Katika vitu vilikuwa vinaogopwa enzi ya Nyerere.........!!

Ole wako usiende mafunzo ya Mgambo
Umalize form 6 au chuo usiende JKT utajuta!!
Gari za wizara unatakiwa mnunue Bedford,landrover,tractor ford Bus za wafanyakazi ni Layland arabion au CD!!(nyuki)
 
ukiwa na mabob marley kichwani ni lazima uwe na kibali....la sivyo....mbona utajibeba....
 
Wanafunzi walikuwa hawaruhusiwi kupanda mabasi kwenda shule, hata za hapa mjini, ilikuwa ni kwenda na kurudi kwa miguu, ole wako ukutwe ndani ya basi na sare zako za shule!
 
watoto walikuwa hawaruhusiwi kupanda ndege, ole wako ajulikane ulimkatia mwanao tiketi ya ndege, utajieleza ukiwa lupango
 
1:Ole wako siku hiyo mkuu wa kaya anapita kijijini kwenu afu usiwepo barabarani,utajibeba. Afu akipita hasimami wala kupunga mkono. Utasikia keshapita,ilhali mmemsubiri toka asubuhi hadi saa 10 jioni no msosi!
2: Dawa kwenye zahanati zetu zilikuwa zinaletwa kila tarehe 1 ya mwezi. Kuanzia tarehe 2 kila mwanakijiji mgonjwa. Ikifika tarehe 5 bado hujaumwa utajibeba. So ilikuwa lazima kuumwa,ili familia iwe na stock ya dawa kwa mwezi mzima. Maduka ya dawa yalikuwa wilayani tu. Private health centre zilikuwa za mission,nazo ziko huko mijini na vijiji vichache vyenye bahati.
 
ole wako ukiwa mwanafunzi usitoe mchango wa mbio za mwenge, mchango wa UPE au UMISHUMTA utaenda kusomea nyumbani kwenu sio shuleni.
 
Ole wako ufungue redio ya kulima yumbani bila idhini ya baba au mama, utajuta kuzaliwa
 
Baiskeli lazima iwe na plate no vipat vya mviringo!!

na ilikuwa inalipiwa kodi kaka, ole wako ukutwe unaendesha baiskeli ambayo haijalipiwa kodi na mgambo wa kijiji, utaibeba kichwani hata ni umbali wa 5km, mgambo alikuwa anaheshimika sana
 
Baiskeli lazima iwe na plate no vipat vya mviringo!!

na ilikuwa inalipiwa kodi kaka, ole wako ukutwe unaendesha baiskeli ambayo haijalipiwa kodi na mgambo wa kijiji, utaibeba kichwani hata ni umbali wa 5km, mgambo alikuwa anaheshimika sana
 
Enzi hizo walimu ndiyo walikuwa na uhakika wa kunywa chai kwakuwa ndiyo waliokuwa matajiri
 
. Ole wake mwanafunzi atumwe na mwalimu wake aende anatembea badala ya kukimbia.
 
Piiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii...! Mikingamo ni sauti ya umma, tuambie, wapo wapi na wanafanya nini, kuendeleza rushwa magendo na kudhurumu mali ya umma....!

Ole wako ukamatwe na askari unaendesha gari siku ya mwisho wa wiki (weekend), jumamosi na jumapili na uku huna kibali cha kuendesha gari ziku hizo, utajuta.

Ole wako saa kumi na mbili jioni ikukute Kawe na wewe unaishi Mbagala, utatembea kwa mguu...!

Ole wako ugombane na mjumbe wa nyumba kumi, na siku ya mgawo wa duka la kaya ifike, ndio utamjuwa yeye ni nani.

Ole wako usisimame pale mwimbo wa taifa unapopigwa kwenye jumba la senema (New Chox, Avalon, Cameo, Odeon, Empire, Empressna Drive inn Cinema), utakoma kulinga.

Ole wako uingie kwenye jumba la dansi wanapopiga Msondo Ngoma na kisha ukanyage kivuli cha bausa, utamtambua yeye nani.
 
Bendi zote za dance zinapomaliza show, lazima zipige mwimbo wa "♪♯♭Chamaa ♪ chetuu♪ cha Mapinduziiii♪ chajenga nchii x2 ♪♯♭"
 
- Kumiliki 504 peugeot utajuta unashindana na rais
-Sinema iwashwe katikati ya wiki...utakoma
-Mfanyakazi wa Serikali kujenga...utachunguzwa pesa umetoa wapi
-Kula bar..bar zilikatazwa kupika watu wakale kwa wake zao
-Kwenda na msichana ambaye si Mkeo gesti...utaulizwa maswali mpaka ujikojolee
hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa loh!
 
Back
Top Bottom