Kauli Bora za Viongozi

Mariswaga

JF-Expert Member
Aug 25, 2015
201
2
KIKWETE
"Hatujakosea kumteua Dk. Magufuli kwani ana sifa zote, ni mwadilifu, mwaminifu na mchapakazi ambaye ameonesha kwa vitendo hivyo atawafikisha Watanzania sehemu sahii wanayotaka"

JAJI JOSEPH WARIOBA
"Dr. Magufuli ni mchapakazi na hana masihara, miaka 20 aliyofanya kazi inatosha kuelezea jinsi alivyo muadilifu na mchapakazi"

ABDURAHMAN KINANA
"CCM tumejipanga vizuri kimuundo, kihoja na kimkakati kwa ushindi mkubwa wa kishindo unaokuja kupitia wagombea wetu waadilifu na wachapakazi"

MAPINDUZI PEMBA
Mwenyekiti wa Bodaboda wilaya ya Ilala
"Madereva bodaboda tuko tayari kupiga kampeni nchi nzima hata kwa miguu ili kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo kwenye uchaguzi huu"

Kiongozi bora ni lazima awe Muadilifu, Mchapakazi, Mzalendo wa kweli na mwenye rekodi nzuri zaidi kiutendaji

CHAGUA CCM, CHAGUA MAGUFULI
 
Nendeni Tanganyika pakers mkaone viongozi bora sio kujifungia lumumba na masaki na kuandika huu -----
 
Vpi Kuhusu Ile Meli Alokamata Na Faini Ya US DOLAR 3.5 Pamoja Na Fain Ingine Ya Muda Tulowapotezea Wachina Wale
Je Atalipa Magufuli, Ccm, Au Watangananyika Wote?
 
NUKUU ZA VIONGOZI

''Mweshimiwa Mwenyekiti wangu wa Taifa naomba unisamehe lakini ukweli utabakia kuwa ukweli. Wewe ni Mwenyekiti wangu wa Taifa lakini ulikaa na wanafiki ndani ya chama ambao kwa kiasi kikubwa wametufanya tufike hapa tulipo

''Kwa hiyo ninakuomba Mwenyekiti wangu mpendwa ukitengeneze chama chetu vizuri. Usiwaonee huruma wanafiki. Ukishamgundua mnafiki leo, usikae naye, fukuza kesho. Ni mara kumi tubaki na wanachama wachache kuliko kukaa na wanachama wanafiki wanatuhujumu na kusabisha kushindwa kufika kwenye malengo yetu ya chama.

''Naomba Mwenyekiti wangu unisamehe kwa kulisema hili kwa sababu kama nisingelisema lingekaa kama kiungulia ndani ya moyo wangu wakati nimekumbana nalo sana wakati nafanya kampeni sehemu mbali mbali nchini.''

- Rais Dr. John Pombe Magufuli
30 Novemba 2015


 
Back
Top Bottom