Kauli hii ya JK kuhusu mchakato wa kupata Katiba mpya imejaa utata | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli hii ya JK kuhusu mchakato wa kupata Katiba mpya imejaa utata

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Patriote, Feb 6, 2012.

 1. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Katika kuadhimisha miaka 35 ya kuzaliwa kwa CCM Rais Kikwete aliwapongeza wabunge wa CCM kwa uamuzi wao wa kuitetea Sheria ya Mabadiliko ya Katiba mpya 2011, na aliwaambia kwamba muswaada huo umeshawasilishwa tena bungeni, hivyo ataunda tume ya kukusanya maoni kwa Watanzania ambapo aliwaomba wana CCM kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao, maana muwamba ngoma huvutia kwake.

  “Hili la Katiba mpya tumechukua mapendekezo ya vyama vya upinzani, kikiwemo CCM ambacho nacho kimetoa mapendekezo manane. Nawashukuru sana wabunge wa CCM katika hili, lakini wana CCM jitokezeni kwa wingi kutoa maoni yenu maana muwamba ngoma huvutia kwake.”

  Maoni yangu


  Rais anaingiza suala la itikadi ya vyama katika kuandaa Katiba ya Taifa ambayo ndiyo Sheria mama ya nchi. Rais anasahau kuwa Katiba inayoandaliwa sio mali ya chama fulani na hivyo hakupaswa kutoa matamshi haya ya muwamba ngoma huvutia kwake. Hii maana yake ni kwamba kwa kutumia Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Mpya iliyopitishwa na Bunge na yeye kuisaini na kuirudisha tena Bungeni.

  Kwa maneno haya watanzania tusio wa CCM tusitegemee kupata haki zetu kupitia Katiba Mpya itakayotengenezwa kwa Sheria hiyo iwapo Bunge litakataa kuijadili upya kwa kuwa Rais anaamin dhana ya Muwamba ngoma huvutia kwake inahitajika kutumika katika kuandaa Katiba Mpya. Na inawezekana ndio maana waliowekwa kusimamia mchakato mzima wa kuandaa Katiba mpya ni wanaCCM kuanzia maDC, ma RC na wengineo. Nini kifanyike kama Bunge litagomea kuujadili upya Sheria hiyo????
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Ni usanii tu. Katika vikao na Chadema alisema anakubaliana na mapendekezo yao.
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mkuu huyu jamaa akiwa Davos anaongelea ku Manufacture teachers anakosea hata anacho ulizwa ana anza kuchanganya na zake ulitegemea pale atasema nini ? Mie nilisha choka kabisa mkuu wangu wacha tuone.
   
 4. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Pole kiongoz, tulielezwa kuwa kura nyingi za huyu bwana zilitoka vijijini, tuvumilie tu. Hii ndio athari ya kuchaguliwa Rais na wanavijiji.
   
Loading...