Kauli 10 za mtu asiye na malengo wala uthubutu

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
1,481
2,000
1: Sina Mtaji
mara nyingi mtu asiye na malengo na uthubutu hukili kukosa mtaji..hata kama anao hawez kujua aufanyie nini mana hajaweka malengo

2: Sina Connection
Mtu asiye na malengo wala uthubutu hukili pia kukosa connection'mwingine atajiuliza nitaanzia wapi?'hukili kukosa pa kuanzia..

3: Nitaanza Rasmi kesho
hahaaa..kesho ikifika anasogeza tena kesho, kumbuka kesho haziishi..kesho hutokea kila siku,( hata leo ina kesho, kesho pia ina kesho..mwendelezo wa kesho..kesho, kesho , kesho.....

4: Mimi ni wa hivi hivi tu
asiye na malengo hukili uthaufu alionao na kukubali kuendelea kuwa sehemu alipo, hawezi kupiga hatu mana yeye anaona ni wa hivo na ni wa hapo kwa sababu hana malengo na hana dira hivyo haoni pa kwenda na hahangaiki kutafuta uelekeo ( pa kutokeza) mana hana malengo na ameridhika.

5: Mifumo mibovu ya serikali ndiyo inayonirudisha nyuma
mara nyingi mtu asiye na malengo hulalamika tu, et serikali ndiyo imesababisha awe jinsi alivyo, kana kwamba serikali imefumba macho yake na fikra zake..huyo hana malengo

6: Mke/mume/ndugu zangu ndiyo waliyonirudisha nyuma kimawazo
asiye na malengo hupoteza mda kwa kulaumu na kulalamika tu bila kuchukua hatua,,japo inaweza kutokea kukutana na watu kama hawa wakawa vikwazo, ila kumbuka hawawez kukuzuia kuinuka tena na kuanza upya,, acha kushikilia makosa uliyofanyiwa,usipoteze muda kwa kulalamika na kulaumu juu ya mabaya uliyofanyiwa..utachelewa sana,, tafuta suruhisho la makosa hayo na uyatatue,,

7: Kupata ni majaliwa
hahahaa..hii ndo inachekesha sasa, huwez kujaliwa kupata bila kutafufa , ukiwa umekaa tu na kujikatia tamaa eti kupata ni majaliwa..waliyojaliwa kupata walipata baada ya kutafuta, hawakupata wakiwa wamekaa.

8: Usilazimishe mambo
kama una malengo ya jambo fulani ni lazima ufanye bidii na kulazimisha yatokee, onyesha bidii zako.

9: Kuna watu special siyo mimi
hivi hao watu special uspecial wao ukoje? Wanatofauti gani na wewe..hata wewe ni special ukiamua , usiendelee kukaa tu na kusema et kuna watu special, hata hao unaowadhani ni special waliamua kuwa special..kwa nini wewe usiamue kuwa special??

10: Sina bahati
hivi maendeleo ni kubahatisha?!mmhusibahatishe mambo, weka mipango na mikakati yako ya kutoka ( strategic plan)
 
Son of Gamba

JF-Expert Member
Oct 26, 2012
3,389
2,000
Nakubaliana na wewe kwa kiasi fulani, lakini pia wapo watu wana "ideas" kibao za kutoboa lakini wamekosa "mitaji".

Unaweza ukawa na mikakati, mbinu, maarifa, jitihada, na kila namna ya malengo, lakini ukakosa capital na ukabakia hapo hapo ulipo.
 
Eyce

JF-Expert Member
Mar 16, 2016
3,239
2,000
Sometimes kuna milango ikigoma kufunguka haimaanishi sisi ni wabovu, wadhembe au hatujaweka focus ila tu ni kuwa hiyo milango ni ya watu wengine, yetu ipo wazi mahali pengine

Hata diamond angekomaa na elimu pengine angekuwa hata karani ambaye ni nadra kufikia level za umaarufu na mafanikio aliyonayo

Inshort, kukubali umeshindwa na kuacha unachokifanya, ni njia mojawapo ya kuelekea kule unapotakiwa kufika
 
glass amo

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
3,038
2,000
Nakubaliana na wewe kwa kiasi fulani, lakini pia wapo watu wana "ideas" kibao za kutoboa lakini wamekosa "mitaji".

