Kauli mbaya zinazotolewa dhidi ya wahitimu wa vyuo wasio na ajira inawakatisha tamaa wazazi wengi kulipia ada watoto wao

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,026
Graduates wanatolewa mifano mibaya sana inayoaminisha wazazi wengi wasiwalipie ada watoto wao.

Wahitimu wengi hurudi makwao na kukaa muda mrefu bila ajira kwasababu wasomi ni wengi na ajira zimezidi kupungua na wasomi wengi akili zao zimejengwa kuajirika.

Mtoto wa jirani ambaye wazazi wake wamepanga kumpeleka mtoto wao chuo wanakatishwa tamaa kwa kuambia mnapoteza pesa zenu bure oneni mtoto wa fulan kamaliza chuo ila yuko tu nyumbani yaani unakuwa kikwazo kwa wengine.
 
Ya kwanza kiswahili, historia, project planing, Rural development,PS,PA nk. Hivi na akili zako unaenda kusoma digrii ya kiswahili ili uifanyie nini.
Bora usome BBA,Account,ecomics, Oriental language,tourism, Entrepreneurship,journalism Nk unaweza kuanzisha kitu.
 
Ni kweli ila wehu zaidi ni kumlazimisha mtoto asomee Engineering au Udaktari halafu aje ku disco mwaka wa mwisho kwa sababu ya L
We ulisoma kwa kulazimishwa? Ni bora aliedisco engineering kuliko muhitimu wa art ambae hana pa kutumia knowledge yake asipoajiriwa.

Engineer atamudu mtaa na kuishi kwa kutegemea muhuri wa Authirized Engineer au ataanzisha workshop yake ya kukarabati vifaa mbali mbali, sasa wewe mwenzangu wa historia sijui utanzisha masimuluzi wapi watu wakulipe.Engineer anaweza kujiongeza hata kijiwe cha kukarabati simu.

Halafu mfumo wa kumdisco mwanafunzi mwaka was 3 na 4 in hovyo hata usiupigie chapuo.
 
Ni upotevu wa pesa kutumia ada ya million 2 bado matumizi ya ziada kwa mwaka ndani ya miaka isiyopungua mitatu haifai.

Pendekezi tutumie muda huo wa miaka isiyopungua mitatu kuwafunza ujuzi utao ingiza pesa pasipo ajira au biashara
 
Jamani tuache kuibeza Elimu Wala kuwabeza wasomi kwa kigezo cha ukosefu wa ajira ambao practically ni "transitional problem".

Wasomi ni muhimu sana katika jamii sema ni vile tu katika awamu hii ya tano wametupiliwa mbali na kiongozi wa malaika lakini awamu zote zilizopita hakuna aliyewahi kunyanyua mdomo wake kuwabeza wasomi.

By the way, Elimu ni long-term investment isipolipa leo, italipa kesho

Wewe endelea kuuza hizo nyanya zako hapo mtaani halafu tuone wewe na hao wasomi unaowabeza mtakua wapi ndani ya miaka mitano ijayo!!

Unaweza ukaanzisha biashara ikafa na usiweze kunyanyuka kiuchumi tena, unaweza kuwa na kipaji lakini nacho kinachuja kadri muda unavyozidi kwenda lakini Mimi na degree yangu ni yangu tu mpaka naingia kaburini.
 
Kibongo bongo mtu akienda chuo anaonekana yuko vzr, mm hapa mtaani na diploma yangu naonekana genius wakati nmesoma diploma in cooking
Hivi ninyi mnaposema chuo huwa mnamaanisha nini?? Kwani wewe hiyo diploma umeipatia secondary au??
Au mtu aliyesoma certificate, diploma yeye sio msomi?? Hopeless kabisa
 
Waziri wa elimu na wizara kwa ujumla inatakiwa kuboresha mitaala kuwezesha wahitimu kupata elimu ya kujiajiri kupitia elimu zao na wahitumu pia mbona elimu za ujasiliamali zinatolewa sana tubadilike
 
Graduates wanatolewa mifano mibaya sana inayoaminisha wazazi wengi wasiwalipie ada watoto wao.

Wahitimu wengi hurudi makwao na kukaa muda mrefu bila ajira kwasababu wasomi ni wengi na ajira zimezidi kupungua na wasomi wengi akili zao zimejengwa kuajirika.

Mtoto wa jirani ambaye wazazi wake wamepanga kumpeleka mtoto wao chuo wanakatishwa tamaa kwa kuambia mnapoteza pesa zenu bure oneni mtoto wa fulan kamaliza chuo ila yuko tu nyumbani yaani unakuwa kikwazo kwa wengine.
Mkuu, waambie hao jamaa ya kuwa elimu ni zaidi ya ajira na kupata pesa nyingi is just a matter of time. Kama pesa ipo peleka mtoto shule apate elimu mkuu.
 
