Kauli au msemo maarufu wa CCM unaoniudhi na kunikatisha tamaa ni huu hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli au msemo maarufu wa CCM unaoniudhi na kunikatisha tamaa ni huu hapa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Dumelambegu, Apr 11, 2011.

 1. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,053
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Wapendwa wana JF,

  ''Tunaunda timu kabambe ya ushindi wa kishindo ifikapo 2015''. Hicho ndicho kibwagizo cha chama hiki cha CCM kilichopauka na kupauka na kupoteza mvuto mbele ya kizazi kipya. Akili ya CCM imejielekeza kupata ushindi wa kishindo na siyo kuunda timu itakayoiletea nchi maendeleo. Ndiyo maana wanaopata vyeo ndani ya CCM ni wapiga domo na siyo watu wenye akili, mipango na uzalendo wa kuikomboa nchi yetu kimaendeleo.
   
 2. M

  Mopalmo JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 453
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hii haiwaingii akilin vijana wote hivyo wasubiri waone 2015 kibao kitakavyo wageukia
   
 3. A

  Anyambilile Member

  #3
  Apr 11, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna kazi kwelikweli kujivua gamba mwishowe huyu nyoka atakufa kwa kumchuna ngozi.CCM wachane na mambo ya kizamani hii ni tanzania ya kizazi kipya wafanye utafiti wa kutosha ili kuweza kuweka chama kiwe salama na ninocho jua kwa wasomi hawezi kwenda maana hali ilisha badilika. Ngoja tusubri
   
 4. B

  Bobby JF-Expert Member

  #4
  Apr 11, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,673
  Likes Received: 171
  Trophy Points: 160
  DM kwani kipi kinachokushangaza? Bahati mbaya sijawahi na sitasoma katiba yao asilani, lakini walioisoma wanasema lengo kuu lililoanishwa kwenye katiba ni kushinda uchaguzi full stop. Kipi kinafuata baada ya kushinda huo uchanguzi, nikimaanisha ni namna gani wamwondoe mtanzania kwenye umaskini si issue kwao no wonder wanafanya madudu kila uchao kwenye serikali lakini wanaona poa tu, business as usual.

  By the way, did you know kwamba chanzo kikuu cha migogoro ya sasa ndani ya ccm ni viti vya ubunge walivyopoteza 2010 na kura ndogo walizopata za urais? ccm watu wa ajabu na wanakera sana sana, yaani kushindwa kwa mwenyekiti wao kuongoza hii nchi na kuisababisha matatizo lukuki ya kijinga kwao si tatizo. Ila tatizo ni kupoteza viti vya ubunge wakati hata wakivipata huwa wanaenda kulala tu Dodoma. Ninaitamani na kuiongoja kwa hamu siku ambayo majority ya watanzania watang'amua kwamba chanzo cha matatizo yao ya kuendelea kuogelea kwenye umaskini wakati wana kila aina ya resource ni ccm kwa kuwa imegoma kubadilika. Hii siku ikinikuta nikiwa hai nitakosa maneno ya kumshukuru Mungu kwa tunu hiyo isiyo na kifani.
   
 5. kwempa

  kwempa Member

  #5
  Apr 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "Tunaunda timu kabambe ya ushindi wa kishindo ifikapo 2015'' Ni heri kama wangeunda timu ya kuwasaka mafisadi kwa nguvu zote@@
   
 6. Linamo

  Linamo JF-Expert Member

  #6
  Apr 11, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 6,376
  Likes Received: 13,483
  Trophy Points: 280
  Navyojua mimi maneno ya CCM siyo MSAAFU wala BIBLIA kusema kwamba hayawezi kubadilika,wakati wa kuburuzwa umekwisha.
   
