Katika utawala huu chini ya CCM; Taasisi ya ukaguzi wa mahesabu, TAKUKURU ni usanii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katika utawala huu chini ya CCM; Taasisi ya ukaguzi wa mahesabu, TAKUKURU ni usanii

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Japhari Shabani (RIP), Mar 30, 2012.

 1. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #1
  Mar 30, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Hivi katika nchi yetu ambapo ufisadi na ufujaji wa mali na rasilimali za nchi kila taasisi za serikali na umma tunaweza kusema "TUNA TAASISI YA UKAGUZI WA MAHESABU?" Hayo madudu ya ubadhirifu na ufisadi yanayoibuliwa na taasisi hiyo katika mashirika ya umma na taasisi za serikali na Ikulu yenyewe HAKUNA HATUA YOYOTE INAYOCHUKULIWA.

  KATIKA UTAWALA HUU CHINI YA CCM. TAASISI YA UKAGUZI WA MAHESABU, TAKURURU NI USANII NA MZIGO KWA WALALAHOI, WANALIPWA MISHAHARA NA WANATUMIA PESA NYINGI MATOKEO HAKUNA.

  MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 2. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Unaumwa mdondo wewe
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Mar 30, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu mbona umeiweka vizuri hiyo post yako hapo mwanzoni lakini mwishoni unaharibu. Hapa tatizo siyo Taasisi ya Ukaguzi wa Hesabu (nadhani una maana ya NAO/CAG). Kwa upande wao wanatekeleza majukumu yao na wanaibua ufisadi kama ulivyosema jukumu la kuchukua hatua ni la serikali. Taasisi ya Ukaguzi haiwezi kukagua na kuchukua hatua. Hivyo basi yenyewe inatimiza majukumu yake.

  Suala la TAKUKURU lina matatizo ya kimuundo. TAKUKURU haina independence na hata mkuu wake hana independence na security of tenure kwa maana kwamba Mkuu wa Nchi anaweza akamfuta kazi wakati wowote bila kujadiliana ama kuulizwa na mtu awaye yote. Nadhani ili hii Taasisi iwe effective inatakiwa iwepo kikatiba na iwe huru na siyo uhuru wa kupewa na mkii kwenye hotuba bali uhuru wa kikatiba.
   
 4. c

  collezione JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Umeongea point sana. Na hiki ndo nachosema kila siku.
   
 5. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  kweli. rejea ushuhuda wa boss wa takukuru uliovujishwa na wikileaks
   
 6. R

  Rwiai Member

  #6
  Mar 30, 2012
  Joined: Jul 17, 2009
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Umetoa hoja iliyoenda shule, big up
   
 7. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #7
  Mar 30, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu ndiyo maana nikasema"KATIKA UTAWALA HUU CHINI YA CHAMA TAWALA CCM"Sina tatizo na tatizo na hilo la kuwepo kwa NAO/CAG au TAKURURU lakini taasisi hizo katika utaratibu uliopo na utawala uliopo hata wafanyekazi vizuri kiasi gani tatitizo linabaki palepale.Kama taasisi hizi zitafanya kazi kwa utaratibu mwingine na utawala makini ZINAUMUHIMU WAKE Lakinini kwa sasa kama zilivyo ni USANII.
   
 8. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2012
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mimi nadhani ndio mana jamaa akasema kuwa ni USANII mtupu. Hawa jamaa wanalipwa mishahara ya bure kwa sababu kazi zao hazina maana. Hata wanapoibua ufisadi, mpaka mkuu wa nchi aamue. Kama rafiki yake ndiye amekamatwa na ufisadi, anaweza tu akaamua kuwa hakuna tatizo. Ndio mana TAKUKURU ilishindwa kuibua ufisadi kwenye RICHMOND kwa sababu raisi alikuwa anahusika. Mpaka kamati ya bunge ambayo hata ilikuwa haina wala haikutegemewa kuwa na wataalamu wakagundua ufisadi, ila TAKUKURU pamoja na wataalam wao walishindwa kugundua. Au suala la Jairo, CAG pamoja na wataalamu aliokuwa nao alishindwa kuona ufisadi, lakini kamati ya bunge ikaona. Nchi hii ina matatizo mengi. Hawa jamaa wameshindwa kazi kwa sababu ya madaraka makubwa aliyopewa raisi. Imagine bunge kupitia kamati ya serekali za mitaa inaona ufisadi mkubwa kwenye halimashauri nchini, lakini TAKUKURU na CAG wanashindwa pamoja na wataalamu wao wote walio nao. Aheri wakazivunja hizi taasisi ili kuwe na independent body kabisa lakini kwa mfumo tulio nao, ni ngumu kupunguza ufisadi
   
