Kauli hii ya Kikwete kwa anaowaita wazee wa Dar imenisononesha sana. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli hii ya Kikwete kwa anaowaita wazee wa Dar imenisononesha sana.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NdasheneMbandu, Mar 13, 2012.

 1. NdasheneMbandu

  NdasheneMbandu JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 940
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa wale waliofuatilia hotuba (siyo mazungumzo) ya Kikwete kwa anaowaita wazee wa Dar bila shaka watakubaliana nami kuwa madaktari wamedharirishwa mbele ya jamii na kuonekana kuwa ni watoto wadogo wasiotumia busara. Kwa ujumla, rais ametumia fursa hiyo kuonyesha kuwa yeye ndiye mshindi na madaktari hata iweje hawawezi kupambana na serikali.

  Miongoni mwa kauli iliyonisononesha ni pale aliposema kwamba wao kama serikali waliamua kutulia tu. Eti nao wangekataa kuongea na madaktari hali ingekuwaje? Inavyoonekana huyu MTAWALA bado hajatambua vema dhamana aliyonayo kwa wananchi katika kulinda maisha yao. Yeye anadhani kwa kugoma kuongea na madaktari angekuwa amewakomoa lakini hajui kwamba kwa uamuzi huo, angekuwa anawaumiza waliomweka pale magogoni. Ama kweli sasa nimeamini bila busara huwezi kuitwa kiongozi.

  Poleni madaktari kwa kudharirishwa kiasi hicho. Tulidhani movement yenu ingeiamusha serikali usingizini kumbe ndiyo imeiongezea blanketi lenye usingizi mnono zaidi.
   
 2. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Wewe ni ANANILEA au BISIMBA nini? Kwa nini usononeke?
   
 3. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  "ukitaka kujua uendako kukoje waulize unaokutana nao..."
   
 4. ossy

  ossy JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2012
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 877
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  ukilaza mwingine bana...
   
 5. Kiwewe

  Kiwewe Senior Member

  #5
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hii sasa ndiyo hatari kubwa kuliko mgomo. Kama Serikali haitarekebisha mambo, basi tutarajie huduma mbaya na vifo vinavyozuilika vitakuwa vingi sana. Nimemsikia Dr. mmoja humu akisema kuwa hata tumia vocha yake kuomba ushauri kwa daktari mwenzake, hatamchangia mgojwa kiasi kidogo kama amekwama baadhi ya vifaa ili ampe huduma, hatakwenda kuazima mashine ya vipimo idara nyingine, kama khajapewa chanjo hata gusa wagonjwa wanaoweza mwambukiza, kama hakuna gloves hatamgusa mgojwa. Na amesikitika kusikia wananchi wakiwalaani kwamba wao ni wauaji wakati walikuwa wakitetea kuboresha mazingira ya Afya ambayo wananchi ndiyo wafaidika. Na kunajamaa zangu wamevunjika moyo kiasi kwamba wanasema wataihama hiyo fani soon. Bila shaka Madaktari wengi wamevunjka Moyo na hivyo basi tutarajie mabaya.

  Hii hali itakuwa kama huu mgoma baridi wa waalimu, nafikiri mnajua products zinazozalishwa kwenye mashule ya serikali hivi sasa na pia matokeo ya miaka ya sasa ni mabaya mno, lakini serikali yetu sikivu haijaliona hilo bado. Basi, itakuwa sekta moja baada ya nyingine ikidhoofishwa mpaka Tanzania turudi kipindi kabla ya Uhuru ndiyo tutastuka. Nimeingiwa na uwoga mkubwa sana ndani ya nchi yangu ninayoipenda.
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  MIKUTANO YA KIKWETE NA WAZEE WA DAR:
  Imepoteza maadili na malengo ya muasisi wake Mwl Nyerere

  * Mtuhumiwa wa ufisadi anakuwa mwenyekiti wa mkutano

  NA HILAL K. SUED

  Kila enzi ina vitabu vyake, methali inasema. Kwa kifupi, tafsiri ya methali hii ni kwamba historia ina lazimu ya kuzeesha mambo, kuyapa muonekano wa kupitwa na wakati na hivyo kuyatupilia mbali.

  Kwa mfano tabia za watu wa jiji la Dar es Salaam, mienendo yao, mahitaji yao na hata fikra zao katika miaka ya sitini haviwezekani kuwepo, kuviendeleza au kufanyika tena kwa wakati huu wa sasa, labda katika kulazimisha tu, tena kwa sababu au lengo maalumu.

  Na kutokana na ukweli huo, viongozi wa nchi nao hulazimika kubadili staili zao za utawala, au tuseme utendaji wao wa kazi, na hii hutokea katika kipindi cha kila kiongozi anayekuja madarakani. Mazingira ya kisiasa yanalazimisha.

