Katika Siasa, Kwa Vile Mama Kaondoka Bila Kuaga...

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Baba kwa maana ya Kiongozi Mkuu ana mawili ya kuchagua; kuufyata au kutoa makucha yake.

Na kwa vile hakukuwa na tofauti za masaa kushindwa kuliona tukio la kuapishwa kwa Mama, uzoefu unatwambia, kuwa Kiongozi Mkuu atachagua la pili ili kujijengea uhalali wake na wa chama kwa wanachama na wapenzi wa chama; Kutoa makucha.

Kuonyesha ACT kweli ni chama cha upinzani. Ndio maana yake, upinzani ni kutoa makucha kwa Serikali iliyo madarakani. Na kutakuwa na kauli za maonyo makali kwa wengine wenye kuwa na fikra za kufanya kama alivyofanya mama.

Yote hayo yatasahaulika baada ya siku kadhaa tu, tukisubiri mengine.

Ndio siasa ilivyo, wakati mwingine ni kama burudani.

Maggid Mjengwa.
 
Attachments

  • 4.jpg
    4.jpg
    20.2 KB · Views: 74
Natamani ningepata wasaa wa kumuuliza Mheshimiwa Mama, alijisikiaje siku Kongamano lilipozuiliwa na endapo na yeye yu tayari kuzuia makongamano Kilimanjaro
 
Baba kwa maana ya Kiongozi Mkuu ana mawili ya kuchagua; kuufyata au kutoa makucha yake.

Na kwa vile hakukuwa na tofauti za masaa kushindwa kuliona tukio la kuapishwa kwa Mama, uzoefu unatwambia, kuwa Kiongozi Mkuu atachagua la pili ili kujijengea uhalali wake na wa chama kwa wanachama na wapenzi wa chama; Kutoa makucha.

Kuonyesha ACT kweli ni chama cha upinzani. Ndio maana yake, upinzani ni kutoa makucha kwa Serikali iliyo madarakani. Na kutakuwa na kauli za maonyo makali kwa wengine wenye kuwa na fikra za kufanya kama alivyofanya mama.

Yote hayo yatasahaulika baada ya siku kadhaa tu, tukisubiri mengine.

Ndio siasa ilivyo, wakati mwingine ni kama burudani.

Maggid Mjengwa.
Ndugu majid njaa haina mbabe, wanasiasa wetu hawajazoea njaa Na wengi wameeingia ktk vyama Si kwa kufuata itikadi au sera Za vyama , wameingia kwa kuangalia nafasi gani anaweza kupata ktk chama."vijana wanasema sijui nitoke Vipi "
Kupitia CCM au Chadema au CUF . Ukiangalia hivyi vyama vyetu vya siasa vingi vina itakadi au sera zinazovyanana.
 
Mwanaone, na katika siasa hapo kuna waliozibwa midomo. Wale wenye kupita hata kwenye korido za kimataifa wakisema jamaa anawaminya wapinzani. Sasa kwenye aina hiyo ya teuzi wataambiwa anawaminyaje wakati ni mara ya kwanza katika historia ya nchi hii kwa wapinzani kupewa mikoa kuongoza na hata kuwa makatibu wakuu. Na ajira nyingine kwa wapinzani hazijafungwa!
 
Akiba ya Chama Tawala= ACT.. wacha wateuane eeeH..wacha wateuane ee..
 
Ndugu Maggid labda ungefafanua kuna mshkeli gani kwa mama kuwa na kofia mbili za Uenyekiti wa Chama na Ukuu wa Mkoa?
  • Cheo cha Mkuu wa Mkoa ni kidogo sana kwa hadhi yake?
  • Chama cha ACT ambacho kiliambulia kura laki moja tu ktk uchaguzi uliopita ni kikubwa sana kiasi kwamba mwenyekiti wake hawezi kuwa Mkuu wa Mkoa?
  • Dhana ya 'Trojan Horse' haiwezi kuwa ndo imemsukuma kukubali uteuzi? Yaan mama ameona ana nafasi nzuri ya kushauriana na rais na hivyo kubadili baadhi ya mambo yanayomkera maana sasa ana fursa ya kuongea na rais moja kwa moja?
  • Nafasi ya Mwenyekiti siyo ya kiutendaji (mtendaji ni katibu mkuu), ni kwa vipi kunaweza kutokea mgongano wa kimaslahi mpaka imlazimu mama kukataa uteuzi?
Hizi ndio siasa zetu waafrika, ukiwa mpinzan unaweza kupendwa sana na watawala au ukachukiwa sana. Yote mawili hayana heri.
 
Back
Top Bottom