Katumbi asalimu amri kwa Samatta, kuongozana nae Ubelgiji

Wonderful

JF-Expert Member
Apr 8, 2015
7,347
5,985
VUTA nikuvute ya muda mrefu kati ya mmiliki wa klabu ya TP Mazembe, Moise Katumbi na Mbwana Samatta imemalizika jana Ijumaa baada ya mmiliki huyo kukubali mshambuliaji wake kuondoka kwenda kumalizana na KRC Genk ya Ubelgiji.

Samatta anatarajia kuondoka usiku wa leo kuelekea Ubelgiji ambako atasaini mkataba wa miaka minne na nusu ukiachana na ule wa awali aliokuwa amesaini kabla ya Genk kumalizana na Katumbi jambo ambalo lilizua mtafaruku ambao uliingiliwa na serikali ya Jamuhuri ya Muungano Tanzania kupitia Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo.

Katika msafara huo wa kwenda Ubelgiji, Samatta ataambatana pia na bosi wake Katumbi ambaye atashuhudia usainishwaji wa mkataba huo.

"Baada ya majadiliano ya muda mrefu hatimaye Katumbi amekubali kumwachia Samatta hivyo ataondoka leo usiku kwenda Ubelgiji kumalizana nao kabisa. Akimaliza atarejea nchini kwa ajili ya maandalizi yake ya kwenda kuitumikia klabu hiyo mwezi ujao," alisema mtu wa karibu wa Samatta.

Jana Meneja wake, Jamal Kasongo alisema kuwa walikuwa na kikao na serikali pamoja na mwanasheria wao kikao ambacho kinaonyesha kuzaa matunda
 
Tunamtakia mafanikio mema huko Ubelgiji aipeperushe bendera yetu
 
Kweli lazima serikali imeingilia kati inasemekana huyu jamaa hana kawaida ya kuuza wachezaji.wakiwa bado na uwezo.
 
Katumbi huyu ndio yule muimbaji wa Dar es salaam Ikibindankoi na wakina Alain Mulumba?
 
Sijapenda hii ya serikali kuingilia kati,wangeacha Samatta amalizane na klabu yake kiroho safi badala ya wao kuingilia kati name kuishinikiza TP Mazembe kumuachia huru Samatta, bila TP Mazembe Samatta asingejulikana, hivyo klabu yake ina haki zote juu yake kwavile mkataba wake haujamalizika bado,kwa tabia hii ya serikali kuingilia mambo yasiyowahusu watasababisha wachezaji wengine wa Tanzania wasichukuliwe na klabu hiyo
VUTA nikuvute ya muda mrefu kati ya mmiliki wa klabu ya TP Mazembe, Moise Katumbi na Mbwana Samatta imemalizika jana Ijumaa baada ya mmiliki huyo kukubali mshambuliaji wake kuondoka kwenda kumalizana na KRC Genk ya Ubelgiji.

Samatta anatarajia kuondoka usiku wa leo kuelekea Ubelgiji ambako atasaini mkataba wa miaka minne na nusu ukiachana na ule wa awali aliokuwa amesaini kabla ya Genk kumalizana na Katumbi jambo ambalo lilizua mtafaruku ambao uliingiliwa na serikali ya Jamuhuri ya Muungano Tanzania kupitia Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo.

Katika msafara huo wa kwenda Ubelgiji, Samatta ataambatana pia na bosi wake Katumbi ambaye atashuhudia usainishwaji wa mkataba huo.

"Baada ya majadiliano ya muda mrefu hatimaye Katumbi amekubali kumwachia Samatta hivyo ataondoka leo usiku kwenda Ubelgiji kumalizana nao kabisa. Akimaliza atarejea nchini kwa ajili ya maandalizi yake ya kwenda kuitumikia klabu hiyo mwezi ujao," alisema mtu wa karibu wa Samatta.

Jana Meneja wake, Jamal Kasongo alisema kuwa walikuwa na kikao na serikali pamoja na mwanasheria wao kikao ambacho kinaonyesha kuzaa matunda
 
Sijapenda hii ya serikali kuingilia kati,wangeacha Samatta amalizane na klabu yake kiroho safi badala ya wao kuingilia kati name kuishinikiza TP Mazembe kumuachia huru Samatta, bila TP Mazembe Samatta asingejulikana, hivyo klabu yake ina haki zote juu yake kwavile mkataba wake haujamalizika bado,kwa tabia hii ya serikali kuingilia mambo yasiyowahusu watasababisha wachezaji wengine wa Tanzania wasichukuliwe na klabu hiyo

I don't buy your argument, sasa ulitaka serikali ikae kimya tu kipaji kinaoza Congo kisa wachezaji wengine hawataitwa TP Mazembe? Bila TP Mazembe Samata asingejulikana, okay, mbona uongeu juhudi zake binafsi walizoziona mpaka wakampa gwanda? Mbona uongei jinsi gani ameisaidia klabu hiyo kwenye mashandano mbalimbali. Fikiria kabla hujaongea, Samata sio mchezaji wa kwanza kuvunja mkataba na klabu yake. Ndio maana ukaitwa mkataba, ndani yake kuna maelezo mengi tu kwahiyo TP Mazembe watafaidika na Samata anaendelea na maisha yake.
Au wewe umetoka Congo nini?
 
Simzungumzii Samatta,nafahamu kwamba Samatta ana haki zote za kuamua kama aachane na klabu yake ya sasa au aende klabu nyingine.Mimi naizungumzia hii serikali inayopenda kuingilia mambo yasiyoihusu,yenyewe yadhani inamsaidia Samatta just for now lkn kumbe wanawaharibia wachezaji wengine in the near future, bado nasisitiza kwamba suala la uhamisho wa wachezaji ni juu ya wachezaji husika kumalizana na klabu zao na si jukumu la serikali kuingilia.Ulishawahi kuwahi kusikia wapi serikali za nchi kuingilia masuala ya uhamisho ya wachezaji ktk klabu wanazotumikia?This is the first time,klabu inapomnunua mchezaji huwa inakuwa na malengo naye flani,ndio maana klabu kama Barcelona imetangaza wazai kwamba haina mpango wa kuwauza akina Messi na Neymar, hiyo ni mipango yao na hao wachezaji na hakuna atakayewaingilia.

Hivi suala hasheem thebeet hakuna maali serikali iliingilia kati
 
Mjomba unachanganya mambo, sasa unachanganya Messi kwa Barcelona na Samata kwa TP Mazembe. Messi pale alipo anaishi kwenye ndoto zake wakati Samata still searching for them. Nikuulize swali, wewe ukiwa kwenye matatizo ya kikazi na mwajili wako nje ya nchi, serikali aipaswi kukupa msaada? Ni sawa na samata, anahaki ya kupata msaada kutoka kwa serikali pale inapobidi. Au Messi akipata matatizo nje ya Argentina, hawezi kupewa msaada na serikali ya Argentina kwasababu ni mcheza mpira. Nani anapaswa na nani hapaswi kupewa msaada na serikali? Kitu gani kinachokufanya ufikiri swala la Samata kama raia wa Tanzania serikali aliwahusu? Bora unyamaze kwasababu huna hoja. Tena usiendelee kuniudhi nataka kuangalia game sasa
 
Sijapenda hii ya serikali kuingilia kati,wangeacha Samatta amalizane na klabu yake kiroho safi badala ya wao kuingilia kati name kuishinikiza TP Mazembe kumuachia huru Samatta, bila TP Mazembe Samatta asingejulikana, hivyo klabu yake ina haki zote juu yake kwavile mkataba wake haujamalizika bado,kwa tabia hii ya serikali kuingilia mambo yasiyowahusu watasababisha wachezaji wengine wa Tanzania wasichukuliwe na klabu hiyo
jamaa anaweza kumweka benchi Ulimwengu forever
 
Sijapenda hii ya serikali kuingilia kati,wangeacha Samatta amalizane na klabu yake kiroho safi badala ya wao kuingilia kati name kuishinikiza TP Mazembe kumuachia huru Samatta, bila TP Mazembe Samatta asingejulikana, hivyo klabu yake ina haki zote juu yake kwavile mkataba wake haujamalizika bado,kwa tabia hii ya serikali kuingilia mambo yasiyowahusu watasababisha wachezaji wengine wa Tanzania wasichukuliwe na klabu hiyo
jinga sana wewe
ama kweri watanzania hatutaendelea tukiwa na watu wenye mawazo finyu kama wewe
 
Back
Top Bottom