Katika utawala wake, hayati Magufuli hakwenda New York kuhutubia UNGA, je tulirudi nyuma kiuchumi na kisiasa?

Hakwenda UN kwa sababu kubwa 2;
1. Kale pacemaker maarufu kama kabetri kalikuwa kana mfanya asiwe comfortable na usafiri wa anga, hasa safari ndefu
2. Lugha ya Malkia au English ilikuwa haipandi pamoja na kuwa holder wa FAKE PhD
Acha chuki za kishamba we bwege.
 
Mwendazake hakwenda UNGA katika miaka yake ya Urais wa JMT lakini bado hayo matatizo ya ajira, matundu ya vyoo mashuleni na madarasa hayakuisha. Kwa kutokwenda kwake imesaidia nini? Hongera SSH kwa maaumuzi yako sahihi ya kwenda kwenye forum za Kimataifa kubadilishana mawazo na dunia. Siyo Rais wa nchi unajifungia ndani ya nchi huku ukishauriwa na wajingawajinga kama Bashite, Polepole, Kibajaji, Babu Tale, Sabaya and the like. Mwisho wa siku agenda ya kujenga nchi inakufa na kubakiwa na agneda ya kutekana na kununua wabunge, madiwani na viongozi wa juu wa vyama vya upinzani.
 
Nitafurahi kama tunaweza ku discuss, bila kumbeza marehemu, exposure ni personal, sio transferable useme kwa vile Balozi Dr. Mahiga amekaa Marekani na kuzunguka dunia 20 years, hivyo baada ya kuteuliwa na JPM, anaihamishia hiyo exposure yake kwa JPM. Exposure ni kama dose, ili upate exposure, ni lazima wewe ndio uwe exposed na sio kuwakilishwa.

Mtu ujifungie chumbani kwako for 5 years huku ukituma watu wakuwakilishe, what do you expect?.
P
Umeulizwa Kikwete aliyezunguka Dunia nzima alipata exposure gani? mbona Mambo yaliaribika sana na Nchi kujaa ufisadi baada ya usimamizi wa mali za umma, kitu ambacho Magufuri pamoja na kutokuwa na exposure
 
Umeulizwa Kikwete aliyezunguka Dunia nzima alipata exposure gani? mbona Mambo yaliaribika sana na Nchi kujaa ufisadi baada ya usimamizi wa mali za umma, kitu ambacho Magufuri pamoja na kutokuwa na exposure
Wacha kujitoa akili, JK kafanya makubwa sana katika kujenga uchumi wa nchi. Hata huyo DIKTETA wenu wa Chato aliyakuta yamekamilika ndiyo akaanza kuyazindua
 
Miaka mitano yote akiwa madarakani tuliwakilishwa na mawaziri wa nje. Na hakuna mtanzania aliyeona labda tumepungukiwa kiuchumi. Zaidi ya kuona maendeleo kwenye sekta za afya, miundo mbinu na ukusanyaji mapato.

Safari hii tumewakilishwa na mkuu wa nchi. Je, ndio kusema taasisi kubwa kama Imf, Wb na taasisi Tanzu za UN zitaisadia Tanzania na kupaaa kiuchumi? Je haya madhila ya kukosa ajira, kukosa madarasa, kukosa maji na uvunjifu wa haki za binadamu vitaisha?
In fact kutokwenda kwake huko kulisababisha viongozi wengine wawe wanamsikia kwa mbali na tu na hivyo kuwa na hamu ya kumwona. Katika utawala wake tulipata hela za WB na IMF kama kawaida tu, ni hao viongozi wa IMF na WB ndio waliokuwa wanakuja kumwona
 
Neno la Mungu linasema' heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao'!

'Amelaaniwa amtegemeae mwanadamu na kumfanya kuwa kinga na moyoni mwake amemwacha Mungu'......kwa maneno rahisi(limelaaniwa Taifa ligemealo mataifa/Taifa mengine/lingine)

Hii ni kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja mpaka Taifa!
 
Hadi anafariki kama sikosei Uchumi ulikuwa umeshuka mpaka 4.7% na ndiyo maaana Mama alishindwa kupandishwa mishahara!
 
