Kauli kama hizi za CHADEMA zinapotosha watanzania na historia ya nchi kwa ujumla | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli kama hizi za CHADEMA zinapotosha watanzania na historia ya nchi kwa ujumla

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mujumba, Apr 17, 2011.

 1. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  CHADEMA siku za karibuni kimekuwa kikijinadi kwa nguvu sana juu ya kupambana na ufisadi,kinajaribu kuwaonyesha watanzania kuwa wao ndio pekee wanaopigania dhidi ya ufisadi na wengine hawana mamlaka kabisa ya kupinga ufisadi,hata pale ccm walipotangaza kupambana na ufisadi wao walibeza hatua hiyo,sasa tuwaeleweje?? wengine wasishiriki katika kupinga ufisadi?
  kwanini historia ya nchi inapotoshwa?? kujinadi kwa CDM kwamba wao ndio walioanzisha hoja za ufisadi na kutamka hadharani majina hadharani ni kukana au kudharau juhudi za mwl NYERERE ambaye alipinga ufisadi kwa vitendo na ninaweza kusema ndio muasisi wa vita vya ufisadi hapa nchini kwahiyo hakuna anaeweza kujitapa zaidi yake,Nyerere alipinga matendo yote ya kifisadi bila kuogopa mtu,ndugu zangu cdm ufisadi si tuu kudokoa mali za umma na hata kujilimbikizia mali,angalia miradi na mabiashara makubwa yanayomilikwa na viongozi wenu,angalia mavazi wanayovaa,angalia maisha yao kiujumla,watoto wao wanakosoma,nini tofauti iliyoko kati yao na maisha ya kifisadi? wengi wao tunajua maisha yao yalikuwaje kabla hawajawa wanasiasa,lakini sasa ni kula starehe na kuwajaza wananchi hofu kuwa nchi yao inaliwa wakati na wao wamo kwenye kula hiyo national cake(ref to 90 million) wala hawakuzikataa!hii inanikumbusha novel moja inaitwa"beautyfull ones are not yet born" kuna ndege anaitwa chichidodo,huyu ndege alikuwa hapendi kinyesi lakini alikuwa anakula wale wadudu wanaotoka/ishi katika kile kinyesi. Cha msingi CDM waache unafiki kama wana nia ya dhati ya kuleta mabadiliko,basi yaanzie kwao kwanza,KAMA KWELI WANAPINGA UFISADI BASI MAISHA YAO YADHIHIRISHE HIVYO
   
 2. U

  Uswe JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  haya asante kwa malalamiko, tumekusikia
   
 3. U

  Uswe JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  angekua hai leo, angekua mwanachama wa CHADEMA
   
 4. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Chijana "unatumiwa", tena "unatumiwa" vibaya.............ni mbaya na hatari "kutumiwa" mpaka unaisha namna hiyo.........."umetumiwa" mpaka umepata mental disorder.........Ubongo umeuacha mbali sana na ukweli.................

  Nenda pitia hoja za mwenyekiti wako na vilaza wenzake utajua ni nani aliewapa jamba jamba mpaka wameamua kujivua hayo sijui ndo magamba mnaita wenyewe!
   
 5. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #5
  Apr 17, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ngoja nikasali
   
 6. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #6
  Apr 17, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,216
  Likes Received: 3,777
  Trophy Points: 280
  Karibu kija wa mafisadi naona wamekutuma nawe unatumika tena vibaya! Ninachowasifu nikuwa hawawezi kufungua blog yao wameamua shiriki ktk jf nainaonyesha wametambua kuwa jf haimilikiwi na cdm
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  Apr 17, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kashaga nashawishika kusema kuwa unataka umma wa watanzania waamini kuwa hoja ya Ufisadi ilianzishwa na CCM. Inference yako ya matamko ya Mwl Nyerere inafanya niseme hivyo. Assume, for the sake of this arguement that indeed CCM ndio wa kwanza kuleta hoja ya ufisadi. Then CCM imefanya nini au imewafanyia nini hao mafisadi? imewakamata? imewafungulia mashtka? CDM wametaja hadharani majina ya wanaowaita mafisadi. Ni nani au ni chama gani chengine kimetamka kwa majina hao wanaowatuhumu kufanya ufisadi? Tunakata a complete 360-degree hoja ili kama kuna mtu/chama kinadandia umaarufu katika hili basi tutenganishe pumba na mchale. oh nimekumbuka... baada ya siku 90 tutaona cheche kama wazee wa kujivua magamba walivyohubiri! Subira huvuta heri!
   
