Katoliki: CCM wajihoji kumpoteza Dk Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katoliki: CCM wajihoji kumpoteza Dk Slaa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by fangfangjt, Mar 19, 2011.

 1. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  Katoliki: CCM wajihoji kumpoteza Dk Slaa

  Israel Mgussi, Dodoma
  RAIS wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Mkuu Yuda Thadeus Ruwa'ichi amewaponda wanasiasa wanaotaka kuwafumba mdomo viongozi wa dini nchini wanaokemea rushwa, ufisadi na ukiukwaji wa maadili unaofanywa na baadhi ya viongozi waandamizi wa Serikali na vyama vya siasa.Ruwai'chi ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki, Mwanza pia amewajia juu wanaolihusisha kanisa hilo na ustawi wa Chadema akisema kuwa huo ni uzushi na kuwanyooshea kidole baadhi ya wanaCCM na baadhi ya waandishi wa habari aliosema hawapendi kuchanganua mambo na kuwa na uhakika nayo.

  Askofu Ruwai`chi (pichani) alisema Kanisa Katoliki halikiteulii chama chochote cha siasa mgombea na akakipa angalizo CCM akitaka kijidodose juu ya sababu zilizomfanya Dk Willbrod Slaa kukihama na sasa kuonekana kama ni mtu anayekichanganya akili na kutaka iache alichokiita propaganda zenye malengo ya kuwagawa watu katika misingi ya dini.

  “Kama Slaa (Dk Willbroad Slaa) alikuwa mwanaCCM akaikimbia. Sasa jifunzeni na kukumbuka historia, CCM wana mchango gani katika hilo la Dk Slaa kuikimbia, wakijibu swali hilo itakuwa vizuri sana," alisema akisisitiza.Askofu Ruwai'chi alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Parokia ya Kibaigwa, Dodoma muda mfupi baada ya kumpokea Askofu mteule wa Jimbo Katoliki la Dodoma, Mhashamu Gervas Nyaisonga ambaye atasimikwa rasmi leo mjini Dodoma.

  Kuhusu Kanisa Katoliki kudaiwa kuwa limekuwa likikiunga mkono Chadema, Askofu Ruwai'chi alisema kuwa hakuna ukweli wowote kuhusu uvumi huo na kwamba kauli hizo zimekuzwa na baadhi ya wanaCCM ambao wamekosa sera na kukurupuka kutoa kauli zisizo za msingi.

  “Hizo ni kauli danganya toto, Kanisa halina chama, ila likibidi kuzungumza litazungumza kama lilivyokuwa likifanya kwa maslahi ya watu wote. Viongozi wa dini wasipozungumza watakuwa hawalitendei haki taifa, wanapaswa kusimamia haki pale inapoonekana kupotoshwa, kanisa halina chama," alisema Askofu huyo.Alisema Chadema ni chama chenye mkusanyiko wa watu wa dini na madhehebu yote, hivyo watu watumie akili zao kutafuta ukweli wa uvumi huo aliosema ni wa kupotosha.

  Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki nchini alisema kila mtu ana wajibu wa kuhakikisha kwamba Tanzania inakuwa njema. Akaeleza kushangazwa kwake na wachache wanaotaka kupandikiza mbegu ya udini ambayo alisema kimsingi haipo nchini.

  Alisema kauli kama hizo alizoziita za kichochezi pia zinajenga swali kuwa, huenda CCM ni chama cha watu fulani, lakini akasema kuwa wao viongozi wa dini na kanisa kwa ujumla kazi yao ni kuhakikisha maslahi ya taifa hayachezewi wala hayaendi kiholela, akisisitiza kuwa ni haki ya kila mtu kuwa na mtazamo tofauti wa kisiasa muhimu asivunje sheria.

  Huku akisisitiza kuwa Tanzania haiendeshwi katika misingi ya falsafa za kidini wala madhehebu, Askofu Ruwai'chi alisema kuwa viongozi wa dini zote nchini wanapaswa kuzungumza na kukemea dosari za kiutendaji na kiuwajibikaji zinazofanywa na baadhi ya viongozi na watumishi wa umma na kwamba bila hivyo itakuwa ni kutowatendea haki Watanzania.

  Alisema viongozi wa dini wanapaswa kuzungumzia matatizo yaliopo nchini, kuhamasisha haki, ukweli, amani na kushughulikia maendeleo ya watu wote bila kuogopa wanaowabeza na kutaka kuwaziba midomo kwa kisingizio kuwa wanaingilia Serikali.

