Katoka sultani mwarabu waingia usultani wa mtu mweusi zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katoka sultani mwarabu waingia usultani wa mtu mweusi zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbunge, Jul 30, 2009.

 1. M

  Mbunge Senior Member

  #1
  Jul 30, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HALI ilivyo ni kuwa upo uwezekano mkubwa chini ya CCM Zanzibar isiyo na mwelekeo wala visheni ya kule visiwa vinavyokotakiwa kuwa baada ya 2015....sasa wanazua jambo juu ya jambo.

  Nalo sio jingine ila lile la uwezekano wa kuwa na the Karume aristocracy in Zanzibar. Hivi tunahitaji tena uongozi wa kina Karume kweli visiwani. Na akingia Hali hii basi itakuja Hali ya Wajukuu wa Mzee Abedi nao kuwa maraisi na vitukuu wao na hili ndio sera ya serikali ya mapinduzi.

  Wazanzibari wenzangu, ndugu zangu, wandani wangu haiwezekani kuwa na demokrasia ya kweli visiwani kwa sababu kwanza kuna kitu haramu ambacho kiko katika katiba. Nacho sio kingine ila ni kile kinachoitwa Baraza la Mapinduzi.

  Bila baraza hilo kufutwa kikatiba sio rahisi kwa ujinga tuliokuwa nao Zanzibari kuhimili vishindo vya kushinikizwa na bara na viongozi wa visiwani wasiokuwa na sifa wala uwezo wa uongozi kuwa ndio viongozi wetu. Hili linafanyika wakati nusu ya Wazanzibari wenye uwezo wa uongozi mara 10 ya uwezo wa kina Karume wanatengwa kisiasa chini ya huruma, ulinzi na rehema ya CCM bara.
   
 2. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #2
  Jul 30, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Kiongozi akiingia madarakani,watu wanataka kuona utendaji kazi wake. Kama ameingia kwa Demokrasia au kwa Mapinduzi;kama ana matatizo yoyote kama ana ugonjwa wa moyo,au matatizo yoyote ya mahusiano,watu hawajui hayo. Wao wanategemea mambo fulani kutoka kwa Rais wao,kutoka kwa mtu yeyote anayeitwa "Rais''. Kama akishindwa kutekeleza kwa sababu yoyote,watu watakuwa disappointed. If there is a problem,the President must step down.


  ''Some[Presidents] are well prepared, some are not; some
  have enormous advantages, others have few; some seek the office, others
  have it thrust on them. Often, however, expectations of performance are
  uniform''
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu si wanasema ana haki ya kuchukua fomu?
  Kwa hiyo akigombea na akapitishwa na wajumbe wa halmashauri kuu watakuwa wameamua wao wajumbe.
   
 4. C

  Chakarota Member

  #4
  Jul 30, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa maoni ya wa-zenj huu Usultani mweusi unafanyika kwa baraka ya Muungano, kwani chama tawala ndio wanachagua nani anewafaa kua kibaraka chao na kumtumia kwa remote control. Sasa wanaamini kua madam CCM inataka itawale daima, katu uchaguzi huru hautofanyika. Be prepare next generation kua na raisi wa zenj chotara wa ki-arabu.
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mbunge,

  Hakika umezungumza mambo takriban matatu katika bandiko lako.

  Zanzibar hatuna tatizo kabisaaaa na akina Karume kugombea na hata kuchaguliwa kuwa viongozi kama WATAKUWA NA SIFA NA UWEZO WA KUONGOZA. Hakika Zanzibar tunataka kiongozi aliye shupavu, mwenye uwezo na sifa zote sahihi za uongozi na awe aliyechaguliwa na Wazanzibari wenyewe. Hatuna ubaguzi kwa hilo.

  Demokrasia ya kweli Zanzibar itapatikana tu kama Katiba ya Zanzibar ifanyiwe marekebisho makubwa ingawa mimi ningependa iandikwe upya ili kukidhi mahitaji na matakwa ya jamii kwa sasa. hapo ndio tutakuwa wazi kabisa katika kulichambua BMZ na muundo mzima wa Serikali, Balaza la Wawakilishi na mfumo mzima wa mahakama.

  Vile vile Znz itakuwa huru kuchagua viongozi wake bila kuingiliwa na Bara. hapo tutapata kiongozi safi, mwenye uwezo, aliye na sifa na aliye chaguo la wazanzibar.

  Kinyume cha hapo tutaendelea kuchaguliwa viongozi na Bara.

  Nasriyah.
   
