Kauli mbiu "Maadhimisho Uhuru " Imekushtua, au baridi tu?

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,429
Wakuu,

Katika pita pita zangu nimesikia kuwa kauli mbiu maadhimisho ya uhuru hapo kesho ni "Mwananchi jitokeze kuipigia kura katiba inayopendekezwa" .

Kauli mbiu hii inaashiria kuhamasisha watu wajitokeze kupiga kura amma ya ndio au hapana, lakini ninachojiuliza ni kwamba kwa nini wale wanaosubiria kura ya maoni 2016 hawastuki tu!


Hii ngoma kama imeiva wakuu! sijui kama 2015 tutatoboa kabla ya kura ya maoni. Kama hutaki kura ya maoni ipigwe ili watu waamua juu ya katiba wanayoitaka ni bora ukaanza michakato mapema maana sioni namna.
 
betlehem,hakuna Katiba mpya wala ya zamani,tupo tupo tu.Hiyo pesa iko wapi wakati serikali iko taabani kipesa?Kama wameshindwa kununua hizo BVR machine kuna kupiga kura hapo?

Pili hakuna cha maana hata ukisema hapana bado wataiba tu,na bank za nje wataweka,hakuna cha zaidi ya kuwaambia ruksa kufungua account nje,na hata ukikwapua pesa za umma ni rukhsa,kwani bila KUKWAPUA PESA ZA UMMA HAKUNA CCM
 
Wanakataza kampeni wakati wenyew wanazifanya apo apo
 
"Mwananchi jitokeze kuipigia kura katiba inayopendekezwa"
.
Kuipigia kura.........
Nipigieni kura..........Sio nipigieni kura ya hapana.


Akili ya Salva hii...akili mseto.

 
Wanakataza kampeni wakati wenyew wanazifanya apo apo

Sifikiri kama wamekampeni, maana kuwahamasisha watu kujitokeza kupiga kura hiyo si kampeni katika muktadha unaouzungumzia wewe. hiyo nafikiri ni sehemu ya wajibu.
 
Sifikiri kama wamekampeni, maana kuwahamasisha watu kujitokeza kupiga kura hiyo si kampeni katika muktadha unaouzungumzia wewe. hiyo nafikiri ni sehemu ya wajibu.
Michadema kwani inajua nini, yenyewe kazi kuforce tu.
 
Back
Top Bottom