 7. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #7
  Apr 11, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,034
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  CCM???????????????????/ BORA angerudi mwingereza au mjerumani kututawala tutapata maendeleo
   
 8. mangi waukweli

  mangi waukweli JF-Expert Member

  #8
  Apr 11, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 246
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yani akiliyako ndiyo imefikia mwisho wa kufikiri kabisa,ccm wanachokifanya kinaitwa strategic plan na huwezi kuwaletea maendeleo wananchi kama hujapata ridhaa kwa wananchi wakupigie kura then mambo mengine yanafuata,hakuna plani nzuri kama huji asses mwenyewe ccm tayari wameshagundua weakness zao wanajipanga upya kwa ushindi wa 2015 wewe unacheka unafikiri itakusaidia kuitoa ccm madarakani? We endelea kulala
   
 9. w

  wa hapahapa JF-Expert Member

  #9
  Apr 3, 2015
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 4,972
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  kirusi hatari
   
 10. mr brocken

  mr brocken Senior Member

  #10
  Apr 3, 2015
  Joined: Apr 2, 2015
  Messages: 166
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ivi uwezi kuchangia bila kuchanganya lugha
   
 11. Kifimboplayer

  Kifimboplayer JF-Expert Member

  #11
  Apr 3, 2015
  Joined: Nov 24, 2013
  Messages: 1,388
  Likes Received: 212
  Trophy Points: 160
  huyu mkuu sijui bado yuko hai
   
 12. mr brocken

  mr brocken Senior Member

  #12
  Apr 3, 2015
  Joined: Apr 2, 2015
  Messages: 166
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wangelikuwa wa maana wangelitumia kauli mbiu hii, 2015 tutaunda timu kabambe ya kuwakamata wauwaji wote wa ndugu zetu ma albino
   
 13. B

  Bobby JF-Expert Member

  #13
  Apr 5, 2015
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,673
  Likes Received: 171
  Trophy Points: 160
  Bao napumua kuu Kifimbo!
   
 14. h

  hapohapo Member

  #14
  Apr 5, 2015
  Joined: Feb 5, 2015
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukowap ewe mkoloni ulie tutawala rud pleas upngoz umetushnda at a zile leli tumeshndwa kubolesha viwanda vimetushnda Madin nanishat ndo kabisa tunagawa bule pleas rud walau uchukue hivi vitu walau utatuachia ata barabara bola nakutuboleshea huduma za jamii.nakukumbuka ewe mkoloni huku kuna watu wametengeneza katba inayo ruhusu kuiba kama were ulvyo Fanya wao wanakula mpaka mifupa bola wewe ulie kula mifupa ukasaza.
   
 15. Kifimboplayer

  Kifimboplayer JF-Expert Member

  #15
  Apr 6, 2015
  Joined: Nov 24, 2013
  Messages: 1,388
  Likes Received: 212
  Trophy Points: 160
  umekuwa adimu mkuu Bobby we mwenyewe unajua...
  Au ndo mambo multiple @id's

  jambo la kheri sana kama kushuhudia huyu dhalimu wa maisha ya mtanzania akifungisha virago
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Qualifier

  Qualifier JF-Expert Member

  #16
  Apr 6, 2015
  Joined: Dec 14, 2012
  Messages: 1,235
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Absolutely true!!!
   
 17. B

  Bobby JF-Expert Member

  #17
  Apr 6, 2015
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,673
  Likes Received: 171
  Trophy Points: 160
  Nashukuru mkuu ni kweli nimeadimika kdg si kwa sbb nina ID nyingine, hpn majukumu kidogo yameongezeka.

  Acha tu mkuu siku hizi hata siongei sana. Mm sishangilii sana kuondoka kwa huyu mtaalamu wa fundraising kwani sijajua watanzania watamweka nani come October. Upo uwezekano mkubwa ni kutoka timu ile ile inayotufanya tuendee kuogelea kwenye umasikini zaidi ya nusu karne baada ya uhuru wakati tuna kila aina ya rasilimali tunayohitaji kwa maendeleo.

  Namna ambavyo huyu anayemaliza muda alivyovishusha viwango vya utendaji, sitarajii miujiza kutoka kwa ajaye.

  Kizuri ni kwamba sijakata tamaa kwamba Tanzania yenye uwajibikaji na neema yaja japo sijui ni lini.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...