  “Kuzungumza siyo kuingilia, viongozi wa dini wana wajibu wa kutoa kauli na kuwashuhudia watu mambo mbalimbali yanayotokea katika nchi, wasipoongea watakuwa hawalitendei haki Taifa,” alisema Askofu Mkuu Ruwai'chi.

  Askofu Ruwaichi alisema kuwa viongozi wa dini mbali na kutunza dini, lakini wana wajibu mkubwa wa kusimamia mustakabali wa taifa kwa kuhakikisha wanakemea na kusemea mienendo ya kiovu ambayo kwa namna moja au nyingine, inaweza kuvuruga amani na umoja wa kitaifa.

  Askofu mteule Nyaisonga atasimikwa leo katika Kanisa Kuu la Paulo wa Msalaba Mjini Dodoma na Rais Jakaya Kikwete pamoja na Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na viongozi wengine wa dini na madhehebu mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria.

  Juzi, mamia waumini wa Kanisa katoliki walijitokeza na kuandamana kwa ajili ya mapokezi ya askofu huyo mteule aliyewasili majira ya saa 7:00 mchana Kibaigwa, Dodoma akitokea Mbeya ambako alikuwa akitumika katika shughuli za kitume akiwa Padri Daraja la Pili.
   
 2. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2011
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Hawathubutu kujihoji kwa sababu maadili yameishapotea na sasa wanajivunia ubabe.
   
 3. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Too late now, kumeshakucha tayari shuka halina umuhimu tena.
   
 4. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2011
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Sawa kabisa, hawa ccm now wanatafuta pakujishika, matawi ya mti waliojishikilia yamechengwa yote! Sasa sehemu pekee ya kutokea ni kuhubiri mambo ya udini na ukabila ambayo ni nadharia tu na ni kwa faida zao za kisiasa!
   
 5. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Saturday, 19 March 2011 09:37

  RAIS wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Mkuu Yuda Thadeus Ruwa'ichi amewaponda wanasiasa wanaotaka kuwafumba mdomo viongozi wa dini nchini wanaokemea rushwa, ufisadi na ukiukwaji wa maadili unaofanywa na baadhi ya viongozi waandamizi wa Serikali na vyama vya siasa.Ruwai'chi ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki, Mwanza pia amewajia juu wanaolihusisha kanisa hilo na ustawi wa Chadema akisema kuwa huo ni uzushi na kuwanyooshea kidole baadhi ya wanaCCM na baadhi ya waandishi wa habari aliosema hawapendi kuchanganua mambo na kuwa na uhakika nayo.

  Askofu Ruwai`chi (pichani) alisema Kanisa Katoliki halikiteulii chama chochote cha siasa mgombea na akakipa angalizo CCM akitaka kijidodose juu ya sababu zilizomfanya Dk Willbrod Slaa kukihama na sasa kuonekana kama ni mtu anayekichanganya akili na kutaka iache alichokiita propaganda zenye malengo ya kuwagawa watu katika misingi ya dini.

  “Kama Slaa (Dk Willbroad Slaa) alikuwa mwanaCCM akaikimbia. Sasa jifunzeni na kukumbuka historia, CCM wana mchango gani katika hilo la Dk Slaa kuikimbia, wakijibu swali hilo itakuwa vizuri sana," alisema akisisitiza.Askofu Ruwai'chi alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Parokia ya Kibaigwa, Dodoma muda mfupi baada ya kumpokea Askofu mteule wa Jimbo Katoliki la Dodoma, Mhashamu Gervas Nyaisonga ambaye atasimikwa rasmi leo mjini Dodoma.

  Kuhusu Kanisa Katoliki kudaiwa kuwa limekuwa likikiunga mkono Chadema, Askofu Ruwai'chi alisema kuwa hakuna ukweli wowote kuhusu uvumi huo na kwamba kauli hizo zimekuzwa na baadhi ya wanaCCM ambao wamekosa sera na kukurupuka kutoa kauli zisizo za msingi.

  “Hizo ni kauli danganya toto, Kanisa halina chama, ila likibidi kuzungumza litazungumza kama lilivyokuwa likifanya kwa maslahi ya watu wote. Viongozi wa dini wasipozungumza watakuwa hawalitendei haki taifa, wanapaswa kusimamia haki pale inapoonekana kupotoshwa, kanisa halina chama," alisema Askofu huyo.Alisema Chadema ni chama chenye mkusanyiko wa watu wa dini na madhehebu yote, hivyo watu watumie akili zao kutafuta ukweli wa uvumi huo aliosema ni wa kupotosha.

  Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki nchini alisema kila mtu ana wajibu wa kuhakikisha kwamba Tanzania inakuwa njema. Akaeleza kushangazwa kwake na wachache wanaotaka kupandikiza mbegu ya udini ambayo alisema kimsingi haipo nchini.

  Alisema kauli kama hizo alizoziita za kichochezi pia zinajenga swali kuwa, huenda CCM ni chama cha watu fulani, lakini akasema kuwa wao viongozi wa dini na kanisa kwa ujumla kazi yao ni kuhakikisha maslahi ya taifa hayachezewi wala hayaendi kiholela, akisisitiza kuwa ni haki ya kila mtu kuwa na mtazamo tofauti wa kisiasa muhimu asivunje sheria.
  Huku akisisitiza kuwa Tanzania haiendeshwi katika misingi ya falsafa za kidini wala madhehebu, Askofu Ruwai'chi alisema kuwa viongozi wa dini zote nchini wanapaswa kuzungumza na kukemea dosari za kiutendaji na kiuwajibikaji zinazofanywa na baadhi ya viongozi na watumishi wa umma na kwamba bila hivyo itakuwa ni kutowatendea haki Watanzania.

  Alisema viongozi wa dini wanapaswa kuzungumzia matatizo yaliopo nchini, kuhamasisha haki, ukweli, amani na kushughulikia maendeleo ya watu wote bila kuogopa wanaowabeza na kutaka kuwaziba midomo kwa kisingizio kuwa wanaingilia Serikali.

  “Kuzungumza siyo kuingilia, viongozi wa dini wana wajibu wa kutoa kauli na kuwashuhudia watu mambo mbalimbali yanayotokea katika nchi, wasipoongea watakuwa hawalitendei haki Taifa,” alisema Askofu Mkuu Ruwai'chi.
  Askofu Ruwaichi alisema kuwa viongozi wa dini mbali na kutunza dini, lakini wana wajibu mkubwa wa kusimamia mustakabali wa taifa kwa kuhakikisha wanakemea na kusemea mienendo ya kiovu ambayo kwa namna moja au nyingine, inaweza kuvuruga amani na umoja wa kitaifa.

  Askofu mteule Nyaisonga atasimikwa leo katika Kanisa Kuu la Paulo wa Msalaba Mjini Dodoma na Rais Jakaya Kikwete pamoja na Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na viongozi wengine wa dini na madhehebu mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria.
  Juzi, mamia waumini wa Kanisa katoliki walijitokeza na kuandamana kwa ajili ya mapokezi ya askofu huyo mteule aliyewasili majira ya saa 7:00 mchana Kibaigwa, Dodoma akitokea Mbeya ambako alikuwa akitumika katika shughuli za kitume akiwa Padri Daraja la Pili.
   
 6. Unyanga

  Unyanga JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2011
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 402
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Anawponda ccm kisha hao hao viongozi wa CCM wamealikwa na kanisa kwenda shughuli hizo ni ajabu sana. Mi nafikiri ili kuwaonyesha ya kwamba hampendezwi na wanayoyafanya ingekuwa ni bora kuwatenga kabisa mpaka kwenye shughuli zenu ili kuonyesha ya kwamba mnachukizwa na yanayofanywa na viongozi hao. Kuhusu hili la chadema na kanisa katoliki itapendeza kama wote tutazungumza kwa lugha moja
   
 7. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Ndugu wasikosolewe??
  kumkosoa mtu anapokosea si kuwa unamponda na kumbuka akupendaye anakukosoa unapokosea tatizo la ccm wanapenda kusifiwa hata wanapokosea!:juggle:
   
 8. boss80

  boss80 Member

  #8
  Mar 19, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15

  Huu nao ni ufinyu wa mawazo, kwani kuwakaribisha kunahusiana vp na mada hii, hilo ndo tatizo lenu la kuongelea watu, yeye hajata mtu, sasa kinachokuuma ni nini hapo? Au mesikia amewakaribisha ccm? japo hata kama angewakaribisha sioni tatizo. na najua mahubiri ya leo balaa tena naomba ahubiri Pengo uone mziki wake.
   
 9. M

  Mkandara Verified User

  #9
  Mar 19, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mtanisamehe sana wakuu zangu lakini nitasema ukweli ingawa utawaudhi sana waumini wanaoamini watu na sio dini zao..