Kutaja namba ni rahisi sana kila mtu anauwezo wa kutaja au kuzitamka na kuandika. Lete reference au rejea ya hizo takwimu. Unapoongelea kipato kwanini wakati wa Kikwete Tanzania haikutangazwa kuwa nchi ya uchumi wa kati. Sina mahaba kama wewe unavyodhani. Naongea ukweli. Na katika viongozi ambao mimi uwa nawapenda kama yangekuwa mahaba ni ngemtaja Kikwete. Kwa sababu ndo ungozi ambao hata mimi naweza sema nilikuwepo.
Mlinganyo unaoufanya hauendani kiuchumi. Chukua thamani ya miradi ya magufuli linganisha na thamani ya fedha ya miradi ya hiyo ya hospitali ulizo zitaja. Hospitali alizojenga kikwete ni mbili, Mloganzira na Benjamini. Aloboresha huduma za hospitali hizo umemsahau kumtaja ununuzi wa vifaa na upanuzi. Hospitali kubwa ya Rufaa ya Mkoa wa Mara ambayo iliwashinda wengi ilijengwa na nani? Vituo vya afya nchi zima, achana na hizo hospitali kubwa mbili.
Unaweza linganisha thamani ya miradfi mikubwa, kama reli, bwawa la umeme, Madaraja makubwa baharini na ziwani, ununuzi wa meri mpya na vivuko, ujenzi wa makao mapya. Hivi thamani yake ndo utalinganisha na mloganzira. Magufuli aligusa kila sehemu ya mkoa.
Hata hayo mabarabara ni Magufuli alie simamia. Ni miradi mingapi ambayo ilishindikana japo walikuwepo Mawaziri. Kuvuta maji kutoka ziwa Victoria umekuwepo miaka na miaka lakini Magufuli akatekeleza.
Tuache wivu wa kike, Magufuli alikuwa zaidi ya Kikwete. Roho itakuuma lakini ndo ukweli. Unapoongelea thamani ya miradi. Wakati wa Kikwete, watoto wengi walishindwa kusoma ada mashuleni. Lakini leo kuanzia kwa Magufuli hakuna ada. Ati unakimbilia kutaja Mloganzira na Benjamini ambazo thamani yake hazifikii miradi ya Magufuli. Weye ndo unamahaba. Mie nampenda sana Kikwete na namheshimu.
Lakini nitaongea ukweli kuwa Magufuli alijitahidi.

Kiongozi sio Magufuli alijitahidi, sema alifanya mapinduzi ya maiaka 50 ijayo! Achana Na vijana wanajifanya wanaakili kumbe maarifa zero
 
Hata Kama Mayala hataki kukubali, Ila ukweli ni kwamba umempiga knock out

Ndombwindo unaupiga mwingi!

Mayala anacheza karata ati anajifanya kuzichanga ili nae aonekane kwenye teuzi walau za uDAS baada ya kujua Hangaya pia huwa anapitapita huku!
 
Tanzania ni sehemu ya dunia. Juhudi zilizofanywa na sukumagang kuitenga na dunia zilikuwa za kishetani!
 
Hata Kama Mayala hataki kukubali, Ila ukweli ni kwamba umempiga knock out

Ndombwindo unaupiga mwingi!
Hahaaaahaaa!!! Pascal Mayalla anatetea udhaifu, anaongelea exposure as if watu wapo gizani kiivyo, dunia yenyewe siku hizi ipo kinganjani.

Kutoka nje kwa Kikwete hakutufanya tuwe hata robo ya North Korea kwa Kim Jong ambaye hatoki kizembe nchini kwake lakini kwa technology sio wenzetu kabisa. Imagine Mpaka leo tunaomba misaada Cuba ambako kuna vikwazo toka enzi za mwalimu, jamaa hawapendani kabisa na Wamagharibi lakini maisha yanadunda tena zaidi ya jana, huku kwetu watu hawafikiri kabisa.
 
tukijaribu kusimamia hoja na sio ushabiki..

Exposure na kwenda pamoja na dunia ni jambo zuri kuliko kujifungia ndani, sio ujanja kutohudhuria hivi vikao kama mkuu wa nchi, uwepo wa UN na mambo kama haya una maana ndio maana ukawepo huo utaratibu...Dunia imetoka mbali na kufika hapa na taasisi hizi zina mchango wake kuhakikisha dunia iko hapa.....

UN ilianzishwa kwa madhumuni maalumu hapa duniani baada ya miaka ya nyuma dunia kuwa shaghala bhaghala na watu kujifanyia mambo watakavyo kiasi cha vita na mauaji kuwa mengi...uwepo wa UN angalau umeleta amani na ustawi duniani...Vikao vya marais hufanyika kuwaweka pamoja marais na nchi zao kujadili ya duniani na kuwa na muafaka na mambo mbalimbali..

Mfano sasa marais wote duniani wasiwe wanahudhuria hivi vikao...maana yake UN itakufa...UN ikiwa haipo unafikiri maisha yatakuwaje duniani hapa?
Safi sana umewaelewesha kama darasa la 2. Watakuwa wameelewa. Kwamba wote wakiweka wawakilishi au wasiweke kabisa, Itakuwa vp? Maana jamaa aliondoka na akili zao hata umuhimu wa UN hawajui. Wanachojua ni kula mahindi barabarani huku wanaongea.
 
Hadi anafariki kama sikosei Uchumi ulikuwa umeshuka mpaka 4.7% na ndiyo maaana Mama alishindwa kupandishwa mishahara!
Uchumi ushuke halafu world bank isifie na kusema kuwa uchumi umepanda hadi kiwango cha kati! Unatania wewe. Tamko la uchumi wa kati lilitolewa na world bank, halikutolea na serikali ya Tanzania wala CCM! Na wao hufanya tathmini ya miaka mtatu mfululizo kabla ya kutoa tamko hilo.
 
