Elections 2010 Katu Kikwete Hakushinda 2010 nani anabisha?

Magulumangu

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
3,047
452
Ukweli jamani upo pale pale kuwa Mkwere 2010 hakushinda, na dhambi ya wizi daima watz tutaona matokeo yake........
 
Na dhambi hii itamtesa daima, hatatoa speech katka baadhi ya matukio muhimu na muda mwingi atakua nje ya nchi na hata pale atakapolazimika kutoa maamuzi basi atatoa kwa maslahi ya mafisadi wenzie!!!
 
ALIFANYA MAPINDUZI YA KIJESHI NAMSHAURI DR SLAA APELEKE VIELELEZO ICC WATAMSIKILIZA NA HIYO NDIO ITAKUWA NJIA YA UKOMBOZI.

Kwa faida ya wale ambao hawakuipata TAARIFA KAMILI YA CHADEMA
Najua kuna wengi huenda hawakuipata hii. Nimeitafuta sijaiona jamvini baada ya rafiki kuniambia niitafute. Ila nimeikuta feacebook yake. Wanaoitafuta kama mimi, hii hapa

Msimamo wa Chadema haujabadilika

by Dr. Wilbrod Slaa on Tuesday, December 14, 2010 at 7:29pm

Kuna taarifa ambazo zimekuwa zikiandikwa na kuripotiwa na vyombo vya habari ambavyo zinaashiria kuwa Chadema tumebadili msimamo wetu kuhusu masuala ya uchaguzi.

Hakuna mahali popote Chadema imebadili msimamo wake na kusema kuwa Kura hazijaibiwa au kuchakachuliwa. Taarifa niliyotoa jana kwa TBC ilieleza wazi kuwa Kamati Kuu, ilipokea na kujadili na kuridhia mapendekezo yote yaliyowasilishwa na Sekretariat ya Chama kuwa Chadema imekataa matokeo ya Uchaguzi kutokana na irregularities 15. Chadema inaamini kuwa iwapo Katiba ya nchi isingelikuwa imezuia kuhoji matokeo ya uchaguzi Mkuu wa Rais mahakamani, matokeo hayo yangeliweza kubatilishwa. Kwa vile Katiba inakataza kuhoji matokeo kuhojiwa mahakamani, basi japo Kikwete's Presidency ni Lawful it is Illegitimate.

Chadema ilitumia maneno ya kiingereza kuonyesha tofuati kubwa kati ya maneno hayo mawili. Huo ndio msimamo wa Chadema toka mwanzo na haijawahi kuyumba, japo maneno ya kiswahili yamekuwa yakipewa tafsiri tofauti na watu mbalimbali. Ni kwa msingi huo, Kamati Kuu ikasisitiza " Kuundwa kwa Tume Huru" kuchunguza Dosari " Irregularities" hizo kubwa katika uchaguzi. Nasisitiza, Chadema ni Chama ambacho toka mwanzo ilisisitiza kuwa "Haiko Tayari kuingia Ikulu kwa kumwaga Damu ya Watanzania".

Inawezekana wanaopenda na kufurahia vurugu, Chadema haiko tayari kwa hali hiyo. Tunasukumwa sana na wapenzi na wanachame wetu kutoka mitaani na kuandamana, na ndicho pia wanachotaka ndugu zetu akina Mwanakijiji. Maandamano, (ya amani au ya kushinikiza), kwa watu wanaojua mchakato wa demokrasia ni hatua ya mwisho kabisa baada ya njia zingine zote kushindikana. Pili, ili Tanzania isiingie katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015 kwa Katiba na Sheria mbovu kama tuliyonayo leo, Chadema inasisitiza upatikanaji wa Katiba mpya, Shirikishi na ya Wananchi.

Upatakanaji wa Katiba hii utakuwa na mchakato, na kama Serikali haitaki, basi Chadema kwa kushirikiana na wadau na watu mbalimbali wakiwemo wananchi itatutumia njia zote zinazoweza kuipatia nchi Katiba ya Wananchi. Yote haya ni mchakato, na kwa mtu yeyote anayoamini kuwa mchakato huchukua muda, basi atakuwa mvumilivu. Hakuna sababu ya kutumia lugha kali, kukashifiana na kutukanana japo jamvi letu ni mahali ambapo "we dare to speak". Tukivumiliana na kuheshimiana tutafika salama bandarini.

Tukikurupuka tunaweza pia tusifikie lengo tunalotaka. Hekima na busara vikitawala na kuongoza matunda yatakuwa mazuri kwa Taifa letu. Taifa ni letu tukilibomoa hatuna pengine pa kwenda, labda tukiamua kulowea penginepo. Tukikurupuka tunaweza kuwaumiza wanaohusika na wasiohusika. Uvumilivu na Busara daima huvuta heri.