  Staili ya utendaji ya Ali Hassan Mwinyi ilikuwa tofauti na ya Mwalimu Julius Nyerere, na vivyo hivyo kwa Benjamin Mkapa kuwa tofauti na watangulizi wake wawili. Jakaya Kikwete naye ana staili yake tofauti na hao wengine wote. Wanalazimika kufanya hivyo, na si kitu cha hiari.

  Nimeanza makala yangu namna hii kwa sababu nataka kuzungumzia suala la kiongozi mkuu wa nchi kukutana na kuzungumza na wazee kuhusu masuala ya kitaifa. Aliyeanzisha mpango huu ni muasisi wa taifa hili, Mwalimu Nyerere, na alikuwa na sababu zake miaka ile ya 60 na ya 70.

  Tusisahau kwamba wazee wa Dar es Salaam ndiyo walimpokea, katika vuguvugu walilolianzisha la kudai uhuru na ndiye walimchagua kuwa kiongozi wao katika harakati hizo. Hivyo Mwalimu alijikuta amejifunga na wazee hao na hivyo kila mara alikuwa anakwenda kwao kutaka ushauri wa mambo kadha wa kadha kutatue changamoto mbali mbali zilizokuwa zinajitokeza katika harakati hizo.

  Na hata katika miaka ya baada ya uhuru, Mwalimu alijikuta ana deni au tuseme fadhila kwa wazee hao hivyo ilikuwa inamuwia vigumu kuwatupa. Naambiwa na mzee mmoja aliyewahi kuwa anahudhuria mabaraza hayo katika miaka ya mwisho mwisho ya 60 kwamba yalikuwa yanafanyika kwa njia ya usawa, kwa majadiliano, na Mwalimu alikuwa anauweka kando urais wake.

  Mijadala ya mikutano hiyo haikuwa kwa njia ya hotuba ya upande mmoja na wala haikuwa inatangazwa moja kwa moja redioni (wakati huo kulikuwa hakuna TV).

  Rais wa Awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi aliwahi kufanya mabaraza ya namna hiyo na wazee ingawa si sana. Yeye alipendelea kukutana na wananchi pale Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba kila mwisho wa mwezi, kusikiliza matatizo yao.

  Utaratibu huu ulisitishwa baada ya kuja mfumo wa vyama vingi. Kwa wanaokumbuka, Mwalimu Nyerere aliwahi kumkosoa Mwinyi kwa utaratibu wake huo kwa kumwambia kuwa matatizo ya wananchi ni mengi mno hivyo yeye kama Rais hataweza, na hana muda wa kuyasikiliza kutoka kwa kila mmoja mmoja.

  Benjamin Mkapa, Rais wa Awamu ya tatu naye aliwahi kufanya mikutano na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambayo pia haikuwa ya utaratibu ule wa ‘mwalimu’ wake, Julius Nyerere. Isitoshe wakati wa Mwalimu kulikuwa chama kimoja tu cha siasa TANU – na baadaye mrithi wake – CCM. Hivyo wale wazee wote walikuwa ni wanachama au wafuasi wa chama hicho.

  Katika enzi hii ya mfumo wa vyama vingi ni vigumu kwaona wazee hao kuwa ni wa majumuisho ya vyama mbali mbali vya siasa – ni wale wale wa chama tawala, ingawa haitamkwi bayana kwamba sasa hivi mikutano hiyo ni wazee wa vyama vyote. Hali hii bila shaka imeachwa kimakusudi na watu wawe wanahisi tu.

  Lakini katika enzi hii ya Jakaya Kikwete tunaishuhudia mikutano hiyo kwa utaratibu tofauti kabisa – imegeuzwa kuwa ni jukwaa la yeye kutoa hotuba kwa wazee hao na siyo kujadiliana nao kwa njia ya usawa kama ilivyokuwa enzi za Mwalimu Nyerere.

  Kwa ujumla mikutano hii ya Kikwete na wanaodaiwa kuwa wazee wa Dar es Salaam imegeuzwa kuwa mahali pa kulishitaki kundi fulani katika jamii linaloonekana kwenda kinyume cha utaratibu – na kuashiria tishio kwa chama tawala. Ni mahala pa kujipa ahueni (solace) kutoka kwao.

  Mwezi Novemba mwaka jana Kikwete alikutana na wazee hao katika ukumbi wa PTA Kilwa Road kuwahutubia kwa kuwatuhumu Wabunge wa Chadema kususa kwao Bungeni mjadala wa Muswada wa Mchakato wa katiba Mpya.

  Wengi wanaona kuwa sasa mikutano hiyo imekuwa ni ya kutafuta huruma kupitia wazee, mfumo ambao umepitwa na wakati kwani nchi ina idadi kubwa ya vijana (zaidi ya asilimia 70 ya Watanzania wote) wenye matatizo (silipendi neno ‘changamoto’) lukuki hivyo wao pengine ndiyo wa kukutana nao na ambao wangependa kusikilizwa.

  Hilki linatokana na ukweli kwamba vijana ni kundi muhimu katika jamii ambalo Kikwete anafanya makosa makubwa kulikwepa kwani wao ndiyo walimuingiza madarakani mwaka 2005 wakiwa na matumaini makubwa.