 6. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Some people are just previliged and have more resources than others. Mfano tuchukulie Marekani. Bush mdogo won the presidency in large part because of his families position. He had the resources and political connects. On the other hand you might have someone like Obama who had no large capital, resources or political connections Bush had but he had other advantages which are natural charisma, a good campaign team and fund raising skills. My point being, mtu yoyote anaye taka chochote hato sita kutumia the resources they have. Wakina Karume ni kama Bush, their biggest resource is their name. So you can't blame themfor trying to use it. Kinacho takiwa ni mtu makini na mwenye uwezo wa kuongoza. So let's judge the Karumes according to their talents and skills and not by their name.
   
 7. j

  johnk Member

  #7
  Jul 30, 2009
  Joined: Apr 15, 2009
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  usishangae sana kuhusu usultan ndugu yangu kwani hata mkikwepa la Karume basi ujue la Mwishi ambaye ni waziri wa ulinzi hamuwezi kulikwepa, akishindwa kupata Karume Balozi basi jiandaeni na Mwinyi waziri mtoto wa Mzee Ali Hassani Mwinyi hii ndio Tanzania ya watu wachache kuhodhi madaraka kwa kisingizio cha kulinda serikali ya mapinduzi ya Zanzibar au kwa kulinda amani ya Tanzania wakati watu wakijenga nyumba wanazungusha kuta sasa amani ipo wapi? waende Canada waone maaana ya amani hakuna maukuta makubwa yanayozunguka nyumba ukiona kuta ujue hakuna amani
   
 8. j

  johnk Member

  #8
  Jul 30, 2009
  Joined: Apr 15, 2009
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pia la msingi la kuangalia hapa ni je huyo karume balozi ana elimu gani? anao uwezo wa kuongoza? je keshaifanyia nini Zanzibar katika maisha yake? je ni mtu mpenda maendeleo ya wana zanzibar au ni mtu anayetafuta u rais ili tu awe kwenye kumbukumbu za historia kuwa alishawahi kuwa rais wa Zanzibar? nyie wazanzibar ndo mnamjua tuambieni ili tuunganishe nguvu za kumpinga kama hafai na kumuunga mkono kama anafaa, jina au ukoo sio tatizo ni uwezo wa kiongozi tunaoungalia
   
 9. j

  johnk Member

  #9
  Jul 30, 2009
  Joined: Apr 15, 2009
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  watanzania inabidi sasa tujifunze kupambanua mambo tusifanye au kujenga hoja kwenye mtandao bila ushahidi au kufanya research kuhusu hilo jambo.
  wazanzibar mnao lalamika kuhusu karume balozi je mlifanya research mkagundua kuwa hafai kiuongozi? au tu ni kwa kuwa yeye amezaliwa na mzee karuma, na kwa kuwa babake alishawahi kuwa rais na kakake pia basi yeye hana haki ya kuwa rais? nani kasema hilo? imeandikwa wapi kwenye katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania au hata kwenye katiba ya marekani? hajaona marekani bushi baba na bushi mwana? na hamkuona Clinton mume na kidogo clinton mke naye awe rais? ni kwa kuwa katiba inampa kila mmoja haki sawa ya kugombea kuwa rais na kuchagua rais ampendaye
   
 10. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #10
  Jul 30, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Demokrasia ni pamoja na kuwa na haki kwa kila mtu anayetimiza masharti ya kugombea (Diwani, Bunge, Rais) agombee anapotaka. Na atakapojitokeza kugombea aondolewe kwa taratibu zilizowekwa, na si kusema eti hafai kwa kuwa Baba na Kaka yake wamewahi kuwa maRais.
   
 11. M

  Mtwike Senior Member

  #11
  Jul 31, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Suala la msingi, NI KIPI ALICHOIFANYIYA ZANZIBAR? ZANZIBAR! ZANZIBAR!
   
 12. T

  T_Tonga Member

  #12
  Jul 31, 2009
  Joined: Jul 24, 2007
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tatizo lako wewe hujui karume balozi huyu ameshawahi kuua kwa kurepu mtu huu na ndio maana akatoroshwa na kupewa ubalozi na kumbuka magereza imebadilishwa jina kwa nini kikaitwa chuo cha mazunzo sababu ya huyu kuua ikaonekana itakuwa soo ndio ikabadilishwa jina huyu ni muuaji alimuua mtoto wa kike pale maisara anaitwa shadia uliza uambiwe na sio kurukia tu hakuna tatizo ikiwa ukoo mmoja watakuwa wote marais poa hata wajukuu pia na weje kuwa marais lakini basi hakuna mwengine lazima wawe ni wao kisa baba alikuwa ni mmoja wa aliye pindua hujui historia ya znz lakini ujue kuna makubwa zaidi yatatokea sasa ukoo huu kazi yao ni kuua karime ni muuaji watoto wa karume ni wauaji wajukuu itakuwaje mbona nyinyi bara hamkumuunga mkono awe rais
   
 13. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #13
  Jul 31, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  tatizo kuwa zanzibar haiko huru kuchaguwa wampendae>
   
Loading...