Unaweza ukawa na mikakati, mbinu, maarifa, jitihada, na kila namna ya malengo, lakini ukakosa capital na ukabakia hapo hapo ulipo.
Penye nia pana njia. Nakataaa huu utetezi wa kimasikini
 
green rajab

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
2,672
2,000
Anashindwa hata kutongoza mademu anaanza kujiita mgumu kumbe domo zege au Govinda kabisa
 
Son of Gamba

JF-Expert Member
Oct 26, 2012
3,389
2,000
Penye nia pana njia. Nakataaa huu utetezi wa kimasikini
Wewe hujui bado maisha yalivyo na siwezi kubishana na wewe. Lakini, kuna watu wamepitia magumu katika maisha, nafikiri hao watanielewa namaanisha nini.

Tatizo la "motivational speakers" hawajui uhalisia wa maisha. Kauli kama, "penye nia pana njia", imekaa ki-motivational zaidi.
 
mulwanaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
4,324
2,000
1: Sina Mtaji
mara nyingi mtu asiye na malengo na uthubutu hukili kukosa mtaji..hata kama anao hawez kujua aufanyie nini mana hajaweka malengo

2: Sina Connection
Mtu asiye na malengo wala uthubutu hukili pia kukosa connection'mwingine atajiuliza nitaanzia wapi?'hukili kukosa pa kuanzia..

3: Nitaanza Rasmi kesho,,
hahaaa..kesho ikifika anasogeza tena kesho, kumbuka kesho haziishi..kesho hutokea kila siku,( hata leo ina kesho, kesho pia ina kesho..mwendelezo wa kesho..kesho, kesho , kesho.....

4: Mimi ni wa hivi hivi tu,
asiye na malengo hukili uthaufu alionao na kukubali kuendelea kuwa sehemu alipo, hawezi kupiga hatu mana yeye anaona ni wa hivo na ni wa hapo kwa sababu hana malengo na hana dira hivyo haoni pa kwenda na hahangaiki kutafuta uelekeo ( pa kutokeza) mana hana malengo na ameridhika.

5: Mifumo mibovu ya serikali ndiyo inayonirudisha nyuma..
mara nyingi mtu asiye na malengo hulalamika tu, et serikali ndiyo imesababisha awe jinsi alivyo, kana kwamba serikali imefumba macho yake na fikra zake..huyo hana malengo

6: Mke/mume/ndugu zangu ndiyo waliyonirudisha nyuma kimawazo,
asiye na malengo hupoteza mda kwa kulaumu na kulalamika tu bila kuchukua hatua,,japo inaweza kutokea kukutana na watu kama hawa wakawa vikwazo, ila kumbuka hawawez kukuzuia kuinuka tena na kuanza upya,, acha kushikilia makosa uliyofanyiwa,usipoteze muda kwa kulalamika na kulaumu juu ya mabaya uliyofanyiwa..utachelewa sana,, tafuta suruhisho la makosa hayo na uyatatue,,

7: Kupata ni majaliwa..
hahahaa..hii ndo inachekesha sasa, huwez kujaliwa kupata bila kutafufa , ukiwa umekaa tu na kujikatia tamaa eti kupata ni majaliwa..waliyojaliwa kupata walipata baada ya kutafuta, hawakupata wakiwa wamekaa.

8: Usilazimishe mambo,,,
kama una malengo ya jambo fulani ni lazima ufanye bidii na kulazimisha yatokee, onyesha bidii zako.

9: Kuna watu special siyo mimi,,
hivi hao watu special uspecial wao ukoje? Wanatofauti gani na wewe..hata wewe ni special ukiamua , usiendelee kukaa tu na kusema et kuna watu special, hata hao unaowadhani ni special waliamua kuwa special..kwa nini wewe usiamue kuwa special??

10.. Sina bahati,,
hivi maendeleo ni kubahatisha?!mmhusibahatishe mambo, weka mipango na mikakati yako ya kutoka ( strategic plan)
11. Kuna mikono ya watu kwenye kila kazi nao jaribu kufanya.

12. Maisha yangu yote nimemkabidhi bwana Yesu

13 Maisha tunakaa mda mfupi hi dunia nimapito tu.
 
Fall Army Worm

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
11,391
2,000
100% n ukwel huo tabia hizo nilikuwa nazo zaman had nilipoona mvi moja kwenye ndevu nkashtuka kinyama nikajua umri haunisubir nichukue hatua

Usiulize sahiz nina mvi ngapi
Sasa mvi si ni mambo ya kurithi Mkuu?. Maana unaweza kuta mtu ni kijana mdogo lkn tayari ana mvi.
 
KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
15,983
2,000
Motivational speakers wanawaharibu sana vijana kwa kuwafanya waishi maisha ya kufikirika baada ya kuishi katika uhalisia wa maisha..........
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom