Kauli hizi si-nzuri, binafsi sizipendi....... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli hizi si-nzuri, binafsi sizipendi.......

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Domhome, Jul 23, 2011.

 1. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2011
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 1,986
  Likes Received: 1,043
  Trophy Points: 280
  Kauli hizi kwa hakika zinanikera....
  I. Wakulima kuzuiwa kuuza mazao yao eti kisa huenda kukawa na uhaba mkubwa sana wa chakula baadaye! kauli hii huwa inatolewa na viongozi katika namna ya kuonyesha Mkulima anahurumiwa!

  II. Huyu fulani (wanataja jina) anasema nini sasa? wakati yeye aliwahi kuwa Kiongozi, kwenye Serikali ya awamu fulani?


  Ninakerwa kwasababu,

  Kauli ya I: Mbona wafanyakazi waajiriwa Serikalini au kwenye sekta binafsi hawapewi mishahara yao kidogo kidogo, wakati twafahamu wengine ni walevi, wazinzi n.k.? Kwanini nao wasitendewe kama atendewavyo mkulima?

  Kauli ya II: Hivi ni kosa kwa Mtanzania yeyote kuukosoa utawala uliopo madarakani sasa eti kisa tu aliwahi kuwa DC, RC, etc etc kwenye Serikali ya awamu fulani?


  Ni kwanini lakini? I stand to be corrected!
   
 2. peri

  peri JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kwenye chakula napinga

  na na wewe kwani serikali inapaswa kuwa makini kwa maslahi ya watanzania wote kikubwa ipandishe bei za mazao ili wakulima wanufaiki. Pili, unapokosoa jambo lazima tuone vitendo na sio maneno matupu. Kama mtu alikuwa dc, rc au waziri halafu hakutenda kile anacho hubiri baada ya kustaafu huyo ni mnafiki.
   
 3. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2011
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 1,986
  Likes Received: 1,043
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Shida ni kuwa bei ya mazao kwa mkulima ipo chini, na mfumuko wa bei ni mkubwa mno kumbuka, mkulima anapata mahitaji yake yote kupitia mazao yake. Akili ya kujua mbele kuna nini, kwa maana ya njaa hata yeye(mkulima anayo).

  Kuhusu viongozi, nadhani walitenda vile kwa kutumia ilani ya chama kilichowapa mamlaka hayo kwa wakati huo. Je, vipi kama aliamua kuachia nafasi hiyo baada ya kugundua kuwa(ilani ) haikuwa ikitenda vyema? naye hapaswi kusema?
   
 4. M

  Masuke JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Mimi nitasema kidogo kuhusu chakula hayo ya viongozi tunawaachia wenyewe viongozi, Wakulima siku zote wamekuwa ni watu wa daraja la chini lakini ndo wazalishaji wakubwa wa mazao yote ya biashara na chakula na miaka ya hivi karibuni mfano kanda ya ziwa kwa sehemu wanazolima pamba wamepunguza kwa kiasi kikubwa kulima pamba na wamejikita zaidi kwenye kulima mahindi, kwa hiyo zao la mahindi kwa sasa limekuwa ni kwa ajili ya chakula lakini pia linawapatia pesa kwa ajili ya mahitaji ya kila siku kama vile kulipa ada, kununua mboga, mafuta ya taa, chumvi, sukari, nguo, matibabu, kununua vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kujenga nyumba angalau ya bati na mahitaji mengine mengi ya kila siku. Sasa unapowazuia kuuza kwa kisingizio eti kuna upungufu wa chakula mimi naona ni kuwaonea, labda serikali ingefanya kitu kimoja kuhakikisha kwamba wakulima wanapata mahitaji yao na chakula hakitoki nje ya nchi ambacho ni serikali yenyewe kuwa wanunuzi wakuu wa mazao ya chakula pale ambapo mkulima atataka kuuza kwa ajili ya kujikimu.
   
 5. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  mkuu tatizo ni moja kwenye swala zima la mazao unakuta ukipeleka mazao nje ni rahisi kuliko kusambaza nchini kwa mfno mtu wa rukwa anaona rahisi kuuza mahindi congo kwani wanamfuata wanunuzi kuliko hapa anaekufuata ni dalali afu malalamiko kibao kwa hiyo ni bora mtu auze nje kuliko hapa..
   
 6. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2011
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 1,986
  Likes Received: 1,043
  Trophy Points: 280
  ....tena kwa bei nzuri.
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Nyingine umesahau kali kuliko zote

  "Anatafuta/unatafuta umaarufu"
   
 8. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mkuu inawezekana wewe haujalima na kujua tabu ya kilimo cha bongo, ungejua hilo basi serikali ingemruhusu mkulima kuuza chakula kokote apendako na kama unahitaji kwa ajili ya nchi basi nunua na kuifadhi ili kumfanya mkulima aweze kupata mahitaji yake na kuinua maisha yake, kuliko kumuua masikini wakutupwa na hata hatukubali utendaji wao. yaani MKULIMA NAKUWA KAMA BEKI HASIFIWI HATA SIKU MOJA!
   
 9. M

  Masuke JF-Expert Member

  #9
  Jul 23, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Sure, kama leo nilitune TBC1 nikamwona mkulima mmoja wa Mbozi anasema wakiuza mahindi kwenye masoko ya wananchi wanapata kama elfu nne kwa debe ambayo ni elfu 24 kwa gunia, lakini akasema wakiuza kwenye masoko ya serikali wanapata sh 320 kwa kilo kwa gunia lenye kilo kama 110 kutokana na maelezo ya yule mtu ni kama elfu 35, nikaona ni kitu kizuri lakini kama kutakuwa na ushindani na wafanyabiashara wa nje lazima bei ingekuwa zaidi ya hapo, mfano kwa mikoa ya Mwanza, Mara na Shinyanga debe moja sio chini ya elfu 8.
   
 10. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  1. Amepotoshwa na washauri wake.
  2. Nilipwe posho kwani mie manamba? (Shibuda)- kwani manamba si watu ?
   
Loading...