 8. Mufiyakicheko

  Mufiyakicheko JF-Expert Member

  #8
  Apr 17, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  sidhani kama nizambi kuishi maisha yakifahali malinyingi tunacho jaji jee? Hizomali umezipatakwanjia halali kamaviongoziwa cdm wanbiashala zao halali wanalipa kodi kunaubayagani? ningekuona unaona mbali kamaungetowa vielelezo vyaupatikanaji wamali zao ili tuwajadili mafisadi wanao anikwa kusemwa kirasiku wanatajwa fulani kaiba mf kagoda epa dowans mikataba madini rada nk jee? Cdm wapi wanaiba? nikukumbushe huwezi ukawa upo jararani ujiite musafi niunafiki ccm ndowanashikilia silikali ufisadi wote unawofanyika silikalini wao ndowakuwajibika kuiwajibisha silikali hawasubutu kufanyahayo kwasababu waondowanao husika mimi niwwanachama hai wa ccm ninachowasihi siasa nimaisha halisia ya watu cdm wanachopigania nihaki yakiramutanzania rafikiyangu inawezekana hujuwi maana ya ccm viongozi tulionao kwasasa kujiita wana ccm nizambi hawana hizosifa kuitwa wana ccm wamejaa ubinafis wameishiwa utuu wapo tayali kuuza utu wamutu iliwapate mali nahiyo simaadili ya ccm tulio wengi tunapotea kwaushabiki hatutafuti ukweli
   
 9. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #9
  Apr 17, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  unaandikwa kiswahili au lugha inayofanana na kiswahili?
   
 10. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #10
  Apr 17, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  CCM ya leo ipambane na ufisadi? Si wao ndio wa kuuenzi? nAFURAHI KUWA HATA BAADA YA KUJARIBU KUJIVUA GAMBA BADO CHADEMA YAWATESA....
   
 11. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #11
  Apr 17, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Muhimu umeelewa.....:yawn:
   
 12. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #12
  Apr 17, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kashanga wewe! Huchoki tu? Hv lini utatuletea thread uliyoandika kwa mapenzi yako??? Manake zote ulizowahi kuleta ni za kutumwa! Utatumika mpk lini???
   
 13. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #13
  Apr 17, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wenye hoja za kutumwa mnatupandisha mkari gggggrrrrrrrrhhhhhh5. Siku ukijua ukweli kifo kitakuwa karibu. Utaongelea jemadari ambaye hayupo, unataka tuamini ccm inamsubiria nyerere tena ili awatiue na kusafisha chama. Taljk of today mnamsubiri nyerere? Chadema wanafanya mambo leo wewe unaongelea historia , enzii za nyerere mafuta, chakula, maisha kwa ujunla yalikuwa ya shida kama leo, barabara ndio mnakarabati hatdi mitaani zailikuwa lami pambafu kula hela zao mafisadai ila huna hoja go away
   
 14. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #14
  Apr 17, 2011
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Wakati unailaumu Chadema kwa "kujidai ni wao pekee ndio wanaopinga ufisadi" unasahau kuwa nawe pia unajifanya NDIYE PEKEE unayeijua vizuri Chadema na kasoro zake.Badala ya kutuletea hangover zako za pombe haramu,tupe reference ya mahala walipoandika au kunukuu kuwa CHADEMA NDIO CHAMA PEKEE KINACHOPAMBANA NA UFISADI.Japo nafahamu unachoandika hakitoki akilini lakini si vibaya kukupa darasa hivyo hivyo.Chadema haihitaji sifa za wananchi kwani suala la ukombozi wa wanyonge halina madhumuni ya kusifiana au kupongezana.Wakati mafisadi na ninyi mnaojikomba kwa mafisadi mnapongezana kwa "kujivua magamba" (japo tatizo lenu si magamba bali kansa ya damu), Chadema na Watanzania halisi wanaendelea na mapambano ya kudai uhuru wa pili.1961 tulimtimua mkoloni,sasa tunapambana kuwatimua mafisadi.

  I just hope jina lako la kashanga sio corruption ya "kaubongo kachanga".Haya mambo mengine mnayorukia na kuyaanzishia topiki yanahitaji ubongo uliopevuka na kuimarishwa na taaluma plus uzalendo.Ubongo mwepesi unaoathiriwa na gongo na kukwazwa na elimu ya chini ya mwembe ndio inasababisha mshindwe kuelewa kinachoendelea ktk Tanzania yetu.Kwani mkikaa kimya mtakufa? Oh,hamwezi kukaa kimya kwa vile mnaishi kwa pay-per-JF-post.Kila utumbo unaoandika hapa unaongeza pasenti yako from mafisadi in form of vocha ya simu au chipsi mayai.Umeandika upupu huo hapo juu na sasa una hakika ya mlo wa mchana.NJAA MBAYA.
   
 15. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #15
  Apr 17, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  i always enjoy reading ur pumba,coz hakuna siku uliyoandika point zaidi ya pumba
   
 16. theophilius

  theophilius Senior Member

  #16
  Apr 17, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Japokuwa si mwana CDM nawaunga mkono kwa mambo mengi wanayosimamia, likiwemo la kupambana na ufisadi. kuhusu hoja kashanga kwamba CDM hawataki wengine wapambane na ufisadi, nafikiri huu ni ufinyu wa mawazo na uelewa kama ilivyo kwa CCm na wakuu wake. kwa hiyo unataka CCM nao wapambane na ufisadi kwa kuandamana kama CDm au kulalamika katika mikutano ndiyo waonekane na kusifiwa kuwa nao wanapambambana na ufisadi.

