SoC01 Katikati ya mjadala kuhusu kukubalika na kutokukubalika chanjo COVID-19

Stories of Change - 2021 Competition

MoseeYM

Senior Member
Jul 19, 2021
134
192
Nini maana ya chanjo?
Chanjo ni kitu kinachofanya kazi ya kuupa mfumo wa kinga ya mwili kuzalisha kinga ili kupambana na ugonjwa Fulani.

Chanjo hufanya kazi kwa kuufunza mfumo wa kinga kutambua/kubaini na kukabiliana na vimelea vya magonjwa vinapoingia mwilini.

Historia ya chanjo duniani ikoje?
Inadaiwa kuwa Wachina ndio walikuwa watu wa mwanzo kugundua sampuli ya chanjo katika karne ya 10, kwa kuwaweka karibu na sehemu za makovu za watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimabli ili kuwajengea kinga ya mwili.

Karne ya kumi na nane, daktari Mwingereza Edward Jenner alibaini namna ambavyo wakamua maziwa walipata ndui ya ng'ombe ambayo haikuwa hatarishi, lakini ilikuwa nadra kwao kupata ndui ya binadamu ambayo ni hatari.

Ndui (ya binadamu) ilikuwa ni ugonjwa hatari zaidi wa kuambukiza, ambao uliua mpaka 30% ya wale ambao waliuugua. Wale ambao walipona aghlabu walibaki na makovu mengi ama kupofuka. Mwaka 1796 Jenner alifanya majaribio akimtumia mvulana wa miaka minane, James Phipps. Daktari huyo alimpaka mtoto huyo majimaji kutoka kwenye kidonda cha ndui ya ng'ombe, na baada ya muda mfupi akaonesha dalili za maambukizi. Baada ya kupona kabisa ugonjwa huo, daktari Jenner alimuwekea majimaji kutoka kwenye kidonda cha ndui (ya binadamu), lakini hakupata maambukizi.

Ndui ya ng'ombe ilimjengea chanjo dhidi ya ndui ya biadamu.

Mwaka 1798, matokeo ya majaribio hayo yalichapishwa na neno la Kingereza la vaccine (chanjo) - likabuniwa kutokana na neno la Kilatini la vacca - ambalo tafsiri yake kwa kiswahili ni ng'ombe.
(Chanzo: BBC.com)

Mitazamo iliyopo kuhusu chanjo COVID-19?

Si tu Tanzania bali jamii nyingi duniani zimekuwa na mitazamo tofauti tofauti juu ya chanzo zilizofanyiwa utafiti. Lipo kundi linalokubaliana na kupokea chanjo zilizoanza kutolewa.Kundi hili linaamini kuwa uvumbuzi wa chanjo ni msaada mkubwa katika kupambana na ugonjwa huu.

Hali kadhalika upo upande usiokubaliana na chanjo zilizopo kwa sasa.Kundi hili linatoa sababu tofauti tofauti kuhusu chanjo.Sababu hizo zote zina mlengo wa kutilia shaka ufanisi wa chanjo.

Jitihada gani zinafanyika?

Zipo jitihada nyingi ambazo zimekuwa zikifanyika kuhusu kupambana na UVICO-19.Mfano wa jitihada hizo ni utoaji wa elimu ya namna ya kujikinga,Utafutaji wa chanjo na kutibu wale wanaopatikana na ugonjwa.Kufanya sala na maombi kwa Mungu,ambapo tumeona baadhi ya nchi ikiwemo Tanzania ziliwahi kutengwa siku kwaajili ya kumuomba Mungu atupiganie juu ya hili ugonjwa.

Ukweli na Udhaifu kuhusu jitihada zilizochukuliwa pamoja na mitazamo ya jamii:

Wanaokubali ukweli na udhaifu wao upoje?

Ukweli: Kundi linalokubali uwepo wa chanjo linaweza kuwa sahihi kwa mantiki ya kwamba,yapo matokeo chanya juu ya baadhi ya waliopokea chanjo kutoka nchi nyingine duniani,pasipo kujali ni kwa kiwango gani.hivyo hii yaweza kuwa na matumaini makubwa kwao kuhusu chanjo kusaidia.kwa upande mwingine Viongozi wa dini na watu waliokuwa wakifanya sala na maombi wanaweza kuangukia katika kundi hili kutokana na kuamini kwamba kupitia maombi yao Mungu ameyasikia kwa kuwapa watu wake ufahamu wa kupata chanjo ya ugonjwa.