Anayefikiria kuwa Magufuli ndiye alituingiza kwenye uchumi wa kati, ni mjinga hasa, asiye na uelewa wowote.

Mkapa alipandisha per capita yetu kwa $400, Kikwete alipandisha per capita yetu kwa $380, na Magufuli alipandisha kwa $80. Nani alikuwa the weakest performer?

Projections za Mkapa, ilikuwa kwa vile Mwinyi alipandisha per capita $50, yeye kwa $400, anayefuata (Kikwete) akipandisha angalao kwa $800, na Rais anayefuata (Magufuli) angepandisha hata kwa $800 hiyo hiyo, Tanzania tungekuwa kwenye uchumi wa kati wakati wa awamu ya 5; tukiwa na per capita ya $2,400. Lakini mpaka leo tupo kwenye $1,100. Hatujafikia hata 50% ya matarajio ya Mkapa. Lakini wajinga wanashamgilia.

Ukweli ni kwamba, mpaka leo, Tanzania bado ni maskini sana, na mwanga haupo. Nchi kama Botswana ina per capita $18,110. Namibia $4,175, Madagasca $17,320 Ukiacha Madagascar iliyopata uhuru mwaka 1960, haya mengine ni mataifa yaliyopata uhuru baadaye sana baada ya Tanzania.
Hizo per capital za akina Mkapa na Kikwete zilisaidia nini Nchi? wakati wa Mkapa mashirika yote yaliuzwa pamoja na viwanda na migodi na nyumba za serikali,akaja Kikwete kamalizia kilichobakizwa na Mkapa na kuanza kutumbua kile alichokusanya Mkapa.Huyu unadharau kaongeza per Capital $80 kanunua ndege kumi, kafufua reli ambayo ilikuwa imeshindikana, kanunua meli mpya kila maziwa,katengeneza flyover , kajenga masoko ya madini,kanzisha CGR ,na mabwawa ya umeme ili Nchi iweze kujikwamua kwenye mikono ya matapeli, Magufuri anapata madarakani Muhimbili hata t-sc
Anayefikiria kuwa Magufuli ndiye alituingiza kwenye uchumi wa kati, ni mjinga hasa, asiye na uelewa wowote.

Mkapa alipandisha per capita yetu kwa $400, Kikwete alipandisha per capita yetu kwa $380, na Magufuli alipandisha kwa $80. Nani alikuwa the weakest performer?

Projections za Mkapa, ilikuwa kwa vile Mwinyi alipandisha per capita $50, yeye kwa $400, anayefuata (Kikwete) akipandisha angalao kwa $800, na Rais anayefuata (Magufuli) angepandisha hata kwa $800 hiyo hiyo, Tanzania tungekuwa kwenye uchumi wa kati wakati wa awamu ya 5; tukiwa na per capita ya $2,400. Lakini mpaka leo tupo kwenye $1,100. Hatujafikia hata 50% ya matarajio ya Mkapa. Lakini wajinga wanashamgilia.

Ukweli ni kwamba, mpaka leo, Tanzania bado ni maskini sana, na mwanga haupo. Nchi kama Botswana ina per capita $18,110. Namibia $4,175, Madagasca $17,320 Ukiacha Madagascar iliyopata uhuru mwaka 1960, haya mengine ni mataifa yaliyopata uhuru baadaye sana baada ya Tanzania.

Wacha kujitoa akili, JK kafanya makubwa sana katika kujenga uchumi wa nchi. Hata huyo DIKTETA wenu wa Chato aliyakuta yamekamilika ndiyo akaanza kuyazindua
Yapi aliyoyakuta yamekamilika na kuyazindua?
 
Not nécessarly, ile kutoka tuu na kutembea, unapata kitu kinachoitwa exposure, kukutana na kubadilishana mawazo na wengine kuna ku broaden your perspective, you won't ne the same, think the same, you will think differently.

Tena unaweza usiamini, akikutana na taasisi za human right wings, akirejea tuu, mara pap... DPP anapeleka Nolle na kumaliza hizi kelele !.
Wajameni, haya sasa ndio mambo haya.

Kuna vitu watu tulisema, japo tulibezwa sasa vinatokea na vinajidhihirisha.


Hapa nilisema kitu kuhusu Tanzania ya Samia compared na Tanzania ile, kiukweli kabisa, Tanzania tunakwenda kuwa na Tanzania bora, Tanzania njema na Tanzania nzuri kuliko Tanzania ile, kitu kinachohitajika sasa ni kumpa muda.

Hongera sana Mama Samia, una uwezo na unaweza kututoa hapa tulipo na kutufikisha kule tunapaswa kuwa.

P
Ongeza nguvu mdau Paskali. Awamu hii unaweza kukumbukwa.
 
Back
Top Bottom