hakijatengewa bajeti ya kutosha.Kuna ugumu gani unao sababisha wahisani hawa kufanyia tafiti zao Dar es salaam wakati hakuna maeneo ya kilimo kama nao si ujuha na kuacha kufika maeneo husika kwa kilimo kwa kufanya tafiti zao.

Tumejiandaaje kama nchi ili kuweza kukabiliana na changamoto hizi zilizoanzishwa na Profesa aliishikilia wizara hiyo ya kilimo ambaye fani yake ni uatafiti lakini utafiti wake ukiangukia kwenye makaratasi tu na kushindwa kutumika kivitendo.Mbona viongozi wetu wanataka kutuingiza kwenye aibu ya kuwa mabingwa wa kauli mbiu zisizo na utekelezaji.

Mapinduzi ya kijani yawe ya kweli nasi kuishia kwenye makabrasha huku wananchi wakikatishwa tamaa kwa kukosa chombo cha kuwapigania katika ukombozi wa kilimo.Wakati wa mtikisiko wa uchumi,serikali yetu iliwafidia wafanya biashara wakubwa ngazi ya viwanda kwa kuwapa stimulus package kupunguza makali ya mtikisiko wa uchumi ilihali wahusika wakuu walio sababisha viwanda hivyo kujengwa(wakulima) wakiachwa wakumbane na sunami hilo la economic crisis.

Tunaitaka serikali yetu iachane na kaulimbiu ambazo ni za kuliangamiza taifa kwani zinaishia kwenye makaratasi tu huku pesa za walipa kodi zikifujwa kwa tafiti zisizo na tija kwa taifa na watu wake.
 
Back
Top Bottom