 9. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Kimsingi naona kama mnahoji ufanisi na mchango wa taaluma ya Uhasibu katika kuimarisha utawala bora na udhibiti wa rasilimali za Taifa letu au nakosea?

  Kama ni hivyo, nadhani kuna utaratibu wa hawa wahasibu kufanya kitu kinaitwa Quality Review, tunaweza kudodosa pale NBAA kama huyu CAG ameishafanyiwa Quality Review, sababu kwa kweli hata mimi siridhishwi na utendaji wao?

  Haiwezekani katika taifa ambalo karibia wananchi wote wanalalamika kwamba rasilimali za Taifa zinaliwa na wachache huyu CAG hajawahi kutoa report yoyote inayoreflect perception ya UMA wa watanzania, report zake zote ziko very light,
  ameng'ang'ana na taarifa za fedha za Halmashauri za Wilaya kila kukicha. kuna report aliwahi kutoa ya halmashauri ya wilaya eti issue kubwa ikawa ni kwamba Halmashauri haijatumia pesa ilizopewa. what a finding?

  Natambua kwamba kuna jinamizi la kisiasa linawafanya washindindwe kutekeleza wajibu wao vizuri, cha hajabu wao wenyewe hawajawahi kukiri kwamba Muundo wa taasisi hiyo na namna unavyowajibika kwa Bunge, Rais na Kwa UMA mzima wa watanzania unawakwaza kwenye utendaji kazi wao. Tuwasaidieje sasa, na kitu cha hatari zaidi ni kwamba na CAG amekwisha kuwa na tabia zote za kisiasa, hata alaumiwe na kupigiwa kelele vipi you will never see him come out to clear the dust, anauchuna tu utadhani LOWASA.
   
 10. J

  JacksonMichael JF-Expert Member

  #10
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 339
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  03_12_jveg0j.jpg
  Nimemkubali huyu wa kushoto anaonyesha heshima kwa JK
   
 11. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #11
  Mar 30, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Nakujua, unawapenda sana watu wany'onge na wanaoamini katika kubebwa bebwa
   
 12. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #12
  Mar 30, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu tatizo ni muundo wa vyombo hivi: Kwa TAKUKURU ni suala la Independence ya Taasisi yenyewe na viongozi wake. Hapa hata uje utawala gani bila hili suala kuwekwa kwenye katiba itakuwa bado kuna matatizo.

  Kuhusu CAG suala hapa ni reporting structure; CAG anapeleka wapi Report yake? Ingekuwa vyema kama angepeleka moja kwa moja Bungeni na kuiwasilisha mbele ya wabunge na siyo kwamba ipitie kwa Rais ndio iende bungeni. Kama unafuatilia mambo ya ukaguzi utagundua kwamba katika sekta binafsi hapo mwanzo wakaguzi wa ndani walikuwa wakiripoti kwa Mkurugenzi Mkuu (CEO) ambaye ndiye mwajiri wao. Baada ya mambo kadhaa kutokea huko Duniani likaja suala la Utawala Bora na hapo sasa hawa wakaguzi wa ndani wakawa wanaripoti kwenye Bodi ya Wakurugenzi (oversight) na siyo CEO. CAG wetu japo si mkaguzi wa ndani lakini kuripoti kwa CEO (President - Executive) si suala la busara.