Udhaifu: Kundi la waliowengi wanaamini kuwa kwa kupata chanjo,pengine hawatoambukizwa tena.wanasahau kwamba Ufanisi wa chanjo si wa asilimia mia moja.Hivyo hatua nyingine za tahadhari inabidi kuchukuliwa.Kwa upande mwingine ikumbukwe na tahadhali zichukuliwe na nchi husika kwa kuwa Mataifa yanayozalisha chanjo hizi yanaweza kuwa na mlengo wa 'kibiashara' zaidi hivyo kupelekea kuondoa dhana ya kusaidia kupambana na ugonjwa.


Ukweli na udhaifu wa Kundi la wasiokubaliana na chanjo ukoje?

Ukweli: Kundi hili linaweza kuwa sahihi kwa namna moja ama nyingine.kwa maana ya kwamba.ni ukweli kuwa kuwepo kwa chanjo nyingi,ambapo baadhi ya wazalishaji wa chanjo hizo wamekuwa wakibeza chanjo zinazozalishwa na wazalishaji wengine.Hii inaweza kuwa sababu ya 'walakini' wa hizo chanjo kutokana na kuingiliwa na 'mlengo wa kibiashara au kimaslahi zaidi' kuliko dhana inayotakiwa.Lakini pia utoaji wa chanjo unaweza kuingiliwa na 'Interest' za mataifa yanayotoa msaada wa chanjo hizo.Hivyo umakini unahitajika juu ya makubaliano na ubora wa hizo chanjo.

Udhaifu: Kundi hili kwa upande mwingine linaweza lisiwe sahihi ,kwa sababu wengine wenye mitazamo wa aina hii wameonekana pia kupuuza hata njia nyingine za kujikinga mbali na chanjo mfano kuepuka misongamano isiyoya lazima,uvaaji barakoa nk.Hivyo inawezekana msimamo wao kwa upande mwingine usiwe na maana ikiwa wanashindwa kufuata njia nyingine za kujikinga ilihali ugonjwa upo.Lakini pia Viongozi wa dini na waombaji ambao wamekuwa wakiomba,inawezekana kuwa hatua zinazochukuliwa kama vile utafutaji wa chanjo,ni majibu ya maombi yao kwa Mungu wao.


Hitimisho:

Ni muhimu sana kuwa na taarifa sahihi,ili ziweze kukusaidia kufanya maamuzi sahihi. Lengo la makala haya si kuchochea watu wachanjwe au wasichanjwe,isipokuwa ni mtazamo halisi wa mwandishi juu ya kile kinachoendelea.ambacho kinaweza kuwa na athari mbeleni
 
Kwangu mimi hiyo kitu hapana .Watu wana hidden agendas zao
Mkuu.
Nimekuelewa .

Ingependeza zaidi kama ungetoa mfano wa hidden agendas . ili kusaidia kukuza uelewa miongoni mwetu.Ili kama zipo unazozifahamu watu waelewe,tusibaki kuzikubali au kuzikataa pasipo kuwa na sababu za msingi.
 
Karibuni wadau

Usisahau ku'vote' na kutoa mchango wako kwaajili ya kuboresha maada ili kukuza uelewa utakaosaidia kuamua miongoni mwetu.


Usisahau,kutoa sababu yenye mantiki kwa kile unachokiamini kwenye mchango utakaoutoa ili kukuza uelewa
 
wagonjwa wa,
1.KISUKARI
2.PRESHA
3.MOYO
4.SARATANI
5.UKIMWI
wagonjwa wa maradhi hayo wanapaswa wachue tahadhari sana maana Corona itatumaliza sana.
 
Nimesikia baadhi ya wadau wanaokataa chanjo wakisema changamoto inayowafanya wasichanje ni ile kuwa "chanjo bado iko kwenye majaribio".
Wanadai hawataki miili yao kuwa ya majaribio,
Kuna ukweli kwenye hili?
 
Back
Top Bottom