Kauli inayomgharimu Hadji Mponda dhidi ya Madaktari

..Ni kweli anawajibika jimboni, kwani uongo?

Sasa pale kwenye ofisi za wizara ya afya anatafuta nini? Si aende Ulanga basi akawajibike kwa wapiga kura wake? Ukishakuwa waziri huwajibiki tena jimboni, unawajibika wizarani, ndio sababu hata bungeni waziri hasimami kutetea wananchi wa jimbo lake, anatetea hoja za serikali yake. Siasa ulisomea wapi weye?
Kumbe wewe na yeye wote m^^^buri tu.
 
Binafsi sina uhakika na kauli hiyo ya Mponda, aliitoa wapi, alimwambia nani, lini, na alikusudia nini? Na je Nkya naye ametamka lipi? Nadhani tungepata habari kamili za uhakika, sio umbea na udaku, hapo ndipo tunaweza kutoa maoni.
 
ni kweli mkuu nadhani kuna lililo fichika hapa. kama ni issue ya utendaji hata hospitali za serikali bila kujuana/connection na au pengine kutoa baksishi kumwona daktari ni shughuli pevu, muhimbili is the leading example. hata hiyo fast track wanayoisema muhimbili ni maumivu matupu, wajisafishe wao kwanza...

second, hii nchi inaendeshwa na taaluma moja tu? na je ni kada ngapi za watu wanaidai serikali? ni wafanyabiashara wangapi wanaidai serikali? kila mmoja aje na dai la kutaka waziri husika ajiuzulu kama vile mshahara wake ndiyo unapaswa kuwa malipo yao? kwa kufuata kauli ambazo zinaweza zisiwe za kweli au pengine waziri alijibu hivyo kutokana na mazingira na swali aliloulizwa?
 
Afadhali umetufumbua akili, huyu jamaa kama madaktari hawamhusu anaongoza kina nani?? AONDOKE TU.
 
Jamaa kweli ana bahati mbaya kama kauli hiyo ndiyo inayoua wananchi wasio na hatia. Nchi hii tushasikia kauli mbovu na za kukatisha tamaa toka kwa viongozi wengi tu hakuna haja ya kutolea mifano maana nyingi sana, sdasa hiki si cha mtoto tu?
Kuna watu wengi wamekuwa wakihoji kwa nini Waziri wa Afya ajiuzulu? Hata Waziri Mkuu, Mizengo Pinda nae alihoji swali hili wakati akizungumza na Waandishi wa habari hivi majuzi na akaenda mbali kwa kusema Waziri Mponda ni mgeni pale Wizarani na hadly ana kama mwaka mmoja ofisini. Kwa wale ambao hamjui kiini cha Madaktari kumchukia huyu Waziri napenda tu niwaambie kauli yake moja aliyoitoa wakati akihojiwa na waandishi wa habari kabla ya ule mgomo wa kwanza. Alisema hivi: Nanukuu

Mwisho wa kunukuu!
 
Hapo ndipo utakavyo ona baadhi ya wanasiasa wetu walivyowabinafsi! yeye anajali wapiga kura wake tu! sasa JK alitakiwa kuwajuwa watu kama hawa mapema ili asiwape hayo madaraka yaani kuwa waziri! OMBI: Wadau wenzangu mimi ni mwana CCM lakini ninachowaomba tuungane paoja kuhakikisha tunathubutu kukipigia kura chama kingine ili angalau tuweze kuona MBIVU NA MBICHI! Wataalamu wanasema ukitaka kujua utamu wa ngoma uingie ucheze! Nini maana ya kuwa na vyama vingi halafu hatuone manufaa yake???Natumaini kwakubadili chama viongozi ambao wanaotaka kuingia madarakani watakuwa na challengies nyingi sana, so watabadilika na kuacha kufanya kazi kwa mazoea! Hebu tuamke, hata kama wanaiba hizo kura kuna siku watashindwa kuiba sababu za upinzani zitakuwa zimezidi sana!
 
Nafikiri kama kila kada ikiamka kama madaktari nchi itasogea! Tumshinikize bosi atuletee mawaziri wawajibikaji, walimu vp nyie mawaziri wenu wanawafaa? Kama vp uwasheni na nyinyi!

Bila kumsahau mzee wa megawati naye aondoke tumechoka kukaa na giza !
 
ni kweli mkuu nadhani kuna lililo fichika hapa. kama ni issue ya utendaji hata hospitali za serikali bila kujuana/connection na au pengine kutoa baksishi kumwona daktari ni shughuli pevu, muhimbili is the leading example. hata hiyo fast track wanayoisema muhimbili ni maumivu matupu, wajisafishe wao kwanza...

second, hii nchi inaendeshwa na taaluma moja tu? na je ni kada ngapi za watu wanaidai serikali? ni wafanyabiashara wangapi wanaidai serikali? kila mmoja aje na dai la kutaka waziri husika ajiuzulu kama vile mshahara wake ndiyo unapaswa kuwa malipo yao? kwa kufuata kauli ambazo zinaweza zisiwe za kweli au pengine waziri alijibu hivyo kutokana na mazingira na swali aliloulizwa?

Unajua hata kama mawizara mengine kuna madudu lakini wakanyamaza, inategemea huyo kiongozi anaishije na wale anaowaongoza. Kwani si tuliona jairo alivyorudi ofisini kwakwe alipokelewa kama mfalme wakati huku nje watu wanamwona sio?

Inawezekana hao viongozi wa wizara nyingine ni wajanja na wanahakikisha watumishi wake wanapata stahili zao hata kama itakuwa kwa mateso kwa watanzania wengine. Aende akaongee na waziri kama Mwinyi ampe ABC za jinsi anavyoziweza wizara, ampe tu mfano wa pale ulinzi ndipo atakapoona alivyochemsha.
 
ni kweli mkuu nadhani kuna lililo fichika hapa. kama ni issue ya utendaji hata hospitali za serikali bila kujuana/connection na au pengine kutoa baksishi kumwona daktari ni shughuli pevu, muhimbili is the leading example. hata hiyo fast track wanayoisema muhimbili ni maumivu matupu, wajisafishe wao kwanza...

Kama mwananchi unatozwa rushwa na ukakaa kimya basi na weye ni kilaza, unamsubiri nani amuwajibishe huyo daktari kama si huyo mwananchi? Serikali yenu haina kitu chochote kinachotolewa bure mahospitalini sasa hivi ingawa wanasema baadhi ya huduma bure, mtu ukiambiwa ukajilipie kipimo au dawa unaona daktari anaitaka hiyo hela yako! Mwe!! Amkeni waTanzania tuachaneni na propaganda, bila kutumia actio hatufiki popote, madaktari wamethubutu na sie tuthubutu kama kweli tunaona kuna mahali kuna uzembe.
 
Acha upuuzi wewe hiyo kauli ndiyo iwe sababu hao madaktari ni makanjanja tu, huwezi kumpa Rais masharti.
Mtu mzima mwenye akili timamu hujifanyia maamuzi yake mwenyewe.
Hawezi kutumwa na kibaraka nae akatii na kuisaliti nafsi yake.

Pole sana.......kwasababu unajua unachofanya hapa niutumwa, it will haunt you for the rest of your life.
Specifically, ID ya propaganda za serikali dhidi ya madai ya madaktari.

Huu ni ukenge wa hali ya juu kabisa. .... and you know we know you, right?

Tabia za Fisi hizi. Very little diference........Fisi wakati mwingine anawinda na kujipatia fresh meat, wewe ni Mizoga mwanzo mwisho.
 
hata kauli za pinda na raisi si za watu makini na wenye busara iliyosawazika
 
huwezi kumpa rais masharti?!
yupi mwajiriwa wa mwenzie kati ya rais na wananchi?
usikurupuke mkuu!
 
Madaktari ni makanjanja tu. Sasa itakuwa mchezo kila idara ya serikali iwe inampa rais masharti huo ni upuuzi

hii nchi haina rais,kuna mtu aliyekalia kiti cha rais,na mtu huyo anaitwa jakaya khalfan mrisho kikwete(na huyu mtu hajawahi kuitimiza ile nguzo ya hijja ingawa uwezo anao..)
 
Hivi serikali inasema inashughurukia matatizo ya madaktari, wakati mtuumiwa mmoja bado yuko ofisini, haiingi aklilini.... u\yawezekana kaacha awashughurikia vinala wa mgomo kabla hajatoka, sasa Ma Dr wamestuka
 
Kuna watu wengi wamekuwa wakihoji kwa nini Waziri wa Afya ajiuzulu? Hata Waziri Mkuu, Mizengo Pinda nae alihoji swali hili wakati akizungumza na Waandishi wa habari hivi majuzi na akaenda mbali kwa kusema Waziri Mponda ni mgeni pale Wizarani na hadly ana kama mwaka mmoja ofisini. Kwa wale ambao hamjui kiini cha Madaktari kumchukia huyu Waziri napenda tu niwaambie kauli yake moja aliyoitoa wakati akihojiwa na waandishi wa habari kabla ya ule mgomo wa kwanza. Alisema hivi: Nanukuu

Mwisho wa kunukuu!

Hiki ni kielelezo cha muundo wa ubunge na uwaziri. Ni vema sasa kutenganisha ubunge na uwaziri. Mbunge ahangaike na jimbo, waziri awe kwenye wizara.
 
Kasema hivyo au umeongeza chumvi chifu!!!!!Kama kweli kauli hiyo hata ukiweka madudu yake mengine pembeni itatosha kumpeleka ulanga
 
sasa kwa nini haendi huko Ulanga, wizarani pale anafanya nini...
 
Back
Top Bottom