  Mapema mwezi May 2005 aliporudi Dar kutoka Dodoma baada ya CCM kumteua kugombea urais msafara wake wa kutoka Dar es Salaam Airport kuja mjini ulikuwa na umati mkubwa wengi wao wakiwa vijana.

  Wengine walilala barabarani kwa furaha na matumaini na wengine hata kudandia gari lake wakipiga kelele ‘Ajira! Ajira,” – suala ambalo limekuwa tatizo lao kubwa na ambalo hadi sasa bado ni kizungumkuti kwa Kikwete. Wazee hawakuonekana kabisa kufanya hivyo.

  Na vivyo hivyo ilivyokuwa mikoani alipokwenda kujitambulisha na baadaye katika kampeni zake wakati wa kuelekea uchaguzi mwaka huo.

  Leo hii Kikwete anawaona vijana hawana chochoe cha kumueleza. Pengina amebaini kwamba vijana ni bomu ambalo katika mpangilio wa sera zake, litampasukia tu kabla ya kuondoka madarakani.

  Anaona ni bora awakumbatie wazee kwani bila shaka akiwa miongoni mwao anajisikia anafuraha kwani wazee huwa hawana madai ya msingi kutoka kwake ukilinganisha na vijana.

  Pia anatambua fika kwamba akiwa miongoni mwa wazee hao (ambao wengi wao ni wa CCM kama nilivyotaja), watampigia makofi, vigelegele kwa lolote atakalolisema. Narudia, kwa lolote atakalolisema, kwani huwa hawana uwezo wa kuhoji au kujadili masuala magumu (complexities) yanayokabili taifa na jamii katika enzi za sasa.

  Isitoshe hata katika kile kinachoitwa ‘serikali ya CCM’ kupoteza muelekea, na sasa ‘kuelekea korongoni’ kutokana na ufisadi, kutowajibika na kupotea kwa utawala bora kulikokithiri ndani ya serikali hiyo, hata siku moja hatujasikia wazee hao wamejiotokeza kukemea vitendo hivyo, hasa vile vya ufisadi mkubwa na wizi wa waziwazi wa fedha na mali za umma uliotokea kama vile EPA, Deep Green, Radar, Meremeta na nyinginezo nyingi tu.

  Walikaa kimya kabisa!!! Katika wizi wa EPA Kikwete alionelea ni bora kwenda Bungeni kuweka mashitaka na kutoa hukumu kwa watuhumiwa huku wazee wakikwepwa.

  Jumatatu ya wiki hii alikutana nao wazee hao katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Hall pia kwa njia ya kuwahutubia – kuwashitaki kwao madaktari waliogoma na wanaharakati waliowaunga mkono.

  Lakini kama mtu anataka kudodosa zaidi jinsi mikutano ya aina hiyo ilivyopoteza mantiki na pia maadili (moral standing) ni kuona baadhi ya wazee wanaobeba tuhuma nzito za ufisadi kuwa wenyeviti wa wazee hao.

  Katika mkutano wao wiki iliyopita wengi walistushwa kumuona Idi Simba, Mbunge wa zamani wa Ilala na aliyepata kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara chini ya Mkapa kuwa eti ndiyo mwenyekiti wao.

  Sote twafahamu Idi Simba alijiuzulu uwaziri (baada ya kushinikizwa) kutokana na kashfa ya kutoa vibali vya uingizaji nchini wa sukari kwa njia za upendeleo.

  Na hivi karibuni tu, ‘mzee huyo’ ametajwa katika kashfa ya ubinafsishaji wa kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA) (ambayo yeye ni mwenyekiti wa bodi yake) pale ilipogundulika kwamba baadhi ya fedha za malipo zillingizwa katika akaunti yake binafsi.

  Hivyo kuonekana katika hafla kubwa ya wezee hao wakiwa na mkuu wa nchi kama ‘kiongozi’ wao, na wao (wazee) bila kuhoji ‘ushiriki’ wake kunawakupunguzia sana hadhi wazee hao katika masuala ya kusimamia na kuhimiza uadilifu katika serikali na jamii. Wazee hao wanaonekana kama vile wanayaendeleza maovu hayo, bila ya wao kushituka.

  Chanzo: RAI

  MY TAKE:

  Hayo mambo ya JK ni kama aliyowahi kuambiwa na Makongoro Nyerere katika kikao cha NEC-CCM. Alimwambia JK kwamba "huko saiti wanasema haukutakiwa kufanya hivyo."

  Kweli JK hana aibu kabisa; Anakubali kukaribishwa na Idi Simba kwenye mkutano? Mwl Nyerere asingekubali hii. Tanzania chini ya JK maadili chali kabisa!

 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7

 8. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Watasema tuhuma dhidi yake hazijathibitishwa, utafikiri malaika toka mbinguni ndiyo waje kuthibitisha!
   
Loading...