Jamani tuache kuibeza Elimu Wala kuwabeza wasomi kwa kigezo cha ukosefu wa ajira ambao practically ni "transitional problem".
Wasomi ni muhimu sana katika jamii sema ni vile tu katika awamu hii ya tano wametupiliwa mbali na kiongozi wa malaika lakini awamu zote zilizopita hakuna aliyewahi kunyanyua mdomo wake kuwabeza wasomi.
By the way, Elimu ni long-term investment isipolipa leo, italipa kesho
Wewe endelea kuuza hizo nyanya zako hapo mtaani halafu tuone wewe na hao wasomi unaowabeza mtakua wapi ndani ya miaka mitano ijayo!!
Unaweza ukaanzisha biashara ikafa na usiweze kunyanyuka kiuchumi tena, unaweza kuwa na kipaji lakini nacho kinachuja kadri muda unavyozidi kwenda lakini Mimi na degree yangu ni yangu tu mpaka naingia kaburini.
Safi sana mkuu. Umefafanua kwa ustadi mzuri sana man.
 
Ujue waTanzania wengi hususani ambao hawakubahatika kusoma wana dharau sana wasomi kwa kuwa hawana uwezo mkubwa wa kufikiri jambo kwa mapana na kuangalia mbeleni......mawazo ya watanzania wengi ni short-term, mtu anataka kwa kuwa umesoma basi uwe Kama billgate au umiliki pesa nyingi tena ndani ya muda mfupi tu. Ndio maana hata biashara zinawashinda maana unataka uanzishe biashara Leo baada ya miezi au mwaka tayari uwe milionea!! Pathetic!
Too much expectations!!
 
60% ya watanzania ambao hawakupata fursa ya kusoma wanasumbuliwa na Inferiority Complex na kuchukia wasomi pasipo sababu za msingi.
 
Mentality ya kumpeleka mtoto chuo ili aje aajiriwe ndio inaharibu maisha ya watu. Peleka mtoto chuo kwa mentality ya apate elimu tu mengine baadae.
 
60% ya watanzania ambao hawakupata fursa ya kusoma wanasumbuliwa na Inferiority Complex na kuchukia wasomi pasipo sababu za msingi.
Huo ndo ukweli brother....kuwa msomi katika nchi masikini Kama TANZANIA ni matatizo makubwa mno!

Graduate anakutana na dharau na kejeli nyumbani kwao, mtaani na hata akibahatika kupata kibarua cha kujishikiza Viwandani au mahali popote kote huko ni mwendo wa kudharaulika tu, sishangai ndio maana graduates wenye roho nyepesi huishia kujitoa uhai maana kuendelea kuishi katika jamii isiyostaarabika na kutambua nini maana ya msomi inataka moyo wa kipekee sana kuzikabili dhihaka zao.
 
Mkuu, hivi unajua hata dereva bodaboda hajui kwamba wataalam wasomi ndio wanawezesha mikataba mizuri ya kiniashara baina ya Tanzania na nchi nyingine ndio maana tunaweza kununua hizo bodaboda pamoja na bidhaa zinazoambatana nazo kama Petrolium.

Hiyo yote haiwezekani kwa kuokota mtu yoyote yule mtaani asiye msomi na kumuweka afanye kazi EWURA au Wizara ya biashara.
 
Graduates wanatolewa mifano mibaya sana inayoaminisha wazazi wengi wasiwalipie ada watoto wao.

Wahitimu wengi hurudi makwao na kukaa muda mrefu bila ajira kwasababu wasomi ni wengi na ajira zimezidi kupungua na wasomi wengi akili zao zimejengwa kuajirika.

Mtoto wa jirani ambaye wazazi wake wamepanga kumpeleka mtoto wao chuo wanakatishwa tamaa kwa kuambia mnapoteza pesa zenu bure oneni mtoto wa fulan kamaliza chuo ila yuko tu nyumbani yaani unakuwa kikwazo kwa wengine.
kitaa ni giza
 
Ya kwanza kiswahili, historia, project planing, Rural development,PS,PA nk. Hivi na akili zako unaenda kusoma digrii ya kiswahili ili uifanyie nini.
Bora usome BBA,Account,ecomics, Oriental language,tourism, Entrepreneurship,journalism Nk unaweza kuanzisha kitu.
mkuu hiyo PS,PA umemaanisha kitu gani?
Halafu mtu aliyesoma project planning na intrepreneurship wana utofauti gani kwenye soko sasa
 
Back
Top Bottom