Utopologist
JF-Expert Member
- Feb 17, 2021
- 987
- 2,487
“Mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati yetu Simba na Al Ahly kutoka nchini Misri itapigwa saa 10:00 jioni siku ya Jumanne Februari 23, 2021. Ni mechi kubwa sana kwa Simba, Tanzania na Afrika Mashariki.”- Haji Manara
.
🖋️ “Mabingwa wa Afrika ambao wametoka kushiriki ubingwa wa dunia wamefanikiwa kushika nafasi ya tatu watakuwa nchini kuwakabili mabingwa mara nyingi zaidi wa Afrika Mashariki. Rekodi hizo zitaufanya mchezo kuwa wa kipekee.”- Haji Manara
.
🖋️ “Mara ya mwisho tulikutana hapa Dar tukawafunga goli 1-0 kwenye mechi tuliyosema YES WE CAN na tukaweza. Al Ahly mara zote tukicheza Tanzania tunawafunga.”- Haji Manara
.
🖋️ “Tunao uwezo wa kuwafunga tena, tunao uwezo wa kushinda mechi hiyo. Dhamira hiyo ipo kwa kila Mwanasimba kuanzia wachezaji, benchi la ufundi, viongozi, wanachama na mashabiki wote.”- Haji Manara
.
🖋️ “Al Ahly sio timu nyepesi. Tunaposema tunaweza kuwafunga tunajua ukubwa wao, lakini Simba hupenda mechi kubwa kama hizi.”- Haji Manara
.
🖋️“Tumejiandaa kiakili na tunakwenda kwenye mchezo huu hakuna jambo lingine ila ushindi ili kukaribia lengo letu la nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.”- Haji Manara
.
🖋️ “Mechi ya mwisho tuliita WAR IN DAR, mechi ya jasho na damu ndani ya dakika 90 na sasa tunasema TOTAL WAR : POINT OF NO RETURN hii sasa ni vita kamili ya ndani ya uwanja.”- Haji Manara.
.
🖋️“Malengo yetu ni makubwa, tunataka kuleta heshima kwa Afrika Mashariki. Tunawakilisha zaidi ya watu 150 milioni, wote hao wanategemea timu moja Simba SC. Tunaenda kutetea Simba, Tanzania na Afrika Mashariki yote.”- Haji Manara. #NguvuMoja
.
🖋️“CAF wametwambia wanaruhusu watu 30,000 pekee. Kwa timu kubwa kama Simba SC na Al Ahly kiingilio cha Mzunguko - Tsh. 3,000 ukibaki nyumbani Usimba wako ni wa mashaka. 15,000 - VIP B, 30,000 - VIP A . Viingilio hivi mwisho Jumatatu usiku. Ikiingia Jumanne Mzunguko - Tsh. 5,000, VIP B - 20,000 na VIP A - Tsh. 40,000.”- Haji Manara