Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,173
Mwanasaikolojia maarufu nchini Marekani aitwaye Phil McGraw aliwahi kusema kwenye mada zake tuwe waangalifu sana na watu wanaojibu hoja ambazo wala hawajaulizwa.
Alisema mtu anapoanza kujibu maswali ambayo hajaulizwa inaashiria nafsi yake inamsuta na anaona umuhimu wa kujitetea bila ya hata ya kuulizwa. Hivyo majibu yake yachunguzwe ili kufahamu nini kinamsumbua mhusika huyo.
Nikitumia mbinu hiyo ya Dr. Phil kwa JK nimeona kauli zake zimebadilika mno nikilinganisha sasa na mwaka 2005. Sasa hivi JK anaona umuhimu wa kutuhakikishia ya kuwa atashinda hali ambayo hakuwa nayo mwaka 2005. Yamemsibu nini? Kama ushindi hauna wasiwasi kwa nini anatuelezea sisi. Si asiandikie mate na huku wino upo?
Kwa lugha nyingine ni kwa nini anajibu maswali ambayo hajaulizwa? Hakuna aliyemuuliza kama hatashindwa au atashinda sasa haya majibu yanatoka wapi?
Kwa kujibu maswali ambayo hatujamuuliza na ambayo mwaka 2005 hakuona shinikizo la kuyajibu kwa vile hapakuwepo upinzani tishio ni dhahiri maji yamemfika kwenye koromeo na anaona kuna uhaja wa kujifariji na ushindi njozi angalau kutoka kwenye kinywa chake.................
Hii siyo hali nzuri hata kidogo kisaikolojia kwa JK na CCM yake.............Kujihami kwa kujifariji.....
Inaonyesha ni dalili za awali za kuanza kukiri kuwa huenda Jk na CCM yake wataanguka na ndiyo maana wanapata mashinikizo ya kujibu hoja ambazo hata hazipo mezani....................
Twendeleeni kuwasoma kwa ukaribu wastaafu hawa watarajiwa............ili kwenye historia zetu tuje tuweke rekodi vizuri wakati tunajibu swali............Hivi ni lini jamii ilielewa JK na CCM yake sasa imetosha?