Kauli mbiu kama vile: Elimu ni ufunguo wa maisha, elimu ni dira na elimu ni taa ziondolewe, hazina maana tena kwa zama hizi za Magufuli

Oct 14, 2020
12
53
Kwa hali tunayokutana nayo wahitimu wa Vyuo Vikuu mtaani baada ya masomo, nachelea kusema elimu sio tena ufunguo wa maisha na naiomba selikari iziondoe rasmi hizi kauli mbiu.

Zinawapoteza sana watoto wa masikini hasa wa vijijini, wanakuwa inspired na kauli mbiu kama hizi kwenye logo za shule zao na kujikuta wakitumia muda wao mwingi na pesa nyingi za familia zao, mwisho wa siku wanarudi baada ya kuhitimu vyuo vikuu na kuzifilisi familia wakiwa mikono mitupu, no ajira, no direction nothing to do.

ELIMU SI UFUNGUO TENA WA MAISHA.
 
Zisiondoleww bali mu elimishwe kwamba elimu sio ya darasani tu, Hata mtoto anapofundishwa ale chakula kwa jasho lake ni elimu lakini kinachotuponza tunadhani kwamba elimu inaishiaga darasani
 
Zisiondoleww bali mu elimishwe kwamba elimu sio ya darasani tu, Hata mtoto anapofundishwa ale chakula kwa jasho lake ni elimu lakini kinachotuponza tunadhani kwamba elimu inaishiaga daraasani
...Sawa mkuu tumekuelewa ila...
 
Elimu si kwa ajili ya kuajiriwa tu! Elimu ni silaha inayokuwezesha kupambana na mazingira na kupata kila unachotaka kutoka katika mazingira hayo ikiwemo chakula,malazi na mengineyo.

Anza kufikiria elimu inavyoweza kukupa ujira badala ya ajira.
 
Back
Top Bottom