Katika ulimwengu wa kujenga na kudumisha demokrasia,kukimbizana na wapinzani,ni kukaribisha lawama kimataifa

Ntozi

JF-Expert Member
Feb 1, 2021
226
299
Ukifuatilia suala la Mbowe tangu akamatwe na kufunguliwa kesi mahakamani,kumekuwa na lawama nyingi Sana Kwa serikali yetu na hasa juu ya utendaji kazi wa jeshi letu la polisi.
Kitendo cha maofisa wa balozi za nje kuhudhuria mahakamani kufuatilia kesi ya Mbowe,ilikuwa ni kiashiria kibaya sana Kwa nchi yetu kiasi cha kutia Shaka juu ya demokrasia yetu.
Pamoja na kwamba Mbowe ameachiwa Kwa maelekezo ya DPP,lakini tumewapa watu mashaka mengi juu ya namna tunavyosimamia demokrasia yetu.Washauri wa viongozi wetu na wasomi wetu waliopewa dhamana ya uongozi katika maeneo mbalimbali,yafaa wadhihirishe usomi wao,wamtangulize Mungu na kuachana na UBINAFSI na UNAFIKI ili waweze kushughulika na mambo yenye maslahi mapana ya nchi badala ya kupandikiza chuki katika mioyo ya watu.Mungu ibariki Tanzania.
 
CCM isipocheza faulo maana yake watafute kazi nyingine. Muulize Makonda hiyo maana yake ni nini? Hawawezi shinda uchaguzi wowote bila faulo...
 
Back
Top Bottom