mwanauvinza
JF-Expert Member
- Jul 24, 2023
- 365
- 1,045
Nipo likizo Kahama. Jana jioni rafiki yangu alinunua chupa mbili kubwa za Pombe ya KVant kwenye duka la jumla hapa Mjini. Tulipoanza kutumia nikagundua zina ladha tofauti. Na kweli tulipochunguza zile lebo tukagundua zina utofauti na KVant original.
Tulipozirudisha dukani muuzaji akatutisha kwamba atatufanyia kitu mbaya, tukaenda kutoa taarifa Polisi.
Tulipowaelekeza duka wao wenyewe Polisi wakasema kama ni dukani kwa Mushi magumashi pale ndio zake, kisha wakatuambia tusamehe tu au kama tumekereka sana tukatoe taarifa TRA.
Walevi wenzangu tuwe makini, Pombe feki zimetapakaa mitaani ndio maana wagonjwa wa Figo wanaongezeka kila kukicha.