Kauli hizi za Mwalimu Nyerere ni za Kudumu?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
20,387
38,658
Kuna kauli za Mwalimu Julius Nyerere ambazo ni maarufu sana kwenye siasa za tanzania. Kauli hizo ni hizi zifuatazo!

Ikulu ni Mahala Patakatifu...

Bila CCM Madhubuti nchi yetu itayumba

Rais bora atatoka CCM

Jee kauli hizi zilikuwa na uhalali kwa wakati ule zinatamkwa au ni kauli za kudumu katika siasa zetu nchini Tanzania?
 
Nadhani pia inategemea na wakati maana ni yeye pia alisema ccm sio mama yake kama ingetokea imeenda kinyume na msingi yake angehama tu
 
Ni kweli kwa sasa hivi hazina maana ndani ya ccm hapawezi akatoka kiongozi mzuri,ccm ni ile ile.
 
Ya kwanza ndio kauli ya kudumu. Lakini hizo nyingine zitabadilika jinsi demokrasi inavyozidi kukuwa.
Kwa sasa zote ni muhimu.
 
Kwa hiyo mpaka sasa bado unaamini kuwa Rais Bora atatoka CCM, na bila ya CCM Madhubuti nchi yetu itayumba?
Yes. Ukiangalia idadi ya wagombea urais waliojitokeza kugombea kwa ticket ya CCM ni kubwa wakati UKAWA alijitokeza mmoja.ATC wazalendo walistruggle kupata hata mgombea urais. Hii inaonyesha jinsi upinzani ilivyokuwa na uwaba wa viongozi na demokrasia.

Upinzania wanatakiwa kujenga vyama vyao kwa kukuza demokrasia ndani ya chama na itawavuta viongozi wanzuri kujianga nao.
 
kauli hizo pamoja na nyingine nyingi zitaendelea kutamba na kuongoza siasa za tanzania kwa muda mrefu sana ujao.

watu wengi hawapendi kusikia kauli hii - zidumu fikra za m/kiti(mwl. nyerere). ukweli ni kama nilivyosema hapo juu, zitadumu.

katika uchaguzi uliopita ilidhihirika kwa chama tawala na wapinzani kuzitumia ili kupata uhalali wa wapiga kura kuwachagua.

tukubali tukatae mwl. nyerere was unique na kauli zake zitadumu.
 
Last edited:
Kauli za Rais wa awamu ya kwanza Hayati Julius Nyerere bado zina ukweli na mantiki mpaka leo hii. Ikulu ni mahali patakatifu na ni patakatifu kweli, wale wanaojaribu kuparahisisha kiasi cha wafanyabiashara kuweza kupazoea kirahisi tu wamelipia tabia yao hiyo kwa kubeba mzigo mzito wa lawama baada ya kutoka madarakani. Hiyo ni sababu rais wa sasa aliwakwepa sana wafanyabiashara wakati wa kampeni, hakutaka awe na uhusiano nao wa karibu ili baadae asishindwe kuweka utakatifu katika Ikulu ya awamu ya tano. Utakatifu wa Ikulu unaanza na ugumu au wepesi wa rais katika kuingilika na wanajamii haswa wale wafanyabiashara wakubwa ambao uzoefu wa bara letu unaonyesha kuwa hawawezi kufanya biashara safi kwa asilimia zote 100%. Bila ya CCM madhubuti nchi yetu itayumba, ni kweli kabisa Tanzania imeyumba sana baada ya CCM kushindwa kuwa na sauti mbele ya wale ambao wanachangia kuifanya Ikulu isiwe mahali patakatifu. Magufuli amelazimika kufanya kampeni akitanguliza jina lake ingawa jukwaani alipanda akiwa amevaa mavazi ya CCM!, maana yake ni kwamba chama tawala kiliyumba na yeye kama mgombea alilazimika kukwepa kujihusianisha na madudu ndani ya chama chake. Rais bora atatoka CCM, hili naona linao ukweli pia. Kati ya mgombea wa CCM na yule wa UKAWA nadhani wa CCM alitumia muda mwingi katika kudhihirisha ubora wake na uzalendo mkubwa kila alipopata nafasi ya kufanya kampeni, na hata hivi sasa bado anawatanguliza wananchi wa hali ya chini kila anapopata nafasi ya kuongea. Lakini ni CCM hiyo hiyo iliyokuwa na wagombea ambao kama wangepewa nafasi basi yule wa UKAWA angeweza kushinda. Na tukumbuke kuwa dr. Slaa alisikitishwa sana na jinsi ambavyo CDM ilishindwa kutengeneza kizazi cha wanasiasa vijana ili waweze kuzielezea vizuri sera za chama kwa wananchi walio wengi. CCM sasa hivi inavyo vizazi vya vijana kama Paul Makonda, ambao wamepikwa, na wao wanao wadogo zao ambao wanaanza kuvalishwa magandwa yenye rangi ya kijani. Kwa mtazamo wangu naona kama vile kauli zote tatu zinao uhalali wa kutumika mpaka mwa huu wa 2016.
 
Back
Top Bottom