Kauli hizi za Msibani huwa zinanikera sana.

KakaJambazi

JF-Expert Member
Jun 5, 2009
18,711
12,067
Utakuta kiongozi mkuu au mwakilishi wa taasisi flani anawaambia wafiwa na wananchi (via media) eti "naombeni muwe na moyo wa subira" subira ya nini wakati mtu kesha kufa? Mbona huwa hatupati feedback?
Subira katika lipi? Kwani nani anampango wa kuandamana na kuatarisha usalama wa nchi?

Sio misiba yote inahitaji subira labda kama kuna mauaji flani ivi yanayohitaji uchunguzi.Lakini kifo kimetokana na kusukari au BP,, subira ni ya nini mnayotutangazia? au ni kukariri tu?

Kauli nyingine ni "Mungu ame(m)wapenda zaidi ndo mana amewachukua". Inamaana wale wanaonusurika kwenye ajali mfano ile ya Five stars, Mungu anawachukia?
Walionusurika huwa wanajisikiaje wasikiapo kauli hii?
 
Ni mazoea tu ya ku copy and paste bila kuchuja mambo. Hata kwenye wasifu wa marehemu utasikia Marehemu alianza darasa la kwanza mwaka fulani! Hivi na haya ni matumizi sahihi kweli ya lugha!
 
Nadhani neno subira lina maana zaidi ya moja. Kwenye misiba linatumika kumaanisha: uvumilivu, moyo/ uwezo wa kuhimili machungu, kutokukata tamaa kwa kuondokewa na mpendwa.
 
Ndo maana wengine misibani ni ngoma na sherehe, hizo ndo faraja anazohitaji mfiwa
 
Nadhani neno subira lina maana zaidi ya moja. Kwenye misiba linatumika kumaanisha: uvumilivu, moyo/ uwezo wa kuhimili machungu, kutokukata tamaa kwa kuondokewa na mpendwa.

Ni hii ndiyo maana yake halisi. Ahsante.
Lugha inahitaji ufahamu wa mambo mengi. Mwanzisha mada, kwa siku za baadaye, jaribu kuuliza kwanza na si kutoa hukumu, nadhani umeona majibu yalivyohitimisha mada yako.
 
Utakuta kiongozi mkuu au mwakilishi wa taasisi flani anawaambia wafiwa na wananchi (via media) eti "naombeni muwe na moyo wa subira" subira ya nini wakati mtu kesha kufa? Mbona huwa hatupati feedback?
Mkuu sina uhakika kama unaelewa maana ya neno subira, laiti ungekuwa unazungumza Kiswahili, usingekuwa unakasirika kila unaposikia neno subira.
Subira katika lipi? Kwani nani anampango wa kuandamana na kuatarisha usalama wa nchi?
Subira inaitajika katika kila jambo unalolifanya.
Sio misiba yote inahitaji subira labda kama kuna mauaji flani ivi yanayohitaji uchunguzi.Lakini kifo kimetokana na kusukari au BP,, subira ni ya nini mnayotutangazia? au ni kukariri tu?
Subira inayoitajika hapa, ni kukubali kiakili kuwa msiba umetokea na kuacha kufikiria kuwa Mwenyezi Mungu amewaonea wafiwa kwa kuondokewa na kipenzi chao...!

Subira ni kuzuia nafsi isiungulike au isimahanike au isighadhibike kutokana na mitihani inayomsibu mtu kama vile vifo n.k. Vile vile tunapaswa kuwa na subira kutokana na maudhi ya watu na kuzuia nafsi, ulimi na viungo visilipize maovu anayotendewa mtu. Kusubiri kote huko ni kwa ajili ya kupata radhi za Mwenyezi Mungu.