  Haya ni mambo ambayo yanatakiwa yawekwe kwenye katiba kinaga ubaga kila mtu ajue wajibu wake bila kuingiliwa na siasa.
   
 13. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #13
  Mar 30, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu hatututofautiana katika hilo,kabla ya mapungufu uliyoyataja hayajapatiwa ufumbuzi.TAASISISI HIZO ZINABAKI KUA USANIII.
   
 14. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #14
  Mar 30, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Mkuu, hivi vyombo vimeundwa kwa mjibu wa sheria tena huyo CAG yeye ndio kabisaaa yupo kwa mjibu wa Katiba, sasa ukizema hivi vyombo ndio usanii nashindwa kukuelewa.

  Ni lazima tuwe na vyombo hivi hatuwezi kuviepuka, tunachoweza kufanya ni kuvibarishia reporting chains n.k lakini haatuwezi kuviondoa kama ambavyo tunatakiwa kufutilia mbali nafasi za wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya.

  Hivyo Basi, Advocate Jasha yuko sahihi kabisa anapoattach mapungufu katika utendaji wa vyombo hivi na Chama cha Mapinduzi ambacho kila mtu, kuanzia mahouse girls mpaka nyumba ndogo zetu zinajua kwamba ndio Mlozi anayewatuwangia, hatushine hatupendezi sababu ya chama hiki kimoja.
   
 15. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #15
  Mar 30, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Tunahitaji katiba mpya. Katiba ambayo inazipa uhuru Taasisi hizi kufanya ukaguzi na uchunguzi bila kuingiliwa na Wanasiasa. Katiba ambayo inatamka Wakubwa wa Taasisi hizi wataomba kuongoza taasisi hizi na kufanyiwa usahili na tume maalumu, na baadae wathibitishwe na bunge. Katiba ambayo itampa meno CAG anapobaini madudu katika kaguzi zake awapeleke watuhumiwa mahakamani yeye mwenyewe kwa sababu ushahidi anao.
  Tumechoka kusikia kila mwaka CAG anabaini madudu na bado watuhumiwa wanatamba.
   
 16. J

  JacksonMichael JF-Expert Member

  #16
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 339
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu yaani unataka wati wamdharau Prezzdaaa
   
 17. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #17
  Mar 31, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Hiyo picha inaujumbe gani wa heshima kwa Rais, huko kujikunyata? heshima haipimwi kwa body language wala maneno ya mdomoni wala haya mnayotype hapa.

  Kama wewe na wenzako mmengekuwa mnamuheshimu Rais mngemlindia heshima hiyo kwa kumueleza yeye na wasaidizi wake ukweli, lakini mnachokifanya sasa kwa kumshangilia katika kila maamuzi mabovu anayoyafanya na yale yanayofanyika mbele za macho yake kwa sababu tu mnachumia matumbo yenu mwisho wa siku huyu atakuja kuwa rais mstaafu asiyeheshimika kuliko marais wastaafu wote waliopo na watakaofuatia baada yake.

  Moyo wangu umejielekeza kumuheshimu na kumuenzi Rais wangu, hata Rais ambaye atakuja 2025 kabla sijamfahamu ninatambua heshima kubwa niliyoihifadhi kwa ajili yake, lakini nafsi ya ubinaadamu inanizidia nguvu, uzaifu wake wa kutuongoza umenitia ny'ongo, Kikwete ameniondolea uwezo wa kumuheshimu.
   
 18. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #18
  Mar 31, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu uko sahihi kabisa. Hapa ni suala la katiba ambayo itavipa hivi vyombo pamoja na viongozi wake uhuru. reporting structures zibadilike, wapewe presecutorial powers, kuwe na security of tenure, nk. Hivi vyote dawa yake ni katiba. Mbona jirani zetu wameka utaratibu mzuri sana wa kuwapata wa vyombo hivyo pamoja na kuwapata viongozi wao? Kwani wao waweze wana nini na sisi tushindwe tuna nini?
   
Loading...