Katika vita ya ufisadi na ubadhirifu, nasimama na Rais Magufuli. Ameanza Kebwe, afuate Makonda

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,193
25,504
Kiukweli, Rais Dr. John Pombe Magufuli anaendelea kujipambanua kimaneno na kimatendo katika vita dhidi ya wizi wa mali za umma, ufisadi na ubadhirifu. Hata kabla ya kuchaguliwa kwake mwaka 2015, Rais Magufuli aliahidi kushughulika na ufisadi kwa nguvu zake zote kivitendo. Hatimaye, hata Mahakama ya Mafisadi ilianzishwa.

Pamoja na kuwa vita ya ufisadi kwenye Serikali hii ya awamu ya tano imeasisiwa na inasimamiwa na Mhe. Rais, viongozi katika kila ngazi za kiutawala wanao wajibu wa kuipigana vita hii kwa nguvu na maarifa yao yote. Tena, viongozi hao wana nyenzo zote za kupambana na wizi, ufisadi na ubadhirifu kwa mali za umma. Wanavyo vyombo vya dola kuwasaidia.

Katika muktadha wa kuwajibika, unapotokea wizi, ufisadi au ubadhirifu mahali popote, kiongozi husika anapaswa kuwajibika ima kwa kujiondoa mwenyewe au kuondolewa na aliyemteua. Hivi karibuni, Waziri Mkuu alifanya ziara mkoani Morogoro. Akaona, kuusemea na kuukemea ubadhirifu wa kutisha. Aliyekuwa Mkuu wa mkoa huo, pamoja na wengine, aliondolewa.

Mkoani Dar es Salaam, Mhe. Rais amekuwa shahidi wa 'harufu' za wizi, ubadhirifu na ufisadi kwenye Ujenzi wa Fukwe na Machinjio, kwa kutaja machache. Kinagaubaga, akaonyesha kukerwa na hali hiyo na kutoa maelekezo kwa wahusika. Ndani ya Dar es Salaam pia, kuna Mkuu wa Mkoa na watendaji wengine. Kulingana na kauli za Rais juu ya hali hiyo, Mkuu wa Mkoa anapaswa kuwajibika.

Kimsingi, katika vita dhidi ya wizi, ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma, nasimama na Rais Magufuli. Namuunga mkono kwa sababu nyingi ingawa nitataja tatu kubwa. Mosi, mimi ni mmojawapo wa walipakodi wa nchi hii. Ninapoyaona matumizi mabaya ya kodi yangu, naumia sana. Pili, kama mtanzania nina wajibu wa kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi yetu. Nafahamu kuwa Serikali ina wajibu wa kuratibu matumizi sahihi ya kodi yangu. Kupambana na wizi wa lulu hiyo ni lazima.

Mhe, Rais au Mtendaji Mwandamizi mwingine wa Serikali anapozungumzia wizi, ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma, lazima kuwe na wa kuwajibika. Ameanza Dr. Kebwe Stephen Kebwe wa Morogoro, afuate Paul Makonda wa Dar es Salaam.
 
Moja ya mambo yatakayomshushia credit Magufuli ni kumuacha Makonda aendelee kusurvive madarakani..hapa inabidi avae ngozi ya mamba amtumbue hata kupindi cha mwisho mwisho kuelekea uchaguzi 2020 ili kuwachezea danganya toto wananchi tu..hakika ataimbwa kama shujaabwa wakati wote katika historia ya nchi....
 
Makonda atapondwa leo, kesho atasifiwa.
Hivyo credibility ya kuvuliwa inamezwa na sifa atakazopewa.

Subiri uone.
Taraehe 21 aliwaambia waTanzania, pamoja na Rais Magufuli kwamba.....
Kuanzia sasa hato patikana ofisini, na ameamua kusimamia site na atafanya kazi usiku na mchana kwakuwa wasaidizi wake wamemuangusha na akapata aibu/fedheha kubwa mbele ya Rais
 
Kiukweli, Rais Dr. John Pombe Magufuli anaendelea kujipambanua kimaneno na kimatendo katika vita dhidi ya wizi wa mali za umma, ufisadi na ubadhirifu. Hata kabla ya kuchaguliwa kwake mwaka 2015, Rais Magufuli aliahidi kushughulika na ufisadi kwa nguvu zake zote kivitendo. Hatimaye, hata Mahakama ya Mafisadi ilianzishwa.

Pamoja na kuwa vita ya ufisadi kwenye Serikali hii ya awamu ya tano imeasisiwa na inasimamiwa na Mhe. Rais, viongozi katika kila ngazi za kiutawala wanao wajibu wa kuipigana vita hii kwa nguvu na maarifa yao yote. Tena, viongozi hao wana nyenzo zote za kupambana na wizi, ufisadi na ubadhirifu kwa mali za umma. Wanavyo vyombo vya dola kuwasaidia.

Katika muktadha wa kuwajibika, unapotokea wizi, ufisadi au ubadhirifu mahali popote, kiongozi husika anapaswa kuwajibika ima kwa kujiondoa mwenyewe au kuondolewa na aliyemteua. Hivi karibuni, Waziri Mkuu alifanya ziara mkoani Morogoro. Akaona, kuusemea na kuukemea ubadhirifu wa kutisha. Aliyekuwa Mkuu wa mkoa huo, pamoja na wengine, aliondolewa.

Mkoani Dar es Salaam, Mhe. Rais amekuwa shahidi wa 'harufu' za wizi, ubadhirifu na ufisadi kwenye Ujenzi wa Fukwe na Machinjio, kwa kutaja machache. Kinagaubaga, akaonyesha kukerwa na hali hiyo na kutoa maelekezo kwa wahusika. Ndani ya Dar es Salaam pia, kuna Mkuu wa Mkoa na watendaji wengine. Kulingana na kauli za Rais juu ya hali hiyo, Mkuu wa Mkoa anapaswa kuwajibika.

Kimsingi, katika vita dhidi ya wizi, ufisadi a ubadhirifu wa mali za umma, nasimama na Rais Magufuli. Namuunga mkono kwa sababu nyingi ingawa nitataja tatu kubwa. Mosi, mimi ni mmojawapo wa walipakodi wa nchi hii. Ninapoyaona matumizi mabaya ya kodi yangu, naumia sana. Pili, kama mtanzania nina wajibu wa kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi yetu. Nfahamu kuwa Serikali ina wajibu wa kuratibu matumizi sahihi ya kodi yangu. Kupambana na wizi wa lulu hiyo ni lazima.

Mhe, Rais au Mtendaji Mwandamizi mwingine wa Serikali anapozungumzia wizi, ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma, lazima kuwe na wa kuwajibika. Ameanza Dr. Kebwe Stephen Kebwe wa Morogoro, afuate Paul Makonda wa Dar es Salaam.
Hebu wakili msomi nieleweshe kwanza kitu hapa, budget ya kujenga coco beach ilipitishwa na madiwani chini ya Meya ambaye ndiye mwenye dhamana zaidi, je, mkuu wa mkoa anaajibishwaje hapo, angeingilia kupinga budget iliyopitishwa na madiwani?
Kama mkuu wa mkoa ndo anakosa, kwa nini asiajibishwe kwa kutumbuliwa? make imeonekana kuna kaharufu fulani ka rushwa.
 
kwa kujenga ghorofa moja kwa bilioni 14 eti?

Back
Top Bottom