Uchaguzi 2020 Katika Uchaguzi huu, WAZALENDO tutawashinda MABEBERU

Team JPM

JF-Expert Member
Nov 11, 2018
1,074
1,608
Uchaguzi mkuu wa mwaka huu ni mchuano baina ya Wazalendo tunaoipenda nchi yetu, tuliotayari kuzilinda rasilimali zetu dhidi ya Mabeberu na mawakala wao.

Kwanini Mabeberu wanachuana na Wazalendo katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu?. Tafakari sababu hizi kumi kisha uchague upande wa kuunga mkono

1. Hatua za serikali kupitia mikataba ya madini ili kulifanya Taifa linufaike na mapato yatokanayo na madini. Serikali ya awamu ya tano ilipeleka muswada bungeni ili kurekebisha vifungu vya sheria hiyo na kusababisha faida kwa nchi kwa kuwataka wawekezaji ktk madini kuigawia hisa serikali. Jambo hili limeleta faida na mgodi wa Barick umelipa bilioni 100 kama gawio. Jambo hili limewaudhi Mabeberu hivyo wametengeneza vibaraka wao na kuwaunga mkono katika uchaguzi huu

2. Hatua ya serikali kujenga Ukuta wa mererani ili kuzuia utoroshaji wa madini ya Tanzanite. Awali, madini haya yaliwanufaisha Mabeberu kupitia Kenya, afrika kusini na India ambako wamewekeza. Kwa sasa faida ya Tanzanite inabebwa yote na watanzania, hili limewauma sana Mabeberu.

3. Hatua za serikali kukabiliana na Korona na kuishinda, limewaudhi Mabeberu. Serikali ilizuia lockdown na kuruhusu shughuli za uzalishaji Mali na huduma ziendelee. Serikali pia ilibaini mchezo mchafu katika vipimo vya Korona. Hili limewakera Mabeberu
4. Hatua za serikali kufufua Shirika LA Ndege (ATCL) na Kampuni ya simu (TTCL) kumedumaza biashara kwa makampuni ya kibeberu hivyo kuibua chuki dhidi ya serikali.

5. Hatua ya serikali kudhibiti biashara ya dawa za kulevya kumepunguza faida ya biashara hizo kwa Mabeberu hivyo kujenga chuki

6. Hatua ya serikali kudhibiti ujangili wa tembo na wanyama hai kumepunguza malighafi muhimu kwa viwanda vya Mabeberu hivyo kuichukia serikali.

7. Hatua ya serikali kukemea vitendo vya ushoga nchini kumewaudhi Mabeberu

8. Hatua ya serikali kudhibiti safari za nje kwa viongozi kumeua soko LA Ndege pamoja na Hotel na mabenki ya Mabeberu hivyo kuzua chuki

9. Mkakati wa serikali kuhimiza watu kuchapa kazi, kudhibiti rushwa na kudhibiti mapato ya kodi kumekuza uchumi na kupunguza utegemezi hivyo kuwakera Mabeberu

10. Msisitizo wa serikali katika kudumisha amani, utulivu, umoja na mshikamano pamoja na muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ni machukizo kwa Mabeberu ambao wanatamani tuvutugane, kupigane ili watuuzie siraha na kupora rasilimali zetu.

Ni wajibu wetu kama taifa kusimama imara ili kuzilinda, kuzitetea na kuziendeleza rasilimali zetu kwa kuupigia KURA upande wa Wazalendo unaoongozwa na Mheshimiwa John Joseph Pombe Magufuli na Chama cha Mapinduzi

Tusidanganyike eti tumeminywa Haki na Uhuru, hizo ni ghiliba tu za Mabeberu.

Libya walidanganywa, leo hii wanajuta, wanatamani kumfufua Ghadafi lakini haiwezelani.

Mpigie Kura JPM, kwa Maendeleo ya Kweli.
Ahsanteni watanzania kwa kutuelewa na kuungana na wazalendo wengine ili kuwashinda Mabeberu na vibaraka wao
Ushindi wa Kishindo wa kura Mil. 12.5, ni salamu tosha kwamba Tanzania ni nchi huru, inayojiamulia maswala yake yenyewe.
Mgombea anayebebwa na Ubelgiji, Marekani au kwingineko hana nafasi katika Uongozi wa Tanzania.
 