Kauli nyingine ni "Mungu ame(m)wapenda zaidi ndo mana amewachukua". Inamaana wale wanaonusurika kwenye ajali mfano ile ya Five stars, Mungu anawachukia?
Walionusurika huwa wanajisikiaje wasikiapo kauli hii?
Hizi ni Kauli za wale wenye imani na dini, yote hii ni kuwatakia wafiwa faraja...!

Kama wewe si mwenye kuamini kuwepo kwa Mwenyezi Mungu kauli hizi zitakusumbua sana, kwani utazielewa malengo yake.
 
Mtoa mada kiswahili kinampa tabu. Ndo mana anakibananga atakavyo. Subira wakati wa majonzi ndipo mahala pake.
 
Na kwa kuongezea ni hii hapa ya mtu kaiba halafu kachomwa moto! kwenye mazishi yake eti wanasema sisi tulimpenda lakini Mungu alimpenda sana ndio maana kamchukua! tobaaa yaani uibe uchomwe moto halafu Mungu alikupenda?
 
Utakuta kiongozi mkuu au mwakilishi wa taasisi flani anawaambia wafiwa na wananchi (via media) eti "naombeni muwe na moyo wa subira" subira ya nini wakati mtu kesha kufa? Mbona huwa hatupati feedback?
Subira katika lipi? Kwani nani anampango wa kuandamana na kuatarisha usalama wa nchi?

Sio misiba yote inahitaji subira labda kama kuna mauaji flani ivi yanayohitaji uchunguzi.Lakini kifo kimetokana na kusukari au BP,, subira ni ya nini mnayotutangazia? au ni kukariri tu?

Kauli nyingine ni "Mungu ame(m)wapenda zaidi ndo mana amewachukua". Inamaana wale wanaonusurika kwenye ajali mfano ile ya Five stars, Mungu anawachukia?
Walionusurika huwa wanajisikiaje wasikiapo kauli hii?

Hawajisikii lolote zaidi ya kumshukuru Mungu kwa kuwaepushia kifo, huwa wanajihisi wenye bahati zaidi. KakaJambazi umewahi kusikia wasifu unaomlaani marehemu? hata kama alikuwa fisadi au jambazi kama wewe 'mchungaji' atasema marehemu ameacha pengo ambalo halitazibika, marehemu alikuwa na upendo, Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.... na wote wataitikia Amen. sasa unashangaa nini?
 
Mtoa mada kiswahili kinampa tabu. Ndo mana anakibananga atakavyo. Subira wakati wa majonzi ndipo mahala pake.

Kuna tofauti kubwa kati ya subira na uvumilivu, kuwa na subira ni kuahirisha jambo, na kuvumilia maana yake ni kustahimili machungu kwa muda fulani hadi yatakapokwisha. Sasa hapa wagiwa wanatakiwa kusubiri nini. wanatakiwa waambiwe wawe na moyo wa uvumilivu sio kuwa na subira, mtu kesha kufa hakuna cha kusubiri tena hapo. mtoa mada yuko sahihi.
 
utakuta kiongozi mkuu au mwakilishi wa taasisi flani anawaambia wafiwa na wananchi (via media) eti "naombeni muwe na moyo wa subira" subira ya nini wakati mtu kesha kufa? Mbona huwa hatupati feedback?
Subira katika lipi? Kwani nani anampango wa kuandamana na kuatarisha usalama wa nchi?

Sio misiba yote inahitaji subira labda kama kuna mauaji flani ivi yanayohitaji uchunguzi.lakini kifo kimetokana na kusukari au bp,, subira ni ya nini mnayotutangazia? Au ni kukariri tu?

Kauli nyingine ni "mungu ame(m)wapenda zaidi ndo mana amewachukua". Inamaana wale wanaonusurika kwenye ajali mfano ile ya five stars, mungu anawachukia?
Walionusurika huwa wanajisikiaje wasikiapo kauli hii?

hapo kwenye nyekundu hata mimi waga pananishangaza,sasa inamaana mungu akimpenda mtu zaidi anamchukua(anamuua)?
 
Back
Top Bottom