Katika taifa la 'Kidemokrasia' na lenye 'Hazina Kubwa' ya Viongozi, kuna ulazima gani wa Kiongozi wa taifa hilo kuongezewa muda wa madaraka?

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
May 27, 2016
5,416
7,828
Salamu!

Katika taifa linalo jinasibu kuwa ni la 'Kidemokrasia' na pia lenye 'Hazina Kubwa' ya viongozi (wa kila rika na jinsia), kuna ulazima ama umuhimu gani kwa kiongozi wa taifa hilo kuongezewa ukomo wa muda wa kukaa madarakani?

Nafahamu kuna watakaosema kuwa "kama wananchi wanahitaji aendelee kuwepo madarakani basi aongezewe muda" lakini Je, hakuna kabisa watu ama viongozi wengine wa kuweza kuendeleza yale 'mazuri' aliyofanya kiongozi huyo kwa maslahi mapana ya taifa?

Kuna yeyote aliyewahi kujiuliza swali kama hili, ama pengine ni mimi tu, lakini ningependa kupata michango mbalimbali kutoka kwenu kuhusiana na hili.

Kwa kifupi, nawakaribisha!
 
Mkuu wakati mwingine sio Kiongozi yule aliye madarakani hung'ang'ania kusalia madarakani bali ni wale walio wateule wako ambao wameghubikwa na tamaa ya mali na pia wakati mwigine maovu waliyoyatenda wakati wakiwa madarakani. Hivyo huogopa endapo atakuja mwingine basi lolote laweza kutokea juu ya madaraka yao. Mf ktk awamu ya tano ikatokea Kiongozi wa juu kawekwa pembeni nini kitatokea kwa wale wakuu fulani wenye jeuri??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu jamaa anapenda ajiongezee muda siyo kwa maslahi ya Taifa, Bali kwa maslahi yake binafsi na wapambe wake. Full Stop
 
Boss FRANC THE GREAT Hilo ndio KOSA wengi sijui hawalioni au wanaliona ila hawana uwezo kulisema na kulikemea, Je akija Rais mwingine akitaka nae ajiongezee miaka, Je atapitishwa??? Je tutakuwa na Taifa la Bora liende??? !!!
 
Back
Top Bottom