Elimu ya uraia inapaswa ifundishwe kwa ufasaha! Maana neno uzalendo limebadilishwa matumizi!

Dozi moja ya ARv ni kuanzia $300 sasa nunueni cash kama mnavyojinasibu mnanunua ndege cash ili mjiondoe kuwapigia magoti wasiwape kwa masharti ili mdanganye mmepewa msaada!
 
Uzalendo gani mshatuharibia nchi yetu. Inatosha kaeni pembeni nchi yetu sote sio familia ya mtu kufanya mnavyotaka. Uzalendo ni kusimama na Taifa sio na Mtu
Nikweli, uzalendo ni kusimama na Taifa na sio MTU, Magufuli analitetea Taifa, sio MTU mmoja anaewatetea Mabeberu. Chagua Magufuli kwa Maendeleo ya Taifa
 
Hivi nchi hii Wazalendo ndo kina nani hasa?

Na mabeberu ndo wapi?

Yaani mmeamua kuwa watumwa wa meko na wapwa zake kweli? Na kwamba yeyote mwenye mawazo kinzani mnamuita anatumika na mabeberu...

Hovyo sna
 
..hoja za namna hii mngeachana nazo, zinawafanya muonekane hamnazo / wapumbavu.

..mnaonekana wapumbavu kwasababu mkiulizwa mabeberu ni nani hamuwezi kuwataja.

..zaidi, mnadai nyinyi ni wazalendo, sasa ni mzalendo wa aina gani anayeona haya kutetea HAKI?
Haki ya wanaume kuoana hiyo sio Sera yetu, sisi haki ni Elimu Bure, umeme wa uhakika, matibabu bora, amani, ulinzi na usalama na kuchapa kazi. Haki za mashoga, wizi wa rasilimali na ujangili Kazitafute Ubelgiji
 
Hiyo haipo tunataka maendeleo ya watu 28/ tunawakataa
Maendeleo ya watu ndiyo haya, Elimu bure yenye ubora, usafiri wa uhakika, umeme kila kijiji, Huduma bora za Afya, maji safi na salama, Amani, utulivu na usalama, uhakika wa chakula na kinga dhidi ya Mabeberu. Unataka maendeleo yapi wewe?, Wanaume kuoana?
 
Uzalendo gani mshatuharibia nchi yetu. Inatosha kaeni pembeni nchi yetu sote sio familia ya mtu kufanya mnavyotaka. Uzalendo ni kusimama na Taifa sio na Mtu
Wewe siotanzania, wewe ni mbelgiji wakala wa beberu.
 
Heri kushirikiana na mabeberu kuliko kuwa watumwa wa mtu na wajomba zakeh
Hamia Ulaya ukashirikiane na Mabeberu, hatuwezi kuuza utu wetu, amani yetu, rasilimali zetu na Uhuru wetu kwa Mabeberu. Tupo Tayari Kuulinda, Kuutetea na Kuuenzi Uhuru wetu
 
Hivi nchi hii Wazalendo ndo kina nani hasa?

Na mabeberu ndo wapi?..
Mawazo kinzani yenye kuuza Uhuru wa Taifa, kuhatarisha amani ys nchi, yenye kupora rasilimali za Taifa ni Chukizo kwa Wazalendo.
 
Kuzuia ujangili, utakatishaji pesa, wizi wa madini na ubadhirifu ndiko kuwanyonga wanyonge?. Chagua Magufuli, Chagua Maendeleo
Atutaki ukomunistu,utekaji, kubambikwa kesi,kuuliwa, ufisadi na upigaji dili wa Kodi zetu,udini ukabila na ukanda kwa ustawi wa taifa letu
 
Hamia Ulaya ukashirikiane na Mabeberu, hatuwezi kuuza utu wetu, amani yetu, rasilimali zetu na Uhuru wetu kwa Mabeberu. Tupo Tayari Kuulinda, Kuutetea na Kuuenzi Uhuru wetu
Mabeberu ni hoja za watu waliofilisika waliokufa fikra waliosoma sylbus za zamani,na sio kizazi cha sasa ambacho kina global vision huwezi kuwa na maendeleo kwa kuwa kisiwa
 
Back
Top Bottom