  Kwa nafasi waliyonayo CCM ya kushika dola, hawana hata sababu ya kutaka kuonekana wanapambana na ufisadi (ambao kiuhalisia hawapambani nao) wanachopaswa kufanya ni kuchukua hatua, kuagiza viogozi wa serkikali yake kuchukua hatua kwa vitendo vya ufisadi na wahusika wakiwemo waliomo ndani ya CCM na hatua siyo kubebelezwa kujivua uongozi katika chama kama walivyo waadaa wanachma wao majuzi, ni kuwafikisha katika vyombo vya haki watuhumiwa wote wa ufisadi, na kuhakikisha wanachukuliwa hatua za kisheria (kwani hapo outomatically watakuwa wamepoteza nafasi walizonazo za uongozi) hapo hauhitaji kuja hapa kuomba CCm nao wasifiwe kwa kupambana na ufisadi, hata kama CDM hawataona umma wa watanzania wataona!

  kwa bahati mabaya unaofikiri wanapambana na ufisadi ndani ya CCm ndiyo mafisadi nambari one, sasa iweje hata wadhaniwe tu kwamba wanapambana na ufisadi, neno ambalo iliwachukua miaka hata kulikubali kulitumia!
  Tafakari nawe kama kweli unachukia ufisadi, usiwaamini watu hao (CCM)
   
 17. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #17
  Apr 17, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Unafanana na mtu aliyepeleka ushahidi mahakamani lakini akabaki kueleza tu yale aliyoyakariri bila kujua ushahidi huo autoe katika kipengele cha hoja inayotaka ushahidi.

  Kwani kama kwanza hoja ya kupiga vita ufisadi siyo kama vile ni sawa na historia ya kuanza kwa chama fulani. Mwl. Nyerere unayemtaja ni baba wa taifa hili na anaheshimiwa na CCM na CDM. Haimaanishi kuwa CDM hawajui kuwa Nyerere ni mpinga ufisadi. hata hivyo kwamba Mwl. alikuwa mwanaCCM kupinga kwake ufisadi hakuwezi kuiokoa CCM kwa vile leo hii inapingana na mawazo ya Mwl.

  Majigambo ya wanaCCM wanaojivua magamba kwa upande mmoja ni ushahidi kuwa kilichokuwa kinasemwa na CDM kilikuwa kweli kwamba kulikuwa na ufisadi katika CCM. Tofauti ya CDM na CCM katika kupinga ufisadi moja tu, yaani CDM wanapigana vita ya kweli wakati CCM wanafanya usanii. Kama ni kweli CCM wametambu kuwa kuna baadhi yao ni mafisadi, kwanini hawajawapeleka mahakamani badala yake wanawaondoa tu kwenye CC? kuwaondoa kwenye CC kumetoa jibu gani kama mwizi aliyeiba amefungwa au amerudisha alichoiba? Mafisadi wamelibia taifa siyo CCM hivyo wananchi tunataka kujua kama wamechukuliwa hatua za kisheria na siyo za kichama. Mungu atuepushe na usanii wa CCM
   
 18. denoo49

  denoo49 JF-Expert Member

  #18
  Apr 17, 2011
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 5,647
  Likes Received: 5,241
  Trophy Points: 280
  nimi ninamashaka na uraia wake. Yapata takribani cku kadhaa zilizopita nilickia ya makambi ya wakimbizi kuvunjwa na wahucka kupewa uraia halali wa kibongo, nahisi yu miongoni mwao. Ni mwanachama Mfu.... wa Chama Cha Misukule.
   
 19. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #19
  Apr 17, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Next time try ur level best to be as objective as possible and not subjective. Wewe ndio umeleta idea ya history ktk kupambana na ufisadi sijui objet hapa ni nini hasa? Kama Nyerere alifight ufisadi at some point kisha kukawa hakuna hizo juhudi tenas I hope ur not suggesting kwamba mtu/watu wengine wasijitokeze kupambana?

  Nasema be objective kwa sababu haina mantiki kusema CCM mmekuwa mkifight ufisadi bila kuzungumzia results ya hizo efforts.

  Labda nikufahamishe tu kuwa watu wengi (sio CDM pekee) wanachoibishia CCM kuhusu ufisadi ni mikakati yao na sio CCM as individuals, usiwe personal ktk analysis zako.
   
 20. JAMHURI

  JAMHURI JF-Expert Member

  #20
  Apr 17, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 249
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Aiseeee kweli pamoja na kuwepo uhuru wa kuongea wenzetu sasa wanatusaliti yawezekama mwenzetu ni wakala wa mafisadi kutaka ajua mawazo ya wanajamii,mpeni nafasi yake msimuone kinyaa kwa alichopata kinatosha..
   
Loading...