Kauli hii ya Rais ndiyo matokeo ya chaguzi hizi za hovyo

"Mkurugenzi nimekuteua mimi gari nimekupa mimi, Mshahara nakulipa mimi, Nitakushangaa kumtangaza Mpinzani mshindi."- John Joseph Pombe Magufuli

Hii ndio kauli Rais aliwahi kutoa kwa Wakurugenzi wa Halmashauri mbalimbali nchini kama agizo kwao wakati akiwaapisha ambayo ni kinyume kabisa na hadhi ya cheo chake kama mkuu wa nchi na kiongozi wa taifa, kauli ambayo ni ya kichochezi kwa taifa na inaweza kuleta madhara makubwa sana kwa jamii siku za usoni, kauli ile haikupaswa kutolewa na Rais wa nchi

Leo hii tunaona chaguzi za hovyo kabisa kuwahi kufanyika toka kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini 1992 baada ya uhuru, chaguzi ambazo tunaona ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na utawala bora ukifanyika waziwazi kabisa bila hofu kama kuna sheria zinazosimamia mchakato mzima wa uendeshaji wa zoezi la upigaji wa kura, Rais wa nchi yuko kimya kana kwamba yanayotenda yanatendeka nje ya mipaka ya Tanzania ambako hana mamlaka nako.

Kauli ile ya rais kimsingi inadharau haki ya wananchi kuamua kuchagua kiongozi wamuonaye wao anawafaa kuwatumikia, kauli ile ni tusi dhidi ya Watanzania wanaotumia haki yao kikatiba kuchagua kiongozi wao

Tafsiri ya kauli ile wananchi hawana haki ya kuchagua mwakilishi wao isipokuwa yeye na hao wakurugenzi ndio watawapa ushindi watu wawatakao wao na si wawatakao wananchi

Uzalendo anaosimama kwenye majukwaa ya kisiasa na kuaminisha wananchi kuwa anao ndio huu wa kutumikia maslahi ya chama zaidi kuliko maslahi ya taifa zima!!
Yani magari yanatokana na Kodi zetu yeye akawa kila akiona STK anahisi ni kama ng'ombe wake wapo zizini tu. Heri katuacha aisee, saitani the son of Pharaoh is gone
 
"Mkurugenzi nimekuteua mimi gari nimekupa mimi, Mshahara nakulipa mimi, Nitakushangaa kumtangaza Mpinzani mshindi."- John Joseph Pombe Magufuli

Hii ndio kauli Rais aliwahi kutoa kwa Wakurugenzi wa Halmashauri mbalimbali nchini kama agizo kwao wakati akiwaapisha ambayo ni kinyume kabisa na hadhi ya cheo chake kama mkuu wa nchi na kiongozi wa taifa, kauli ambayo ni ya kichochezi kwa taifa na inaweza kuleta madhara makubwa sana kwa jamii siku za usoni, kauli ile haikupaswa kutolewa na Rais wa nchi

Leo hii tunaona chaguzi za hovyo kabisa kuwahi kufanyika toka kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini 1992 baada ya uhuru, chaguzi ambazo tunaona ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na utawala bora ukifanyika waziwazi kabisa bila hofu kama kuna sheria zinazosimamia mchakato mzima wa uendeshaji wa zoezi la upigaji wa kura, Rais wa nchi yuko kimya kana kwamba yanayotenda yanatendeka nje ya mipaka ya Tanzania ambako hana mamlaka nako.

Kauli ile ya rais kimsingi inadharau haki ya wananchi kuamua kuchagua kiongozi wamuonaye wao anawafaa kuwatumikia, kauli ile ni tusi dhidi ya Watanzania wanaotumia haki yao kikatiba kuchagua kiongozi wao

Tafsiri ya kauli ile wananchi hawana haki ya kuchagua mwakilishi wao isipokuwa yeye na hao wakurugenzi ndio watawapa ushindi watu wawatakao wao na si wawatakao wananchi

Uzalendo anaosimama kwenye majukwaa ya kisiasa na kuaminisha wananchi kuwa anao ndio huu wa kutumikia maslahi ya chama zaidi kuliko maslahi ya taifa zima!!
Inasikitisha sana..

Wananchi walifanya subra Mungu akawapigania
 
Back
Top Bottom