  Nawaomba wana JF kujihadhali sana na tungo za viongozi wadini iwe kutoka upande wowote wa dini zetu wanapozungumzia Udini wakivihusisha vyama CCM na CDM au uongozi wake...

  Hawa wengi wao kama sii wote ni wanafiki wakubwa wanaotumia dini zetu kama daraja la kujenga Udini wakitumiwa na vyombo vya dola baada ya kupokea vibahasha..

  Na mchezo huu haukuanza jana, nakumbuka mwaka 1995 chama cha CUF kilituhumiwa kuwa chama cha Kiislaam na madhara yake tumeyaona... Ni kwa mkono wa CCM, walisimama watu na majoho yao kutangazia wananchi kwamba CUF ni chama cha kidini na inapokea misaada toka nchi za kiarabu kuipindua serikali na tukaonyweshwa mapanga na baadhi ya silaha duni kabisa, watu wakaaminishwa misikitini hadi makanisani..

  Nakumbuka hata Sheikh mmoja alijitokeza na kusema Kighoma Malima na Sheikh Kassim bin Jumaa walikutana kupanga mbinu za kulihujumu taifa ili hali Sheikh Kassim hakuwa nasi duniani muda alotuhumiwa..

  Mchezo mzima ulotumika kuuivunja CUF ndio leo unatumika tena kuivunja Chadema wakitumiwa viongozi wadini kukemea ufisadi hali hawa hawa viongozi wamekuwa mstari wa mbele kutetea ufisadi wao wenyewe ktk maswala yanayohusu misikiti na makanisa...

  Kama kweli waislaam waanamini Waislaam wamekuwa wakionewa toka tupate uhuru na kwamba CCM imekuwa ikio gozwa na kanisa Katoliki, iweje leo mtu kama Dr.Slaa anayeiipiga vita ndiye aitwe mdini wakati hajatawala hata saa moja acha siku, mwaka au awamu moja?

  Iwaje CCM inayodaiwa kwa mabaya yoote yaliyotokea Zanzibar na bara iwe na unafuu fulani anapotawala kiongozi Muislaam au Mkristu hali matukio mengi ya ubaya wa chama hiki yamekuwepo muda woote?

  Binafsi sijawahi kusikia mtu akisifia wakati fulani kulingana na dini ya kiongozi na hawa hawa viongozi wa dini huyaona makosa tu pale wanapoguswa wao na wepesi sana wa kusifia au kuponda kulingana na maslahi yao wenyewe.

  Ndugu zangu tujihadhalini sana na siasa za maji taka.. Viongozi wa dini watakemea Ufisadi kwa kufuata vitabu na mafundisho yake lakini sii kuzua Udini hali ni nyie mlotwambia kwamba JK ni chaguo la Mungu na mnamkaribisha ktk kila sherehe zenu kubwa kubwa..

  Hivi kweli mchungaji mwenye imani kubwa utamkaribisha fisadi tena Muislaam ktk sherehe kubwa ya kiimani? Mtakubali michango yake hali mkijua fedha hizo ni za kifisadi?..

  Na mwisho ni kipi hasa kinachowavutia nyie na Dr.Slaa au CDM ikiwa chama hiki hakijatawala hata siku moka? Kwanini isiwe viongozi wa CUF,NCCR au TLP ila CDM ambayo hamuwafahamu vizuri viongozi wake zaidi ya kwamba Dr.Slaa aliyefukuzwa Upadre, leo mnajaribu kumpamba ili iwe nini? - kama sii kuchonganisha vichwa vya wananchi ktk imani zao?

  Nina hakika kabisa nia na malengo yenu ni kuwa, waumini wa kiislaam wanaposoma habari kama hizi ndio wazidi kumchukia dr.Slaa na chama CDM pasipo kufikiria adha walizozipata nyuma chini ya CCM.

  Na maajabu ya Mussa chama kama CUF kimekubali kushindwa na mwisho wake kuungana na CCM pamoja na imani yao kubwa kwamba CCM ni chama cha kanisa Katoliki lakini bora wao kuliko CDM inayopigiwa debe moja kwa moja na makanisa..