Source: Gonga hapa Msimamo wa Chadema haujabadilika | Facebook

NYONGEZA: Kuna thread imewekwa hapa chini na Mwanajamii mmoja (Chapakazi) anauliza tofauti ya maneno haya mawili (Lawful na Legitimate). Kwa uelewa wangu. Naomba niiongeze hapa kwa mtiririko sahihi. Unaweza toa usahihi zaidi

Moja ya tafsiri za legitimate zilizoko kwenye link hii define: legitimate - Google Search

Zinasema kitu
legitimate ni kile ambacho kiko affirmed to be just na in accordance with recognized or accepted standards or principles.

Na kitu
lawful ni kitu ambacho kiko recognized or sanctioned by law(lawful: meaning and definitions — Infoplease.com.

Kwa upeo wangu hii inamanishaa kitu kinaweza kuwa recognize na sheria lakini kisiwe just kwa sababu hakikiendana na accepted principles

Tukitumia mfano wa tukio lenyewe naweza kusema hivi,

Sheria inasema Raisi ni Raisi kwa kutangazwa na tume (lawful) lakini ili atangazwe lazima kanuni (principle) kadhaa zifuatwe.

Hivyo kama kanuni hazikufuatwa lakini katangazwa (kama sheria inavyotaka) na tume ya uchaguzi basi ni lawful kwa sababu katangazwa kisheria na tume yenye mamlaka ya kisheria kutangaza lakini kama kanuni za kufuatwa ili atangazwe zimevunjwa tunasema ni illegitimate kwa sababu principle s zimekiukwa.

Kwa msaada zaidi gonga hili link uone mfano kule Georgia

http://georgiandaily.com/index.php?o...2829&Itemid=68
 
Mheshimiwa Kikwete alishinda tena alishinda kirahisi sana,naelewa kuwa mnaishabikia Chadema,inawezekana kabisa hamna hata shahada ya kupigia kura seuze kujiandikisha ,hivyo mpo sawa na wale ambao wakienda kwenye mikutano kwa wingi na kujenga tamaa kwa viongozi wa Chadema kuwa wanakura nyingi .kumbe ni washangiliaji tu.
 
Upotoshwaji umekuwa mkubwa sana hasa kupitia gazeti kichefuchefu la serikali na baadhi ya magazeti ya watuhumiwa wa ufisadi. Tunashukuru kusikia msimamo huo wa CDM na ningeomba CDM wangejitokeza mbele ya vyombo kueleza na kuweka wazi msimamo wao huo ili hata wale wasio na fursa ya kuingia kwenye mtandao kama JF na Facebook wajuzwe msimamo wa CDM sasa ukoje

Naomba kuwasilisha.
Kila la lheri na jema kwake Dr Slaa.
 
Mheshimiwa Kikwete alishinda tena alishinda kirahisi sana,naelewa kuwa mnaishabikia Chadema,inawezekana kabisa hamna hata shahada ya kupigia kura seuze kujiandikisha ,hivyo mpo sawa na wale ambao wakienda kwenye mikutano kwa wingi na kujenga tamaa kwa viongozi wa Chadema kuwa wanakura nyingi .kumbe ni washangiliaji tu.
weka data to support your statement!
 
Na dhambi hii itamtesa daima, hatatoa speech katka baadhi ya matukio muhimu na muda mwingi atakua nje ya nchi na hata pale atakapolazimika kutoa maamuzi basi atatoa kwa maslahi ya mafisadi wenzie!!!
this is typical udaku. Shame on you.
 
Na dhambi hii itamtesa daima, hatatoa speech katka baadhi ya matukio muhimu na muda mwingi atakua nje ya nchi na hata pale atakapolazimika kutoa maamuzi basi atatoa kwa maslahi ya mafisadi wenzie!!!

Mkuu umetisha. Utabiri wako umetimia
 
Mheshimiwa Kikwete alishinda tena alishinda kirahisi sana,naelewa kuwa mnaishabikia Chadema,inawezekana kabisa hamna hata shahada ya kupigia kura seuze kujiandikisha ,hivyo mpo sawa na wale ambao wakienda kwenye mikutano kwa wingi na kujenga tamaa kwa viongozi wa Chadema kuwa wanakura nyingi .kumbe ni washangiliaji tu.

JK ni rais wa NEC ,TISS na MAFISADI.
:car:
 
Na dhambi hii itamtesa daima, hatatoa speech katka baadhi ya matukio muhimu na muda mwingi atakua nje ya nchi na hata pale atakapolazimika kutoa maamuzi basi atatoa kwa maslahi ya mafisadi wenzie!!!

Tutaona tu na bado, ngoja tu mambo yazidi mkuu...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom