Katumbi : nitarudi nyumbani hivi karibuni kuongoza maandamano.

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
7f8b7af4d459a0e986431cd83747a68f.jpg

Mwanasiasa wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Moise Katumbi Chapwe ambaye amekuwa nchini uingereza kupata matibabu amesema atarudi nyumbani kuongoza maandamano ya amani dhidi ya Rais Joseph Kabila.

Mwezi uliopita, Katumbi alihukumiwa jela kwa makosa ya kuhusika na uuzaji wa nyumba kwa njia ya ulaghai kwa raia mmoja wa ugiriki.

Mahakama mjini Lubumbashi ilimuhukumu jela miaka 3,hata hivyo Katumbi hujasema ni lini atarejea nyumbani lakini amesema tu kuwa atafika jijini Kinshasa hivi karibuni.

Tayari Katumbi amesema atawania urais dhidi ya Joseph Kabila ikiwa ataamua kuwania tena.

Thomas Dakin mwenyekiti wa mashirika ya kiraia Mashariki katika jimbo la kivu kaskazini amesema ni haki ya Katumbi kuandaa maandamano nchini humo ikiwa atarejea.

Katumbi ameendelea kuilaani Serikali ya Kinshasa kwa kumlenga kisiasa ili asiwanie urais.

Serikali ya Kinshasa imeshtumu Katumbi pia kwa kuhatarisha usalama wa nchi hiyo kwa kuwatumia mamluki kutoka marekani kumlinda.
 
Uyu jamaa alipoingia kwenye siasa ndio kajiaribia.sumtime is gonna die soon.
 
Uyu jamaa alipoingia kwenye siasa ndio kajiaribia.sumtime is gonna die soon.
Hakuna cha kujiharibia unataka aachiwe Kabila mpaka lini

Acha apambane tu haki lazima msukosuko.!
 
Back
Top Bottom