  Mapadre na Masheikh fanyeni kazi mlotumwa kuifanya, nayo ni kufundisha dini na kukataza mabaya kwa kuonyesha mifano na sii kupokea michango ya kina Rostam, Lowasa, JK na viongozi wengineo ndani ya CCM kisha mnatuambia wao ndio mafisadi...Iacheni Chadema na viongozi wake kuwa sababu yenu kukemea Ufisadi, onyesheni mifano nyie wenyewe..
  Viongozi ha wa wapo kwenye payr
   
 10. L

  LAT JF-Expert Member

  #10
  Mar 19, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0

  bandiko lako ni la kinafiki na lisilo na mantiki yeyote ....
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  Mar 19, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  ndio maana yake! Nimekugusa panapouma...
   
 12. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #12
  Mar 19, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Mimi nilidhani Pengo tu ndiye msemaji wa CHADEMA kumbe hivi sasa wamefanikiwa kuinunua TEC yote? hongera CHADEMA.
   
 13. L

  LAT JF-Expert Member

  #13
  Mar 19, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  nashukuru kwa kukiri kuwa mnafiki .... umeonyesha busara nyingi na ukomavu wa undumilakuwili
   
 14. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #14
  Mar 19, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu! Kama ulifundishwa hivyo Madrassa walimu wako walikupotosha. Sisi tunasema yeye aliye dhaifu tunauungana nae na atuwezi kumtenga mtu yoyote kisa yeye ni fisadi au ana tuhuma mbalimbali.
  '
  Kama Yesu angekuja duniani kwa ubaguzi hivi ni nani agentarajia kuuona ufalme wa mbingu.

  Mkuu usiwe na chuki na kiburi mpaka unafikia kuwatenga wenzako, hao mafisadi ni wenzetu yatupasa kuwaambia kweli ili kweli iwaweke huru.
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Mar 19, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  kwa elimu yako ya ufahamu huwezi kunielewa kwani hujui hata maana ya neno dogo kama Unafiki.. Labda kamusi itakusaidia ukisoma neno kwa neno...
   
 16. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #16
  Mar 19, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Jamani jaribuni kuchagua Avatar ambazo haziwezi kupunguza heshima zenu, maana heshima ya mtu humu ni vitu viwili; Mchango wake na pia aina ya Avatar inaweza kuleta picha na taswira ya mtu, maana avatar nayo inaongea.

  Ukiweka Avatar ambayo inaleta taswira kama shoga alafu pia unachnagia kama shoga, unaweza kuwapa watu picha kuwa wewe ni shoga ingawa ukweli unaujua wewe mwenyewe. Samahani kwa yoyote niliye mkwaza lakini kama kuna mtu anaweza kuhisi ni yeye anaweza kufikiri kujirekebesha kama hafanyi maksudi.

  Nimejaribu kusoma hiyo thread mara dufu, sijajua Pengo anaigiaje katika kujadili hii thread, hata kama ndio uwezo finyu sitegemi iwe kiasi hiki
   
 17. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #17
  Mar 19, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hakuna hoja hapa. It is one sided. mambo siku zote hubadilika na wakati, muktadha, na hadhira. Viongozi wa dini kemea ufisadi kwa nguvu zote bula kujali nani inamuuma; wala wa dini gani; na wanaohusisha kukemia kwenu na udini ni mufilisi kwa kimawazo.
   
 18. Criss

  Criss JF-Expert Member

  #18
  Mar 19, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 825
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwa hatua tulioifikia Tanzania binafsi naamini siku na saa ya ukombozi haiko mbali kutimia ,kitu kinachonifanya niamini kua nchi hii itapata " UKOMBOZI "wa kipekee bila hata watu kuingia barabarani ni kwa jinsi hawa jamaa wanavyo weweseka na kivuri na si kitu husika .Hii itapelekea mwisho wa siku wajikute wamebaki wenyewe na ccm yao.Kwa hali ilivyo naamini Tanzania hakuna UDINI wakiwango kinacho zungumziwa zaidi ya UTAIFA tunao utetea.Ushauri wangu wanaharakati tuendelee kuitetea nchi yetu bila kuogopa chochote.
   
 19. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #19
  Mar 19, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ndugu yangu, mafunzo ya biblia yanasema kuwa mpende adui wako, Na "Yesu alikuja kwa ajili ya wenye dhambi" Hawa viongozi wanasimamia misingi hiyo kwa vitendo. Uelewe tu kuwa kualika viongozi mafisadi wa CCM katika shughuli za kiroho ni kutimiza wajibu wao.
  Back to mataifa "Keep your friend close, your enemy closer" Don Corleone(Mario Puzo's Godfather)
   
 20. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #20
  Mar 19, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280

  Kwa hiyo CCM na akina Pengo etal wana uadui?
   
Loading...